Hadi youtube zipo labda kama wewe ni mnufaika wa ukoo wao
Huyo rubbish Sabaya ni mzalendo???Serikali iwe makini, ikifanya kazi kwa michecheto ya wanamtandao itaumiza watu, especially vijana wazalendo.
Kama kuna kitu samia amekosa ni kuwafikisha mahakamani kada wa ccm kwa makosa ya kizushi kutoka wapinzani. Wana ccm wanakua na shaka nae sana huenda ni msaliti wa mstari wa tano hivyo anaenda kuharibu kile hayati magufuli alifanya. Yetu macho tuone jinsi samia ataenda ikabidhi ccm kwa wale fisadi enzi ya awamu ya nne.Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne, leo Ijumaa, wako mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.
Bado haijafahamika mashitaka yanayomkabili
=====
UPDATES:
=====
Arusha. Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.
Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.
Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.
Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.
Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.
Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.
Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
CREDIT: Mwananchi
Zaidi, soma: Thread 'Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18' Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18
Pia soma
1) Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake
2) Ole Sabaya akamatwa pamoja na mabaunsa wake. Ahojiwa na Vyombo vya Dola
View attachment 1807936
Ole Sabaya akitoka kwenye gari la Polisi akiwa kafungwa PINGU
View attachment 1807996
Ole Sabaya akiwa amechuchumaa mbele ya Mahakama
We nawe! Yan pamoja na Uhalifu alioufanya kuutenda bila kupepesa macho, Unataka apewe heshima hio heshima itoke wapi? Heshima ina taratibu zake, ukishaishusha haiwezi kupanda lazima nayo ikushushe.Kwayo kaa kwa kutulia ukisubiri mvua ya hukumu.Kwa kifupi serikali aitakiwi kuwa na tabia za kusutana, kumuonyesha kiongozi kwa namna hiyo ni kama inashabikia ushambenga huku wakijua Sabaya katika nafasi yake alijitengezea maadui wengi kwa sababu mbalimbali (zingine hizo hasira za watu wana haki nazo).
Kitendo cha kumshitaki ni salamu tosha kwa wengine kuna kesho, ila kudhalilishana ni unnecessary.
Asilimia kubwa ya post za humu ni moja sababu mahususi kwanini mtuhumiwa apewe walau heshima au kama atakutwa katika hali ya udhaifu iwe kwa bahati mbaya.
Lakini kitendo cha serikali yenyewe kutengeneza mazingira ya kudhalilisha mahabusu ambae alikuwa kiongozi na katika muda wake wa uongozi ametengeneza maadui wa kisiasa ni unethical to say the least.
Anyway huo ndio mtazamo wangu ata angekuwa ameshitakiwa Mbowe, ningetaka apewe heshima yake sio kumuweka kwenye mazingira ambayo baadhi ya wana CCM watumie picha kumdhalilisha.
Baada ya kusema hayo simlazimishi mtu kukubaliana na mtazamo wangu, maana kuna mijitu imeshaanza kunitukana khaa, kwani watu atuwezi pishana mitazamo bila ya matusi. Mijitu mengine sijui ikoje.
Nashindwa nikuambie nini pimbi wewe.Kama kuna kitu samia amekosa ni kuwafikisha mahakamani kada wa ccm kwa makosa ya kizushi kutoka wapinzani. Wana ccm wanakua na shaka nae sana huenda ni msaliti wa mstari wa tano hivyo anaenda kuharibu kile hayati magufuli alifanya. Yetu macho tuone jinsi samia ataenda ikabidhi ccm kwa wale fisadi enzi ya awamu ya nne.
Kwa takukuru hachomoki.Pole kwake na kwa familia yake kwa matatizo yaliyo mkuta.
sio uungwana kufurahia matatizo ya mwenzako.
Haki itatendeka, kama kweli alitenda basi tena atafungwa kama hakutenda ataachiwa.
We unauliza ushahidi hapa Jf kwani Mwendesha mashtaka wa serikali kampeleka mahakamani bila kuwa na sababu za kufanya hivyo? 18/June hudhuria Mahakamani.Ushahidi uko wapi?
Kila mtu anaweza kusema lolote mtandaoni!
Ushahidi wowote wa maandishi au nyaraka tafadhali? au picha?
Ukipanda mahindi huwezi kuvuna mpungaHivi haya yanayofanyika kwa Sabaya ni mapya yanayotakiwa kuja kulipiziwa au ni malipizi aliyoyafanya yeye kabla?
Katika zote hizo madai ambayo ni ngumu kuthibitisha ni ubakajiNi Martin M.M kupitia Twitter ambapo ameandika haya:
Hati ya Mashtaka ya SABAYA LAINI sana. ML kuna PLEA bargain. SABAYA ameteka, amebaka, amepiga watu misumari, amekata watu masikio, amevamia hoteli na maduka, amelawiti.. Vinginevyo tuelezwe tuhuma nyingine zitaongezwa. Mliokuwa mahakamani, prosecutor kasemaje? Police, act upon!
Na hayo ya plea bargain ni rahisi tu kuyamaliza.Katika zote hizo madai ambayo ni ngumu kuthibitisha ni ubakaji