Arusha: Mahakama yamkuta Lengai Ole Sabaya na kesi ya kujibu

Duh, utetezi unaanza kesho? Mapema sana wangemuacha hata ale weekend tu. Kwahio next week mbivu na mbichi zitajulikana?
Kwa Mbowe mnalilia aachiwe kinyume na sheria. Kwa Sabaya mnataka hata haki aliyonayo ya kisheria asipewe. Aachwe aendelee kusota gerezani. Kwamba ni mapema sana kumwachia!! Nyie wanachadema ni wanafiki sana. Si chama cha Demokrasia na hakijali haki za watu.
 
Ushahidi mzuri Sana sabaya amewaumiza watu wengi Sana lkn sasa ushahidi Hakuna,watu hawataki kuja mahakamani kutoa ushahidi
 
Kesi zote zinapaswa kuwa na mtiririko kama huu.

Ushahidi wote uandaliwe vizuri tena kimyakimya huku mtuhumiwa akiwa zake uraiani,akikamatwa na kufikishwa kortini pasiwe na hadithi za ushahidi kutokukamilika.
Mh. Jaji Biswalo Mganga enzi za u-DPP wake alikuwa kama anapinga hii procedure, sasa sijui sasa hivi ataendelea ku hold same position au ndio atakuwa mweledi zaidi.

Prof. Juma C.J kaongea sana hili swala, ila ni kama alipuuzwa/anapuuzwa. Kitu ambacho kinashangaza pia
 
Kwa Mbowe mnalilia aachiwe kinyume na sheria. Kwa Sabaya mnataka hata haki aliyonayo ya kisheria asipewe. Aachwe aendelee kusota gerezani. Kwamba ni mapema sana kumwachia!! Nyie wanachadema ni wanafiki sana. Si chama cha Demokrasia na haijali haki za watu.
Makosa ya sabaya yako wazi sana,na alishaanza kulalamikiwa na watu miaka mingi nyuma sema hatua ndo zilichelewa kuchukuliwa kwasababu alikua analindwa,na hata sasa anaweza akalindwa na wenye nguvu wakiamua.ila ugaidi wa mbowe ni sinema ile na iko wazi ata kwa kichaa.Kinachofanyika ni watu kutoa mawazo yao sasa hapo unafiki ni upi?.Siku zote ukweli ni mfupi na uongo ni mrefu.
 
Kwa Mbowe mnalilia aachiwe kinyume na sheria. Kwa Sabaya mnataka hata haki aliyonayo ya kisheria asipewe. Aachwe aendelee kusota gerezani. Kwamba ni mapema sana kumwachia!! Nyie wanachadema ni wanafiki sana. Si chama cha Demokrasia na hakijali haki za watu.
Umesoma nilichoandika? Mimi ndio nimesema ako na kesi kujibu? Ndio nilimwambia akapore watu??
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili Sylevester Nyegu, Daniel Mbura, hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea kesho Ijumaa Agosti 13, 2021...
Sabaya atafungwa ilikuhalalisha kumfunga Mbowe
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, na wenzake wawili Sylevester Nyegu, Daniel Mbura, hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea kesho Ijumaa Agosti 13, 2021...
Noma sana,
 
Makosa ya sabaya yako wazi sana,na alishaanza kulalamikiwa na watu miaka mingi nyuma sema hatua ndo zilichelewa kuchukuliwa kwasababu alikua analindwa,na hata sasa anaweza akalindwa na wenye nguvu wakiamua.ila ugaidi wa mbowe ni sinema ile na iko wazi ata kwa kichaa.Kinachofanyika ni watu kutoa mawazo yao sasa hapo unafiki ni upi?.Siku zote ukweli ni mfupi na uongo ni mrefu.
Katika utawala wa kisheria ni mahakama tu ndicho chombo cha kisheria cha kutoa hukumu dhidi ya malalamiko yoyote kwa mtu yeyote. Hakuna kitu kinaitwa 'makosa yako wazi' Yako wazi kwa nani na kwa kigezo kipi.

Ni mahakama tu ndiyo ina uwezo wa kutambua huo ' uwazi' wa makosa, siyo wewe wala siyo mimi. Hivyo tuache mahakama iwe huru kuamua kesi ya Sabaya na pia kesi ya Mbowe. Kiuhalisia huna uthibitisho juu ya nini Mbowe amekuwa akifanya mchana na usiku. Kama mke wake hawezi kuthibitisha hili, wewe ni nani usimame kusema Mbowe si gaidi. Mbowe si malaika.
 
Kwa Mbowe mnalilia aachiwe kinyume na sheria. Kwa Sabaya mnataka hata haki aliyonayo ya kisheria asipewe. Aachwe aendelee kusota gerezani. Kwamba ni mapema sana kumwachia!! Nyie wanachadema ni wanafiki sana. Si chama cha Demokrasia na hakijali haki za watu.
Kama weye ni mtu wa ARA nakuomba uende mtaa wa bondeni umuulize mtu yoyote pale sokoni kuhusu huyo Sabaya na duka la Saad Hajirini....utakavyosimuliwa utalia na utatokwa na machozi ya damu.
TUACHE SIASA ZA KIPUMBAVU KWENYE HAKI NA MAISHA YA WATU.
 
Duh, utetezi unaanza kesho? Mapema sana wangemuacha hata ale weekend tu. Kwahio next week mbivu na mbichi zitajulikana?

Makosa hayaangalii weekend na sheria pia haiangalii weekend. Tukimalizana na mbivumbichi za sabaya tunaendelea kupokea mbivumbichi za mbowe

Maendeleo hayana vyama
 
Kesi zote zinapaswa kuwa na mtiririko kama huu.

Ushahidi wote uandaliwe vizuri tena kimyakimya huku mtuhumiwa akiwa zake uraiani,akikamatwa na kufikishwa kortini pasiwe na hadithi za ushahidi kutokukamilika.
Nafikiri hili limeanza utawala huu mpya, hata ya Mbowe wamesema ushahidi umekamilika, kwamba walishindwa kumkamata mapema sababu ushahidi ulikuwa bado. Ila mimi kama nikizingua then nikijua napelelezwa nalala mbele
 
Kama weye ni mtu wa ARA nakuomba uende mtaa wa bondeni umuulize mtu yoyote pale sokoni kuhusu huyo Sabaya na duka la Saad Hajirini....utakavyosimuliwa utalia na utatokwa na machozi ya damu.
TUACHE SIASA ZA KIPUMBAVU KWENYE HAKI NA MAISHA YA WATU.
Ndiyo maana mahakama inasikiliza kesi hiyo. Waambie hao wa mtaa wa bondeni wakatoe ushahidi, badala ya kunisimulia mimi na nikaishia kulia, wamsimulie hakimu ili aishie kumfunga jela. Ndiyo utawala wa kisheria. Kinyume na hapo ni story za kunogesha vijiwe na kufanya 'hukumu' zisizozingatia haki za maisha ya binadamu
 
Back
Top Bottom