Arusha: Lengai Ole Sabaya afikishwa Mahakamani kwa Uhujumu Uchumi, Utakatishaji Fedha

Kukosekana kwa hili shitaka ni wazi kabisa Sabaya ana kwenda kuwabwaga mahakamani maana hivi kweli watu watumie silaha kuiba simu na elfu 35,000 hahahaha

Kutumia vibaya ofisi ya umma ,kura rushwa ya milioni 90? Wizi wa kutumia silaha clip ipo mkuu na walalamikaji wapo,diwani alikuwa anataka kumtetea mwananchi wake ndio genge la sabaya likaamua kumtisha kwa silaha na diwani aliaambiwa aruke kwenye gari akimbie ila alijiongeza maana angekimbia tu wangemlima "njugu".

Sabaya hatoki leo wala kesho....Mashitaka yake ni hatari halafu plea bargain jiwe aliiweka kusudi kwa ajili ya kuwapora mali wafanyabiashara ila mama mambo ya plea bargain fedha za dhulumati hana...Sabaya anakaa ndani tu.
 
May be he was assassinated by Satan not human being
 
Aliyetembeza bakora Mbeya kapelekwa kwenye jiji kubwa zaidi, Mwanza.
yule alitembeza bakora mbeya, malipo yake ni kama hakutembezewa bakora na mkewe, basi nae akae mkao wa kulipwa.

Malipizi ni hapa hapa duniani. Toa fundisho kwa sabaya na wengine wengi.
 
Huyu bora akutwe na mashitaka akafungwe watu wataridhika akirudi huku uraiani atapotezwa kwasababu wengine aliowagusa nao ma-mafia vile vile...kwakuwa mtetezi wake hayupo watampa shida huku uraiani,hatokuwa na kiburi kama kile kwahiyo watamsurubu tu...
 
Naona hii itakuwa habari njema sana kwa wafuasi wa Mbowe.
Sasa watachekelea utafikiri jimbo la Hai watalipata tena.
By the way, Sabaya alipaswa kupewa tuzo ya heshima na CCM na siyo kushtakiwa. Huu ni usaliti kwa mpiganaji kama huyu.
Unakumutwa wewe. Basi mfuate huko mahabusu mkaolewe wote.
 
Auae kwa upanda atauwawa kwa upanga ndio shart lake sio sisi ndio vitabu vinavyosema!Tulia Mungu ajidhihilishe kwa ubaya kama alitenda!Kama hakutenda upanga utarudi na fidia atapata.Kuwa mpole ni mtuhumiwa bado.
 
Rugemalila na Habinder Sing Seth na wengine ambao hupelekwa mahakamani, huchuchumaa hivyo baada tu ya kutelemka kwenye gari na wakati wa kurudishwa rumande kabla ya kupanda gari. Mtuhumiwa ukiwa hauko kwenye motion (hutembei) unachuchumaa, hiyo ni kuimarisha ulinzi watuhumiwa wasikimbie. Watu wakiwa wamechuchuma hawawezi kukimbia. Mtu utakaye anza kusimama wakati uko kwenye amri ya kuchuchumaa utaonekana kwamba kuna jambo unataka kulifanya kuliko mkiwa mmesimama siyo rahisi kumgundua mtu mwenye nia ya kukimbia.
 
Kama kawaida naona watu wengi wanashangilia Sabaya kufikishwa Mahakamani. Inawezekana Kitakachoendelea au Mwisho wake ukawashangaza wanaoshangilia sasa.
 
Kada mkongwe wa CCM mzee Mgaya anasema aliyekuwa DC wa Hai mh Ole sabaya amevunja rekodi ya uongozi wa Umma kwa kutuhumiwa kufanya ujambazi wa kutumia silaha akiwa Ofisini kama Mwenyekiti wa Mlinzi na Usalama wa Wilaya.

Hii haijawahi kutokea tokea nchi ipate uhuru 1961.

Nchini China kosa kama hili adhabu yake imeandikwa ukutani ukishatiwa hatiani kila Mwananchi anaijua, amemalizia Mgaya.

Ee Msamehe huyu kijana hakujua alilokuwa anatenda.

Jumaa kareem!
 
Kama kawaida naona watu wengi wanashangilia Sabaya kufikishwa Mahakamani. Inawezekana Kitakachoendelea au Mwisho wake ukawashangaza wanaoshangilia sasa.
Lakini atakuwa amejifunza msemo wa wahenga kwamba cheo ni dhamana na kile kiapo ni cha muhimu!Mungu anaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…