Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Credit kwa WasafiTv👇🏼
View: https://youtu.be/dl-pDpB8K2Y?si=AssMQvmbRoW28ILy

Johnson Joseph, mkazi wa Murieti, jijini Arusha, na mfanyabiashara wa vyuma chakavu, anadaiwa kuuawa na watu wawili waliodai kuwa maafisa wa polisi katika mtaa wa Eso, kata ya Ungalimited. Tukio hilo linadaiwa kutokea wakati marehemu akiwa amefungwa pingu na kupigwa vikali kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu, baada ya mtu mwingine, ambaye hajatajwa hadharani, kukamatwa na kumtaja Bw. Johnson kama mhusika wa uhalifu.
Mashuhuda wa tukio hilo, wakiwemo mke na mtoto wa marehemu, wanasema watu hao waliodai kuwa askari polisi walimpiga Bw. Johnson kwa ukatili, wakimkanyaga kichwani licha ya juhudi za majirani na familia kujaribu kuzuia mateso hayo. Mashuhuda hao pia walieleza kuwa watu hao hawakuonyesha vitambulisho vyovyote kuthibitisha kuwa ni askari polisi lakkni hata hivyo, walipofanikiwa kuadhibiti askari hao walikimbia eneo la tukio, japo tayari Bw. Joseph alikuwa ameshafariki dunia.
Baada ya tukio hilo, mashuhuda walipiga simu kituo cha polisi kuomba msaada wa kuchukua mwili wa marehemu. Inadaiwa kuwa askari walipofika kuchukua mwili, walilazimika kurudi kituoni kuchukua funguo za pingu ili kumfungua marehemu.
Pia, mwenyekiti wa mtaa wa Eso, Bw. Selemani Abdallah, ameeleza kuwa askari hao hawakushirikiana na uongozi wa mtaa huo wakati wa tukio hilo na kuwa marehemu alifariki palepale katika eneo la tukio. Mwenyekiti pamoja na balozi wa mtaa wanadai kuizuiliwa kuingia kwenye gari la polisi lililobeba mwili wa marehemu.
Kwa upande wa jeshi la polisi, limeeleza kuwa uchunguzi bado unaendelea. Polisi wanadai kuwa Bw. Joseph alifariki wakati akipatiwa matibabu, madai yanayopingwa na mwenyekiti Bw. Selemani Abdallah, ambaye amesema daktari wa Hospitali ya Mount Meru aliwafahamisha kuwa marehemu alikuwa amefariki kabla hajafikishwa hospitalini. Polisi wamedai pia kuwa wakati wa kumkamata marehemu, walishambuliwa na kundi la watu waliomtorosha marehemu huyo kwa kutumia pikipiki.