Arusha: Kuvuka daraja hili utalazimika kulipia shilingi 400

Arusha: Kuvuka daraja hili utalazimika kulipia shilingi 400

Daraja hili limejengwa na vijana wawili wa kata ya Sinoni katika halmashauri ya Arusha mjini, baada ya eneo hilo Kukosekana daraja kwa miaka mingi.

Daraja hilo hulipiwa kiasi cha shilingi 200 kila avukapo mtu. Hivyo basi wananchi hulazimika kutumia kiasi cha shilingi 400 kila siku kupita juu ya daraja, na endapo mtu atakuwa hana kiasi hicho cha pesa hulazimika kupita kwenye maji.

Mto Themi ni kiunganishi cha kata tatu zote zipo ndani ya jiji.

View attachment 2627031View attachment 2627032
Vipi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha,Kuna ongezeko la bei ya kuvuka?
 
Naona makonda anakuja huko kuwanyoosha hao wanaojiita wadudu wavaa viatu vikubwa makofia mawani makubwa
😄

Ova
 
Lingine hili hapa lipo sinoni hukohuko unaweza kuvunja kichwa hapo.
Nb. Kuishi sinoni yahitaji roho ngumu sana
View attachment 2627034
Mwaka 2012 nilikuwa naenda kwa mshkaji wangu alikuwa anaishi daraja mbili.
Sasa tumetokea kwa huku engo hivi tulipofika hapo yule dogo niliyekuwa nae akavuka kwa kupita juu ya hilo bomba basi na mimi nikasema oii mbona rahisi tu nikapita asee nipo katikati miguu imejaa maji siwezi hata kunyanyua kuna wamama wapo kwa chini wanacheka mwangalie miguu asee..
Nikawaza labda nikae nitembee na matako nikiwa nimekaa lakini nikaona kukaa ndio itakuwa tiketi ya kuanguka nilijikaza kiume nikafika mwisho na sikuwahi kurudia tena kupita juu ya hilo bomba
 
Godbless Lema alikua Mbunge Arusha Mjini miaka kibao Ila ndo vile yeye kelele tu
CCM tangu Uhuru inakusanya Kodi matokeo ndiyo hayo au una maanisha ccm ikikusanya Kodi inampa lema akajenge madaraka,kuna watu wakati wa kuzaliwa mlitakuliza masandambwa na akili Iko hivyohivyo
 
SAFI KABISA, KAZI IENDELEE WAFANYE JERO JERO YAANI BUKU. SI WAO(WANANNCHI) KAZI YAO KUWAPA KURA CCM KILA MWAKA NGOJA TUWAKOMOE SASA.
 
1. "Tsh 200 kila avukapo mtu".

2. "Tsh 400 kila siku kupita juu ya daraja..."

Inasomeka ila haieleweki. Common sense draws blank.

Mfano, what if mtu akivuka mara 9 kwa kutwa? (Leave alone usiku)

Bakia na namba 1 pekee to make ur message well corresponding.

-Kaveli-
Hujaelewa nn hapo kwenda 200 kurudi 200
 
Back
Top Bottom