Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Rais Dkt. Samia amewarudishia kanisa katoliki Mkoani Arusha eneo lao walilokuwa wanalimiki kwa muda mrefu na bada uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Arusha na kisaha kuwataka kanisa katoliki kulipia eneo lao milioni 500 kitu ambacho Rais Samia ameutaka uongozi wa Mkoa kuresha eneo hilo pamoja na fedha walizo chukua.
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ametoa ufafanuzi juu ya eneo la kanisa katoliki walilokuwa wakimiliki kwa siku nyingi na wakanyang'anywa na badae wakatakiwa kulinunua tena na wala eneo hilo halikuwa la serikali ila viongozi waliyokuwepo walikubali kupokea fedha ambazo hawakustahili.
"Jana nimezungumza na Mhe. Rais Samia kumueleza jambo hili na akanambia kwamba, Niwaelekeze Mkoa pamoja na Jiji kuwa eneo hilo lilejeshwe haraka kanisa mara moja na fedha hizo Milioni 500 zilejeshwe kanisani mara moja". Amesema Mchengerwa.
"Nawaelekeza nyinyi Mkoa chini yako Rc Paul Makonda mzirejeshe fedha hizo kwa namna mlivyo zichukua mwanzo na njia hiyo hiyo zirudi kanisani hayo ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia". Amesema Mchengerwa.