Arusha: Mlinzi auawa kwa kuchinjwa, wauaji waondoka na kichwa

Arusha: Mlinzi auawa kwa kuchinjwa, wauaji waondoka na kichwa

Ni mwendo wa kunyofoa viungo vya binadamu walianza na figo za yule dada wakaja kirodani & macho ya yule dereva tax na sasa weamua kuondoka na kichwa cha mlinzi wa 57+years

Vijana punguzeni kula sana ujana maana mtakuja hadhirika sana uzee ukiwafika hivi baridi yote ya Arusha kwa mzee wa miaka zaidi ya 57 anawezawezaje kuwa mlinzi
 
Inasikitisha sana na pole yao sana wafiwa...
 
itafika wkt sasa hakuna kisa cha kuelezea kama hii hali haitafanyiwa kazi mauaji yatakithiri kila pembe.
 
Kwahiyo tuseme wauza supu wamesha fanya yao? ...dah hii dunia haina huruma
 
31696B7A-1425-4477-8AD1-17213C5B206C.jpeg
 
Inasemekana kichwa cha mlinzi kimepatikana
Mlinzi mwenzake anashikiliwa

Ova
 
Nasema hivi mpaka watubu waliomuua magufuli ndo haya mauzauza yataisha.
 
Katika Hadithi moja Mtume (s.a.w.w) alizielezea zama za mwisho hivi: Mtume alisema:

Itapofika zama za mwisho (dalili za Qiyama) Harji itazidi kuongezeka, Watu wakauliza harji ndio nini? Akajibu, ni mauaji, ni mauaji. Maana ya harji iliyotajwa katika hadithi ya hapo juu ya Mtume (s.a.w.w) ni "machafuko makubwa" na "vurugu" ambavyo havitaishia mahala pamoja bali vitaenea duniani kote.

Pia kuhusiana na swala hili maneno mengine ya Mtume yanasema:

Ile saa itafika wakati vurugu, umwagaji damu na machafuko yatakapokuwa mambo ya kawaida. Ulimwengu hautakoma mpaka zije enzi ambapo kutakuwa na mauaji makubwa na umwagaji mkubwa wa damu.

Tukizitafakari Hadithi hizo, tunafikishwa katika hitimisho muhimu. Mtume (s.a.w.w) alielezea mitafaruku, fujo, mauaji na vita vitavyoikumba dunia nzima na kuenea kwa hali ya khofu na akabainisha kuwa matukio haya ni ishara ya Kiama.

Tukiangalia katika karne 14 zilizopita, twaona kuwa vita vilikuwa vya Kinchi kabla ya karne 20. Hata hivyo vita ambavyo vimemuathiri kila mtu duniani, vilivyoathiri mifumo ya siasa, na mifumo ya uchumi na jamii, vimerindima zaidi katika nyakati za karibuni hususan katika vita kuu mbili za dunia.

Katika vita kuu ya kwanza ya dunia zaidi ya watu Milioni 20 walikufa, na katika vita kuu ya pili ya dunia, zaidi ya watu Milioni 50 waliuawa. Vita kuu ya pili ya dunia ndiyo inayotambuliwa kuwa ni vita iliyomwaga damu nyingi mno, iliyokuwa kubwa mno na iliyoleta maangamizi makubwa katika historia.



Migogoro ambayo imetokea baada ya vita kuu ya pili ya dunia, vita baridi, vita vya Korea, vita ya Vietnam, mgogoro wa Warabu na Waisrael vita vya Ghuba na Iraq ni miongoni mwa matukio mabaya sana ya wakati wetu. Hali kadhalika vita vya kieneo, migogoro na vita vya wenyewe kwa wenyewe vimesababisha maangamizi makubwa katika sehemu nyingi za dunia. Katika nchi kama Bosnia, Palestina, Chechnya, Iraq, Afghanistan, Kashmiri na sehemu nyingine nyingi, matatizo haya bado yanaendelea kumkumba mwanadamu.

Mfano mwingine wa machafuko yanayomuathiri mwanadamu mithili ya vita ni Ugaidi unaoratibiwa kimataifa kama wanavyokubali viongozi wengi kuwa vitendo hivi vya Ugaidi vimeongezeka mno katika nusu ya pili ya karne ya 20. Kwa kweli yawezekana kusema kuwa Ugaidi ni jambo makhususi la karne ya 20.

Jamii zilizobobea katika ubaguzi, Ukomunist na Itikadi nyingine kama hizo au zenye malengo ya Utaifa zimeshiriki katika vitendo vya kinyama kwa msaada wa teknolojia ya leo. Katika historia ya karibuni tu, vitendo vya Ugaidi mara kwa mara vimeleta maangamizi. Damu nyingi imemwagika na watu wasio na hatia ama wamejeruhiwa au wameuawa lakini bado wanadamu hawajapata fundisho kutokana na matukio haya ya balaa. Katika nchi nyingi za dunia Ugaidi unaendelea kuwa msingi wa tawala na sera.

Kuna aya nyingi katika Qur'an zinazohusiana na jambo hili. Katika Surati Arum inaelezwa kuwa machafuko yameikumba dunia kwasababu ya yale ambayo watu wameyafanya kwa mikono yao:

Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwasababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu ili awaonjeshe adhabu ya baadhi ya mambo waliyoyafanya, huenda wakarudi (wakatubia kwa Mwenyezi Mungu).
Ni bahati mbaya sana mtume hakubahatika kutoa solution

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mlinzi wa shule ya Winning spirit iliyopo Terat jijini Arusha ISSA DINAIH ISSA miaka57 mkazi wa Terati ameuawa Kikatili kwa kukatwa shingo na kutengenishwa na kiwiliwili na watu wasiojulikana na Kisha kuondoka na kichwa Cha marehemu usiku wa kuamkia leo.

Polisi Arusha imeshindwa kuzungumzia tukio hilo ikiwa ni mwendelezo wa matukio ya mauaji yanayoendelea bila kutolewa ufafanuzi Jambo linaloleta taharuki kwa wakazi Arusha.
Yaani polisi hawajatoa tamko lolote, hata kudhibitisha tu?!
 
mwendelezo wa matukio ya mauaji yanayoendelea bila kutolewa ufafanuzi Jambo linaloleta taharuki kwa wakazi Arusha.
Nani kakwambia tunataka ufafanuzi?

Tunataka jinai zilizotokea ziwe solved na ambazo hazijatokea zidhibitiwe, hatutaki ufafanuzi wa polisi wa Tanzania.
 
Kuna mtoto wa kike wa miaka 13 auwawa na wameondoka na nyeti zake hii habari imenipa ganzi na kunifadhaisha mno.
😥😥😥😥


TABORA: Mwanafunzi wa Darasa la Nne, Maria Kazungu (13) ameuawa na kunyofolewa sehemu za siri huku masikio yakitobolewa na kitu chenye ncha kali

Ongezeko la matukio ya mauaji Nchini yameilazimu Serikali kuunda Kamati ya uchunguzi

Soma - Tabora: Mwanafunzi auawa na kunyofolewa sehemu za siri

#JFLeo
 
Watu wa madini hao mawe yao yana masharti ya kuua tuu...hela gani sasa hizo si bora uwe kawaida tuu kuliko kuua ili mawe yatoke si upuuzi huo..kazi ya DNA ndio hapo kuwapata wauaji sio kutoa taarifa za watoto wa baba tofauti tu hapo Muhimbiri...
 
Hali imeanza kua mbaya...hatua shtahiki zinatakiwa kuchukuliwa
 
Back
Top Bottom