Arusha: Mlinzi auawa kwa kuchinjwa, wauaji waondoka na kichwa

Ni mwendo wa kunyofoa viungo vya binadamu walianza na figo za yule dada wakaja kirodani & macho ya yule dereva tax na sasa weamua kuondoka na kichwa cha mlinzi wa 57+years

Vijana punguzeni kula sana ujana maana mtakuja hadhirika sana uzee ukiwafika hivi baridi yote ya Arusha kwa mzee wa miaka zaidi ya 57 anawezawezaje kuwa mlinzi
 
Inasikitisha sana na pole yao sana wafiwa...
 
itafika wkt sasa hakuna kisa cha kuelezea kama hii hali haitafanyiwa kazi mauaji yatakithiri kila pembe.
 
Kwahiyo tuseme wauza supu wamesha fanya yao? ...dah hii dunia haina huruma
 
Inasemekana kichwa cha mlinzi kimepatikana
Mlinzi mwenzake anashikiliwa

Ova
 
Nasema hivi mpaka watubu waliomuua magufuli ndo haya mauzauza yataisha.
 
Ni bahati mbaya sana mtume hakubahatika kutoa solution

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Yaani polisi hawajatoa tamko lolote, hata kudhibitisha tu?!
 
mwendelezo wa matukio ya mauaji yanayoendelea bila kutolewa ufafanuzi Jambo linaloleta taharuki kwa wakazi Arusha.
Nani kakwambia tunataka ufafanuzi?

Tunataka jinai zilizotokea ziwe solved na ambazo hazijatokea zidhibitiwe, hatutaki ufafanuzi wa polisi wa Tanzania.
 
Kuna mtoto wa kike wa miaka 13 auwawa na wameondoka na nyeti zake hii habari imenipa ganzi na kunifadhaisha mno.
😥😥😥😥


TABORA: Mwanafunzi wa Darasa la Nne, Maria Kazungu (13) ameuawa na kunyofolewa sehemu za siri huku masikio yakitobolewa na kitu chenye ncha kali

Ongezeko la matukio ya mauaji Nchini yameilazimu Serikali kuunda Kamati ya uchunguzi

Soma - Tabora: Mwanafunzi auawa na kunyofolewa sehemu za siri

#JFLeo
 
Watu wa madini hao mawe yao yana masharti ya kuua tuu...hela gani sasa hizo si bora uwe kawaida tuu kuliko kuua ili mawe yatoke si upuuzi huo..kazi ya DNA ndio hapo kuwapata wauaji sio kutoa taarifa za watoto wa baba tofauti tu hapo Muhimbiri...
 
Hali imeanza kua mbaya...hatua shtahiki zinatakiwa kuchukuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…