Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Akinamama hapo wamekosa nini wakati muuaji ni mzazi wa marehemu?Mtoto mwenye umri wa miezi 9 amelawitiwa na babake mzazi hadi kufariki dunia.
Tukio hilo limetokea katika kata ya Olasiti mtaa wa Olasiti kati wilaya ya Arusha mjini.
Mwenyekiti wa mtaa wa Olasiti kati Bwana Bruno amethibisha kutokea kwa tukio hilo mtaani kwake na kusema kuwa marehemu ni ni mtoto wa kwanza kwenye familia hiyo, na kuwa baba wa marehemu ambae ndie mtuhumiwa alikuwa dereva wa daladala jijini hapa.
Wananchi wa mtaa huo wa Olasiti kati wamesikitishwa na tukio hilo katika mtaa huo na kudai ndio tukio la kwanza na la aina yake katika mtaa wao.
Jeshi la polisi tayari linamshikilia Baba na mama wa marehemu kwa mahojiano zaidi.
Wamama tuwe makini sana na wale tunaowaamini majumbani kwetu.
Dhamira ovu ya mzazi ambaye ndiye guardian wa mtoto ni nigumu sana kujua anachokiwaza kichwani mwake ama kumtilia mashaka.