Arusha: Mwili wa Bodaboda aliyekuwa kapotea wakutwa umekatwa shingo na kutobolewa macho

Sio wote wanaouwawa wamefanya hivyo na tusiwahukumu
Mbona mpaka viongozi wanakula? Na kila sehemu wapo wa hivyo na washenzi hao wake za watu ndio wanaogawa
Kwanini wasiwe na adabu zao kama wana familia?

Haki itendeke vijana wanakufa na haki hamna

Wengine wanauwawa kisa pikipiki
Vifo vya boda boda wengi vinatokana na issue 2 tu,kisasi na hiyo kunyanganywa pikipiki.
 
DEREVA BODABODA ALIYEPOTEA ARUSHA, MWILI WAKUTWA UKIWA UMEKATWA SHINGO NA KUTOBOLEWA MACHO

Hamis Idd Masimba, mwenye umri wa miaka 24, dereva wa bodaboda katika kijiji cha Mlima CCM, Kata ya Murieti jijini Arusha, aliyeripotiwa kupotea, mwili wake umekutwa katika Kata ya Olasiti ukiwa na majeraha makubwa, ikiwemo kukatwa shingo na kutobolewa macho.

Wakizungumza, ndugu za marehemu wamesema baada ya Hamis kupotea, simu yake ilipatikana na mtu alivedai kuwa ameokota na kuhitaji Shilingi 10,000 ili airejeshe. Hata hivyo, muda mfupi baadaye simu hiyo ilizimwa. Katika harakati za kumtafuta, ndugu hao walikuta viatu vyake pekee, huku pikipiki aliyokuwa akiendesha ikiwa haijulikani ilipo.

Tukio hilo linakuwa miongoni mwa matukio kadhaa ya mauaji yanayowakumba madereva bodaboda katika maeneo ya Arusha. Takribani miezi kadhaa iliyopita, dereva mwingine wa bodaboda alikodishwa na abiria na kwenda kuuawa katika eneo la karibu na Idara ya Maji, Mateves.

Aidha, katika maeneo ya Meru, dereva mwingine wa bodaboda alikutwa ameuawa, akiwa ametobolewa macho na kukatwa shingo, kabla ya mwili wake kutupwa katika eneo la mashambani.

Matukio haya yanapaswa kulaaniwa, huku madereva bodaboda wakitakiwa kuwa makini zaidi wanapochukua abiria wasiowafahamu, hasa wanapoelekezwa katika maeneo yasiyo na watu.

Zamani haya matokeo tuliyazoea kuyasikia Geita na Njombe
Siku Arusha imewapiku wote hao. Machaliiii sijui wamekuwaje
 
Kafa kifo kibaya sana.. Wauaji ni watu wa hovyo mno
 
Back
Top Bottom