Arusha bangi ni kama sigara tu, sio big deal, Mikoa miingine watu wakijua unavuta bangi huwa unaonekana kama jambazi hivi 😂
Watalii wa nchi mbali mbali waliojaa Arusha wanavuta kitu cha chuga.
Watu wazito, kuanzia mtajiri wa madini, ma ceo wa makampuni, wafanyabiashara wakubwa, n.k wanavuta.
Watoto wa kishua wanavuta, hata supermarket ya Njiro complex nmekutana nao mara kibao wakiwa kwenye range za wazazi wao.
Wanafunzi wa vyuoni kama kawa, nliwahi soma pale chuo cha uhasibu (IAA), hostel kibao huwezi kukosa mvuta bange, pia vyuo vya Arusha Tech kule mianzini nako niliskia wanapuliza.
Boda boda, wauza chips, n.k kama kawa
Na list inaendelea ni ndefu mno.
Sifa kuu ya hii bangi inayofanya isifiwe sana na kupewa jina la kipekee almarufu "kitu cha arusha" ni ubora wake, wakulima wa bangi nahisi wana elimu nzuri ya kulima na kuvuna bangi ili kuteka soko lenye watumiaji wengi wanaohitaji viwango bora kuanzia mapedeshee hadi watalii, kuna bangi hazinaga ubora kabisa, unakuta mkulima anaogopa kukamatwa anavuna haraka haraka wakati muda bado ama hajailima vizuri hizo bangi huwa ni sawa na makapi.
Binafsi nlijifunzia bangi huku Arusha, Nakumbuka siku ya kwanza napiga kitu, nliogopa sana ile mapigo ya moyo yanavyoenda spidi maradufu ili kufidia spidi ya damu inayoanza kutembea taratibu baada ya kuvuta bangi, ila baada ya hapo mapigo yakatulia, kajicho nyanya kwa mbali, nikaanza kusikilizia stim tamu za kitu cha A town.
Pia nakumbuka nikiwa Arusha nilitokea kuwaelewa sana mabinti wake, niliambiwa kwamba mabinti wanapenda ugumu wa kiume ila nikaona huwa wanafosi tu, Mabinti warembo wa kinyaturu, kimbulu na kinyiramba wapi na wapi na ugumu, nilianza kuwa na uraibu nao kwa uzuri wao ila nashukuru nilistuka kuacha uraibu huo ambao ungeweza kuniletea magonjwa, kunifanya nisahau kilichonipeleka chuo, kuishiwa pesa kwa kuhonga, n.k,
Anyway nliacha, siku hizi sipendi kutumia kitu kinacho fujunyua akili ili nijiskie vizuri kuanzia pombe, sigara, bangi, uzinzi, n.k. starehe pekee ninayoipenda ni kusoma biblia, kuchek muvi na kufanya tendo lililoruhusiwa na mke wangu.