Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Mwanamke mmoja ambae bado hajajulikana ameuliwa na watu wasiojulikana na kutupwa mto Themi akiwa bila nguo.
Tukio hilo ambalo limezua taharuki miongoni mwa watu limetokea kata ya Sinoni katika mtaa wa onjavutian.
Mwenyekiti wa mtaa wa onjavutian ambapo tukio hilo limetokea Lesioni Joseph amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo jumanne na kueleza kuwa alifika mtoni baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi na kwenda kuona maiti ya mwanamke huyo, na kupiga simu polisi ambapo polisi wamekuja na kuchukua mwili huo.
=============
Updates...
Mwenyekiti wa Onjavutian katika Kata ya Sinoni, Lesioni Joseph anaelezea kilichotokea:
Hakuna taarifa kama ni kweli ameuawa au amekufa kwa sababu zingine, baada ya kupata taarifa za mwili kuonekana kando ya mto niliita Askari na baada ya uchunguzi wa awali wakabaini kuwa mwili haukuguswa kwa maana ya kushambuliwa.
Marehemu anaitwa Suzan au mama Dorcas, taarifa za uchunguzi wa awali zinaonesha kuwa aliporejea nyumbani jana usiku (Mei 15, 2023) akamwambia dada wa jirani kuwa amepoteza pochi yake ambayo ilikuwa na Tsh. 25,000.
Hakurejea nyumbani tangu alipoondoka, Askari walipokuja na kufanya uchunguzi wamesema inawezekana alidondoka au aliumia akashindwa kutoka kwenye maji.
Mwili wake umekutwa ukiwa hauna nguo ya chini, alikuwa amesaliwa na nguo ya juu tu.. Umri wake ni kati ya miaka 40 hadi 45.