Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Kuna kabila limefanikiwa kuungana na kueneza chuki mbaya mitandaoni kuchochea mabaya kwa Sabaya. Inawezekana kweli kuna mapungufu ya Sabaya, lakini yamekuzwa mno (exaggeration)
Mbowe ana mapungufu mangapi? Ruzuku ya milioni zaidi ya 300 per month, imefanya nini ndani ya chama? Mbona kifo cha chacha Wangwe walipiga kimya?

Serikali iwe makini, ikifanya kazi kwa michecheto ya wanamtandao itaumiza watu, especially vijana wazalendo.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Hivi bado wachaga wana hasira baada ya mbowe kung'olewa ubunge?

Mimi nilifikiri hayo mambo yaliishaga tangu 2020?

Lakini hata hivyo, huyo mbowe kawa mbunge toka miaka ya 1990 huko, anapaswa kuachia ngazi apumzike!

Kila siku kugombea tu, amekuwa kama sultan! Duh.
 
View attachment 1808080

Bado wako wengi waliokuwa viongozi wa aina ya Ole Lengai Sabaya...

Ni aidha waadhibiwe kwa "natural death" kama Mwendazake au gereza likawafundishe namna ya kuwa watu bora na wenye manufaa ktk jamii..

Mwisho, hili ni swali la chemsha bongo tu...

Kati ya hawa waliochutama kichura, Ole Lengai Sabaya ni yupi? Je, ni wa kushoto kwako msomaji au kulia kwako....?

".......usilopenda kutendewa, basi vivyo hivyo wewe pia usimtendee mwenzako jambo hilo........"

Sasa tumuulize swali hili: Unalilia nini sasa Sabaya...??
Saambaya ni huyo ambae hajachana nywele
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikisikia tuhuma mbalimbali zikielekezwa kwa huyu mtu anayeitwa Ole Sabaya — Mkuu wa Wilaya ya Hai (by then).

Sijui ni ugoigoi wangu huu ama elimu duni niliyonayo inayonifanya nisielewe hasa kiini cha jinamizi linalomuandama huyu mtu?

Mwanzoni, nilikuwa namfahamu sabaya kama Kijana jasiri, shupavu, anayejiamini, na aliyefanya kazi chini ya falsafa madhubuti za Rais Magufuli za uchapa kazi na uwajibishaji wa mafisadi yaliyoitafuna nchi hii.

Kwa kadiri ya vyombo vya habari vilivyomripoti, alikuwa anaonekana ni kiongozi anayeshughulikia ujambazi kwa wakati mwingi - eg, ukamataji wa madawa ya kulevya, mabangi, fedha bandia nk...

Zaidi ya yote, alionekana ni kiongozi aliyehusika kwa kiwango kikubwa kukipaisha chama cha mapinduzi na kukiweka kwenye chati, huku akiwashughulikia wapinzani kwa namna za hapa na pale.

Hivi karibuni, baada ya Rais Magufuli Kufariki dunia, huyu Kijana amekuwa akizongwa na majinamizi yaliyoibuka kutoka pasipojulikana.

Kuna wale majasusi wa twitter (wenyewe wanaitwa Twirrah) ndio walikuwa vinara wa kuibua shutuma na tuhuma za hapa na pale.

Ukiachana na hawa majasusi uchwara wa twirrah, kulikuwa na jopo kubwa la multiple ID's Jamiiforums na kwenye mitandao mingine ambazo zilikuwa zinamuandama mpaka hapo aliposimamishwa kazi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hizi tuhuma za mitandaoni, kwa bahati mbaya, hazina ithibati yoyote.

Mimi binafsi huwa napenda kufuatilia mambo na kujiridhisha pasipo shaka kuhusu ukweli na uhalali wake. Sipendi kurukia rukia tu habari.

Kuna majasusi wengine kutoka twirrah wanasema sabaya kabaka wanawake mia mbili. Wengine wanasema sijui kalawiti makada wa chadema.

Stori zimekuwa nyingi sana bila ushahidi kuwekwa hadharani. Kila mtu anaibuka na lake.

Zamani nilisikia pia hata humu kuna majasusi (wanaitwa sijui TISS?) — Ningefurahi kama wangetujuza kwa hakika kuhusu tatizo alilonalo huyu mtu wa kuitwa Sabaya.

Kwa sisi wenye akili duni zisizoweza kuchambua mambo kwa ufasaha tumebaki kwenye mshangao bila kuelewa ni nini hasa tatizo!

Tunaangalia tu huko twirrah kila mtu anasema lake.
siku utakapoelewa maana ya jina la ID yako na tafsiri yake utaelewa ni nini hasa kinamuandana sabaya, mfano(sabaya ni mkatili sana)
 
Hahahaaaa...... Chadema mnashangilia kama mmeshinda ubunge vile!
Najaribu kuwaza leo Sabaya atakavyovuliwa nguo zote kwenye ukaguzi.... anaambiwa kujisaidia haja kubwa bila hata kubanwa.. anaambiwa kuchuchumaaa akiwa uchi wa mnyama mbele ya wale waliomuona boss wao.. tuliposema watu wanadhalilishwa wakafikiri yataishia kwa Chadema tu.
Heche
 
Back
Top Bottom