Arusha: Raia wa Romania akamwatwa kwa kuiba fedha bank.

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha inamshikilia raia wa Romania, Constantin Catalin Podoleanu, mwenye umri wa miaka 39, kwa tuhuma za kutumia taarifa za kadi za benki zilizoibwa na kujipatia fedha kwa njia haramu.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo, amesema mtuhumiwa alikamatwa na maafisa wa taasisi hiyo katika eneo la Njiro jijini Arusha.

Amesema wakati wa upekuzi katika makazi ya mtuhumiwa, maafisa walibaini stakabadhi za malipo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 171, zaidi ya dola za Marekani 55,000, fedha taslimu zaidi ya Sh milioni mbili, noti za Euro 20 pamoja na Riyal 15.

Aidha, Ngailo amesema mtuhumiwa alikutwa na mashine sita za POS, kadi za benki za taasisi mbalimbali, vifaa na kemikali zinazodaiwa kutumika kutengeneza kadi bandia zinazotumika kuiba fedha kwenye akaunti za wateja wa benki.

Amesema pia mtuhumiwa alikutwa na kompyuta mpakato mbili, ambazo zinadaiwa kuwa sehemu ya vifaa anavyotumia katika shughuli hizo za wizi.

TAKUKURU imesema inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo, huku hatua zaidi za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.
 
Attachments

  • 1787402164082.jpg
    1787402164082.jpg
    133.1 KB · Views: 20
  • 1787402160655.jpg
    1787402160655.jpg
    120.1 KB · Views: 18
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha inamshikilia raia wa Romania, Constantin Catalin Podoleanu, mwenye umri wa miaka 39, kwa tuhuma za kutumia taarifa za kadi za benki zilizoibwa na kujipatia fedha kwa njia haramu.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo, amesema mtuhumiwa alikamatwa na maafisa wa taasisi hiyo katika eneo la Njiro jijini Arusha.

Amesema wakati wa upekuzi katika makazi ya mtuhumiwa, maafisa walibaini stakabadhi za malipo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 171, zaidi ya dola za Marekani 55,000, fedha taslimu zaidi ya Sh milioni mbili, noti za Euro 20 pamoja na Riyal 15.

Aidha, Ngailo amesema mtuhumiwa alikutwa na mashine sita za POS, kadi za benki za taasisi mbalimbali, vifaa na kemikali zinazodaiwa kutumika kutengeneza kadi bandia zinazotumika kuiba fedha kwenye akaunti za wateja wa benki.

Amesema pia mtuhumiwa alikutwa na kompyuta mpakato mbili, ambazo zinadaiwa kuwa sehemu ya vifaa anavyotumia katika shughuli hizo za wizi.

TAKUKURU imesema inaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo, huku hatua zaidi za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.
Video:
View: https://www.facebook.com/share/v/1dp3Wgi87M/
 
Pesa duniani ipo kazi ni wewe tu kile unachokifikiria kua halisi
 
benki na wenyewe ni wezi wakubwa, nampa pole mpambanaji huko jela anakokwenda asisite kugawana ujuzi na waungwana
 
Ilikuwa ni suala la muda tu
Hao waromania wanajulikana ulaya nzima kwa huu mchezo
Nilikuwa nasubiri siku nisikie kuwa bongo mmefikiwa
Ila itakuwa malaya anaotombatomba wamemchoma
 
Back
Top Bottom