Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo maana kwa mimi, hajawai kufa polisi/mapolisi nikaumia! Najua hata Mimi Nitakufa siku yoyote niliopangiwa na Mwenyeenzi Mungu.Ni kweli mkuu,lakini nadhani wenye uwezo wa kushawishi mabadiriko hayo ni polisi wenyewe,kwasababu ndio wanachonganishwa na raia kila mara.
Yaani ukimchukua malaika siku moja ukamweka ndani ya CCM, siku ya pili utamkuta amebadilika na kuwa shetaniiMaccm ni majizi yaani hata rambirambi?
Aisee, maskini JF!Pesa ipo over 50m hiyo haijabaki!? Mnalalamikia kiasi kidogo mnachotamani mpewe ha ha aaaaa
Semeni mengine inatia aibu nchi yetu.
Hawa viongozi waliotokea uvccm wakisapotiwa ima kwa ima na mamlaka ya uteuzi wameutia aibu uongozi kwa kuleta visasi uongozini. Ukitofautiana nao ki mawazo umekuwa adui.Kutoa rambirambi inahitaji mfumo gani?
Unamtafuta mfiwa unamkabidhi rambirambi basi umemaliza.
Huko Arusha watoa rambirambi walitumia shule iwasaidie kuwakusanya wafiwa, mkuu wa mkoa anasema hiyo ni siasa!
kwani siasa ni kwa ajili ya viongozi tu,wakifanya raia inakuwa hatari kwa usalama wa nchi? gambo Mungu anakuona.
Amesema hizo pesa zikakarabati Mt.Meru Hospital.Sasa sijui ajali iaingetokea hospitali ingefanyaje.Maajabu ya Utawala wa JPM Rambirambi ndizo zinajenga Barabara, shule na hospitali.
Ajali ziongezeke ili rambirambi ziongezeke kufanikisha mipango ya serikali?
Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko , Mchungaji , Waandishi wa habari 7 , wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako Mayor alialikwa na Umoja wa Shule binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .
Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na taharuki kubwa baada ya kuona viongozi hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya msingi , mpaka sasa wako Polisi wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko isiyo halali .
Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka lini mambo haya ?
======
UPDATES: 1
Waandishi waliokamatwa na jeshi la polisi Arusha kwa madai tulihudhuria kikao ambacho hakikua na kibali katika shule ya Luck vincent ambapo shirikisho la wamiliki wa shule binafsi walikuwa wanaendwa kutoa rambirambi. Sisi tulipata taarifa tukaenda kufanya kazi.
1 .Godfrey Thomas -ayo tv
2.King Alphonce Saul Kusaga
3.Filbert Emmanuel -mwananchi
4.Husein Tuta ITV
5.Joseph Ngilisho -Sunrise radio
6.Geofrey Stephen -Radio 5
7.Janeth Mushi -Mtanzania
8.Zephania Ubwani -The Citizen
9.Elihuruma Yohani -mwakilishi wa Tanzania Daima
10.Idd Uwesu - Azam Tv
UPDATES; 2
Waandishi wa habari waliokamatwa Arusha leo katika utoaji wa rambirambi shule ya Lucky Vincent wameachiwa, polisi waliwaambia waliwapa lift tu.
UPDATES: 3
Kaimu RPC wa Arusha Yusuph Ilembo amesema watu wote waliokamatwa leo shuleni Lucky Vincent ni utekelezajiwa wa agizo la RC wa Arusha Mrisho Gambo
UPDATES: 4
Meya wa Arusha, Kalist Lazaro na madiwani wawili wamenyimwa dhamana.
Hapo awali waliambiwa dhamana ipo wazi na kuanza taratibu za kuwadhamini. Huenda kesho wakafikishwa mahakamani wakikabiliwa na kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali .
Wanaoshikiliwa wengine ni Inocent Kisanyage ambaye ni Katibu wa Mbunge Lema,diwani wa kata ya Olasiti mh. Alex Martin na diwani wa kata ya Muriet mh. Credo Kifukwe.
![]()
Waandishi wa habari tukiwa pamoja kutafakari tukio la leo la kukamatwa na kuambiwa tulipewa lift tuu!
WALIOKAMATWA WAKITOA RAMBIRAMBI WAELEZA WALIVYONYANYASWA
UPDATES;
Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa rambirambi katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa habari wamewekwa chini ya ulinzi na polisi shuleni.
Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye hajamtaja jina amewaambia kuwa wako chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini, wazazi waliofiwa na waandishi kama 10.
Chanzo: Mwananchi
Kuna mtu hapa jamvini alisema nchi yetu ina watu wa aina mbili
- wenye nchi
- wananchi
Wenye nchi nsiyo hao akina Gambo ndugu yangu.
Ndiyo hao wanapukuta ndevu za wenye nchi
Ukiona Kiongozi anadai mpaka Rambirambi ujue analaana kabisa.