Jamaa alikuwa anafuatilia ukweli wa mgawanyo wa rambiramb na kupeleka rambarambi nyingine moja kwa moja kwa wafiwa bila kupitia "middle man/mtu wa kati(RC/serikali).Maana kuna kipengere kilisema chakula na vinywaji vya wageni wa meza kuu ilikuwa milioni 4.3(?),wakati hakuna mtu wa meza kuu aliyekula hata kidali cha bata mzinga,watu walimaliza kuaga wakaingia kwenye magari kukwepa mvua.Sasa hiyo milioni 4 ya chakula na vinywaji ilikuwajekuwaje?
Wafiwa walipewa milioni moja,na baadae wakahaidiwa kupewa milioni 2 na ushee zilizobaki,sasa maswali ikawa,inakuwaje rambirambi zinakuja nusunusu wakati zilitolewa kwa pamoja?
Walisema Serikali itagharamia safari na mazishi ya watoto,walimu na madereva.Lakini kwenye mchanganuo wanaonyesha kuwa pesa za rwmbirambi zilitumika kulipa madereva na magari ya usafiri,wakati kina Chambili,Kampuni ya Leopards na wadau wengine walichangi kama msaada,sasa hizo zilipoteaje?
Kudhihirisha chuki ya Kisiasa,siku ya msiba Gambo alitangaza CHADEMA kama Chama kimetoa shilingi milioni 5,Lakini kwenye mchanganuo wa jedwali lake,hajaweka CHADEMA kama chama kilichochangia,zaidi kawaweka UWT-Taifa,CCM mkoa wa Arusha nk...Sasa haya mambo ndio yanajenga machuki yasiyo na maana.
Wanamtumia Nyalandu kupenyeza "userikali" kwa kuwapeleka watoto marekani,Lakini ukiangalia website ya hawa jamaa,utaona kuwa wao walitaka siku ileile watoto wapelekwe US kutibiwa,lakini urasimu wa serikali na Gambo kwa "kiburi" kuwa serikali itawatibu kiliwachelewesha,mpaka wakatumia nafasi ya Makamu wa Rais alipoenda Hospital Mount Meru,wakawasakizia wale wamama wenye watoto kumsihi Mama Samia watoto waende nje kutibiwa kwa msaada wa Wazungu.
Halafu wanajidai kusema "Uongozi unaoacha Alama"...Hizo ni alama gani?au za chuki na visasi?Buree kabisaa