Arusha: Kada wa CHADEMA kuvunja chungu kisa matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa

Arusha: Kada wa CHADEMA kuvunja chungu kisa matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa

Umenikumbusha mbali sana aisee. Hata 2010 ilibaki kidogo auze kwa Batilda ila wananchi wakajaa nje jengo la manispaa wakitishia kuchoma moto jengo endapo Lema atauza tena ubunge. Lema alikuwa kwenye hilo jengo.
Hilo hawataongea… the guys are blinded

Kwao ni mtume na nabii
 
Watoto wa 2000 wanatamani kuelewa hii tamaduni / dhana ya kuvunja chungu. Ni kitu gani? Faida na hasara zake ni zipi?? Tunaomba tusaidie uelewa Mshana Jr
 
Watoto wa 2000 wanatamani kuelewa hii tamaduni / dhana ya kuvunja chungu. Ni kitu gani? Faida na hasara zake ni zipi?? Tunaomba tusaidie uelewa Mshana Jr
Ni kama Albadiri. Ila hii ni ya kimasai. Ikishafanyika madhara hutokea kwa waliofanya makosa. Na huwa madhara yake ni kifo kwa aliyehusika.
 
Watoto wa 2000 wanatamani kuelewa hii tamaduni / dhana ya kuvunja chungu. Ni kitu gani? Faida na hasara zake ni zipi?? Tunaomba tusaidie uelewa Mshana Jr
Ni kafara la laana kwa waliotenda mabaya yasiyovumilika kwenye Jamii
Ni ibada ya kipekee ambayo mambo mabaya hutamkiwa wahusika mbele ya chungu maalum na mwisho chungu hicho huinuliwa juu na kuachiwa kijibamize ardhini na kuvunjika vipande vipande
Hii haina tofauti na kuvunja kioo
 
Alitangazwa wa Chadema, baadaye usiku akatangazwa wa CCM. Sasa wazee wa kimila Arusha masai wamesema wao hawana polisi, ni wa kwao, Mahakama ni zao, TISS ni yao. Kimbilio lao ni kuvunja chungu aliyetangazwa kiharamu afe.

sikiliza
Kumbe Chadema ndo wanauwa wàtu wa CCM kwa kuwàroga!
 
Inaweza isilete matokeo yanayokusudiwa. Lakini fikiria mtu unajitangaza kuwa kiongozi wa watu wanaokutakia umauti! Unajisikiaje unapowaza kuwa watu unaodai kuwa kiongozi wao wanakuchukulia kama maiti inayotembea! Ni fedhea iliyoje kwako kiongozi uliyejipachika na kwa familia yako!
 
Hatari sana na aibu kwa nchi na ni kwa kijana pendwa anaichafua sehemu husiak kwa heshima yake.
 
Hao ni wahuni waliozeeka. Chungu kwenye siasa inakujaje? Kama wako vizuri wailoge tume ya uchaguzi. Mambo ya kuvunja chungu ni kwa matukio mengine na sio siasa.
Kwan una wasi wasi? Kwan ni vibaya ikiingia kwenye siasa? Chungu si kinakula Kwa aliye dhulumu?
 
Ni kafara la laana kwa waliotenda mabaya yasiyovumilika kwenye Jamii
Ni ibada ya kipekee ambayo mambo mabaya hutamkiwa wahusika mbele ya chungu maalum na mwisho chungu hicho huinuliwa juu na kuachiwa kijibamize ardhini na kuvunjika vipande vipande
Hii haina tofauti na kuvunja kioo
Asante sana kwa ufafanuzi huu Mshana Jr
 
Huyo mzee azungushwe nchi nzima kwa gharama za chadema. Apasue vyungu nchi nzima.
 
Back
Top Bottom