Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Heh! Mama Fatma kafunga safari kutoka Zanzibar hadi Arusha kumpongeza tu au kuna ujumbe mwingine kampelekea?
Mama Fatma Karume amefika Mkoani Arusha mapema Jumamosi ya Disemba 21, 2024 na kuongoza Dua maalumu ya kumuombea Kheri, afya njema na mafanikio zaidi Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akionesha kuridhishwa na Uwajibikaji wake na nia njema aliyoionesha kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha tangu kuteuliwa kwake kuongoza Mkoa huo Machi 30, 2024.