Arusha: Mwanafunzi wa Chuo cha Tumaini, Makumira abakwa hadi mauti

Arusha: Mwanafunzi wa Chuo cha Tumaini, Makumira abakwa hadi mauti

Nilikuwa na muona marehemu kwenye misa ya saa nne pale makumira akiambatana na hiyo familia ya kizungu.......RIP
 
chuo cha makumira ni chuo cha kkkt kinafundisha madansa? nilidhani ni kupiga vyombo tu.ila pole sana mdada sijui ni shida gani ilitokea
Hapana, kinafundisha upigaji vyombo wa cultures mbalimbali na somo hasa la music tena classic ones.
 
Utaniuliza vipi swali lisilohusiana na post zangu, halafu unategemea nisitilie shaka uelewa wako?
Hivi kwani wewe ni Mmeru? ati kwasababu unamzungumzia msichana wa Arusha Makumira, nikulazimishe kujibu swali hilo unaonaje hapo.

Kama na hapo hujanielewa basi utakuwa na kiwango kidogo sana cha uelewa, sorry najitahidi nisikukwaze lakini naona huenda nikakukwaza ndugu.
Acha kuruka ruka wewe... hazihusiani na posts zako kivipi? Post yangu ilikuwa hii hapa:
Sio tu Marehemu hasemwi lakini alichosema hakipo manake amem-judge kwa kuangalia picha aliyopiga beach... sasa sijui ni wasichana wangapi wanavaa madela wakiwa beach.
Msingi wa post yangu ni justification ya watu kwamba ni ya "kujitakia" kwavile anatembea mwenyewe uchi! Wewe ukani-quote na post yako hii hapa:
inamaana wewe ukipiga picha mmadam uko bafuni, na bafuni watu huvua basi ukiiweka mtandaoni ni sawa?
kwamujibu wa maelezo yako ni kwamba hiyo picha kapiga sehemu husika na vazi ila hukuona tatizo ikiwemo kwenye mtandao.
Ulikuwa unajaribu ku-justify simply because alipiga picha ya mapaja wazi akiwa beach na akai-post FB!Na kabla ya hapo ulishatoa hoja ya ku-justify tukio kwamba limetokana na msichana kuanika maungo wazi! Post yako hii hapa:
Hakuna anayetetea ubakaji hapa, tunazungumzia vichocheo vya tukio, bint mrembo halafu mchanga kama anavyoonekana unafikiri rijali gani anaweza pishana naye asigeuke kuona alichojaaliwa nacho, baada ya hapo nini kitafuata?
But still, hufahamu lolote kuhusu dressing ya huyo binti zaidi ya hiyo picha ya beach ambayo alii-post FB! Ndipo nikahoji:
We jamaa mtu wa ajabu sana! Kwahiyo una-assume sio?! Kwamba, kwavile ameweka FB picha aliyopiga beach akiwa mapaja wazi basi hashindwi kutembea akiwa mapaja wazi!! Nimekuuliza, wewe unaweza kubaka kwa ajili ya pic za FB?
Badala ya kujibu hoja, ukaishia kusema uelewa wangu mdogo!!!

Sasa fuatilia huo mlolongo kisha utapata jibu ni nani kati yetu ana uelewa mdogo! Narudia swali:wewe unaweza kubaka kwa ajili ya pic za FB?Kama huna jibu, piga kimya!!! Manake ikiwa umesahau ulichoandika mwenyewe muda mfupi tu uliopita; basi si tu kwamba uelewa wako unatia shaka bali hata uwezo wako wa kuhifadhi kumbukumbu nao unatia shaka!
 
Apumzike kwa amani tu kwani kila jambo linalotekea linasababu yake na hii nadhani dada zetu kuwe makini sana sana maana wengi wenu mnatabia ya kuwasaliti wanaume na kukukimbilia mnapopaona pana usalama wa penzi na kuacha maumivu kwa wanaume kuna wanaume wengine hawajui kuacha sASA linapokuja suala la kuachwa yeye lazima alipe mabaya tu ili nafsi yake ipate kusuuzika na kuwa salama wanawake wengi wanadhani kuwa kumkimbi MWANAUME ndio ngao hata ukiolewa gafla na bado siyo kinga maana malipo ni hapahapa duniani hili neno huwa linafanya kazi sana muhimu umakini unaitajika sana maana dunia ya sasa ni tofauti na ya miaka 30 iliyopita sikuhizi watu wanakula nyama za watu

#mungu nipe maisha marefu niweze kushuhudia mengi hapa duniani hususani Tanznia ili siku ya mwisho niwe na mengi ya kusema mbele zako AMEN
 
Tatizo Arusha hamumpi ushirikiano mkuu wa mkoa na kamati yake je usalama wenu utatoka wapi? Kazi siasa na kukosoa utendaji wa Rais
Haya kamwambie gambo aachane na siasa afanye kazi iliyompeleka, huwez mtenganisha Lema na siasa
 
Hapana nadhani walikuwa wanamlea.....kuwa positive kwanini uwaze kulikuwa na bwana akee
unavyoambiwa uwe unaelewa watu tuna uthibitisho ww unao kama alikuwa analelewa
1478166580182.jpg
1478166594433.png
1478166608297.png
1478166629920.png
1478166639218.png
 
similiki bastola hata wembe kwa kujiami. lakini kwa tukio hili kama ningekuwa nayo nashawishika kuwasaka watuhumiwa kwa bastola na sina uhakika kama naweza zuia hasira yangu ya kufyatua.
poleni sana wafiwa na wanawake wote ambao tukio hili limewakumbusha ukatili wa wanaume waliokwisha wafanyia nyinyi binafsi, wazazi wenu au ndugu zenu wa karibu na ikaibua uchungu kwa tukio hili katika maisha yenu.
 
Mavazi ya mtu au muonekano wa mtu haukupi wewe mamlaka hapa chini na mbiguni kutoa roho ya binadamu mwingine. Watu wanaua wenzao hapo TZ na wala hawanyongwi leo hii huyu binti amevaa nguo ya ufukweni ya heshima kabisa na mnahalalisha kifo chake kwa kumlaumu huyu dada. Nimesikitika sana na huu upumbavu kwa kweli. Hapa Marekani ukilala hata na mke wako kwa kumlazimisha akawaita polisi unashtakiwa kwa kurape. Na ni kifungo cha miaka zaidi ya 20.

Yaani moyo wangu unamajonzi kwa kweli huyu binti amekufa kifo cha kinyama kwa sababu ya mbwa mwitu nyamafu washenzi na watafia jela.
...hapo unapozungumzia we ni marekani......mi nazungumzia in a Tanzanian context...huyu binti kabakwa TZ si marekani....tuwe wazi na reality...we ukija TZ jaribu kupita na ka mini skirt kako kariakoo uone kama utaachwa....huu ndio uhalisia...hatuko marekani hapa...
 
Back
Top Bottom