Arusha: Mtu mmoja anaswa kwa tuhuma za ujambazi, wawili wauawa na Jeshi la Polisi

Arusha: Mtu mmoja anaswa kwa tuhuma za ujambazi, wawili wauawa na Jeshi la Polisi

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limewaua watuhumiwa wawili wa ujambazi eneo la kata ya Moshono jijini Arusha. Aidha, Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Arusha, Salum Hamdun amesema askari waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aliyetambulika kwa jina la Bashiru Ally(45).

Juzi polisi mkoani Arusha iliuwa watuhumiwa wawili wa ujambazii Bashiru Ally maarufu shehe na Mohamed. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Salum Hamduni alisema Septemba 26 majambazi yalitaka kumpora mfanyabiashara fedha zake na mmoja wao akauliwa na wenzake kukimbia mmoja wao akiwa ni huyo Ally aliyekimbilia Dar es salaam ambako alikamatwa.

Alipofikishwa Arusha alikubali kutoa ushirikiano na polisi kwenda kuwaonesha walipo wenzake naye akakubali ndipo polisi walipoweka mtego kwa kumfanya awasiliane na wenzake ambao walidhani ni matayarisho ya kufanya ujambazi mwengine.

Walipokaribia eneo walipo wenzake Polisi wakampa uhuru Ally aende kwa wenzake lakini alipokaribia akapiga kelele kuashiria uwepo wa polisi ndipo walipopiga risasi juu kumuonya asikimbie lakini alikimbia na wenzake walioanza kujibizana na polisi na ndipo walipopigwa risasi na kujeruhiwa na kufa wakipelekwa hospitalini.

Kukamilisha maelezo ya kamanda huyo gazeti la Mtanzania limemnukuu "Alisema wakati watuhumiwa hao wanapelekwa hospitali, Mohamed alihojiwa kabla ya mauti kumkuta na kutaja majina ya wenzake waliotoroka na kueleza kuwa walikuwa na silaha mbili, moja aina ya shotgun na nyingine aina ya pistol ambayo alidai alikuwa anaitumia na aliiangusha eneo la tukio."

Vitu vinavyotia shaka ni kukimbia kwa Bashiru na hatimae kupigwa risasi na Mohamed naye kufariki akipelekwa hospitali lakini muda mfupi kabla kifo alitaja wenzake na idadi na aina za silaha wanazotumia.


Hamduni.jpg

​
Police in Arusha has on Monday gunned down two suspected robbers after an exchange of gun fire, the Regional Police Commander Salum Hamdun has confirmed.

According to the RPC, police laid a trap after they had arrested one Bashiru Ally (45) who confessed to have been involved in an incident where one person was killed.

He said that after interrogation the suspect named his other accomplices and while on the way to show their hide out, he tried to escape from police custody and he was shot by officers.

“When he reached the area he started making noise in a manner that was alerting residents of police presence, police tried to warn him not to run. He instead opted to run as his colleagues shooting at the police. It was then that he was shot together with one other suspect who was only identified as Mohammed,” said the police commander.

The two reportedly died on the way to hospital.

Though the other suspects remain at large police managed to recover one gun with nine rounds of ammunitions
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limewaua watuhumiwa wawili wa ujambazi eneo la kata ya Moshono jijini Arusha. Aidha, Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Arusha, Salum Hamdun amesema askari waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aliyetambulika kwa jina la Bashiru Ally(45)

Ni huyu bashiru wa ccm? Juzi kati hapa alionekana na mabeberu
 
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limewaua watuhumiwa wawili wa ujambazi eneo la kata ya Moshono jijini Arusha. Aidha, Kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Arusha, Salum Hamdun amesema askari waliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aliyetambulika kwa jina la Bashiru Ally(45)

Hakuna mwenye picha yake picha la jambazi
 
Hivi ruhusa ya polisi kuua iko kisheria?
Mkuu sheria inaruhusu kujikinga mwenyewe hadi kuua, kumkinga mwingine, mali n.k. Hivyo kama kuna shambulio lolote dhidi yako au mwingine, basi inaruhusiwa.

Kwahiyo inategemea.

Hiyo ni sheria ya Kanuni na adhabu kwa Tz.
 
Mkuu sheria inaruhusu kujikinga mwenyewe hadi kuua, kumkinga mwingine, mali n.k. Hivyo kama kuna shambulio lolote dhidi yako au mwingine, basi inaruhusiwa.

Kwahiyo inategemea.

Hiyo ni sheria ya Kanuni na adhabu kwa Tz.

Nakuelewa mkuu, miaka hii ya karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la polisi kuwaua majambazi huku bila vithibitisho vya kurushiana risasi ama purujushani.

Sasa inaleta wasiwasi wa kama mauaji hayo ni genuine.
 
Back
Top Bottom