Arusha: Mtoto wa miezi 9 alawitiwa na Baba yake mzazi hadi kufariki dunia

Arusha: Mtoto wa miezi 9 alawitiwa na Baba yake mzazi hadi kufariki dunia

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Mtoto mwenye umri wa miezi 9 amelawitiwa na baba yake mzazi hadi kufariki dunia.

Tukio hilo limetokea katika kata ya Olasiti mtaa wa Olasiti kati wilaya ya Arusha mjini.

Mwenyekiti wa mtaa wa Olasiti kati Bwana Bruno amethibisha kutokea kwa tukio hilo mtaani kwake na kusema kuwa marehemu ni ni mtoto wa kwanza kwenye familia hiyo, na kuwa baba wa marehemu ambae ndie mtuhumiwa alikuwa dereva wa daladala jijini hapa.

Wananchi wa mtaa huo wa Olasiti kati wamesikitishwa na tukio hilo katika mtaa huo na kudai ndio tukio la kwanza na la aina yake katika mtaa wao.

Jeshi la polisi tayari linamshikilia Baba na mama wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

Wamama tuwe makini sana na wale tunaowaamini majumbani kwetu.
 
Hii laana Mungu wangu inatoka wapi jamani?Unamlawiti mwanao wa kumzaa ni tamaa zilizokithiri au ni masharti au nini?Hakika amelaanika,damu ya mwanae na iwe juu yake mwenyewe.Serikali please hii kesi isichukue muda akafie gerezani hayawani na kafiri asiye na utu wala staha mjalaana!
 
Mimi ningekuwa ni Raisi watuhumiwa kama hawa ni kuwanyonga mara moja.

Kesi ikiisha mahakamani na ikathibitika umefanya kosa kama hili, natia saini yangu on the spot ukanyongwe.

Watu wa namna hii hawastahili kuishi hata kwa sekunde moja.
 
Mtoto mwenye umri wa miezi 9 amelawitiwa na babake mzazi hadi kufariki dunia.

Tukio hilo limetokea katika kata ya Olasiti mtaa wa Olasiti kati wilaya ya Arusha mjini.

Mwenyekiti wa mtaa wa Olasiti kati Bwana Bruno amethibisha kutokea kwa tukio hilo mtaani kwake na kusema kuwa marehemu ni ni mtoto wa kwanza kwenye familia hiyo, na kuwa baba wa marehemu ambae ndie mtuhumiwa alikuwa dereva wa daladala jijini hapa.

Wananchi wa mtaa huo wa Olasiti kati wamesikitishwa na tukio hilo katika mtaa huo na kudai ndio tukio la kwanza na la aina yake katika mtaa wao.

Jeshi la polisi tayari linamshikilia Baba na mama wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

Wamama tuwe makini sana na wale tunaowaamini majumbani kwetu.

Hivi Hizi Kesi huwa zinakuwa zina Ukweli au ni masuala ya Wanawake gold-diggers kuwapakazia Wanaume tuhuma ili Wanawake matapeli wa ndoa wapate nafasi za kupora Mali za Wanaume??????
 
Haafu anakuja mtu anasema Mungu yupo, Mambo yote yanapangwa na kuruhusiwa na Mungu.
Mimi nitakuwa wa Mwisho kuamini uwepo wa Mungu mwenye nguvu zote na upendo wote.
 
Nikisema wanaume hawana akili mnachongoa midomo mirefu km chupa..!!

Mwanaume km huyo ndo umuachie mtoto? Mwanamke ndoa ikikushinda beba na watoto wako, huyo kamlawiti mtoto wake na mkewe yupo, vipi ukimuachia haupo??
 
Back
Top Bottom