Arusha: Rais Samia atoa TZS 520BL sawa na 80% ya bajeti nzima ya maji ya Taifa ya mwaka

Hayo ni mahaba au jukumu lake ?
"Ni kama kusema mahaba ya mwalimu wa shule ya msingi, kasahihisha madaftari 200 ya wanafunzi wa darasa la 4B"
 
Huu ni chochezi wa kiwango cha lami yaan serikali itowe pesa alafu wewe unatuletea ngonjela kuwa mama katowa pesa! Hivi ni kweli umeongea kwa kufikiri
 
Sawa.....kazi iendelee
 
Mahaba kwa watu wa kaskazini,ww pumbav sana
 

Hakika uongozi wa Rais Samia ni neema tupu kila kona ya nchi |Arusha wapewa TZS 5.2B kwa mwaka kama 10% ya mapato ya Jiji kwaajili Vijana, wanawake na walemavu,Machali wa " R " Changamkeni acheni Ukamanda fake,​

" Hakuna kama Samia "​


Chini ya Sheria ya fedha ya Serikali za mitaa sura namba 290 kifungu cha 37 ya mwaka 2019 kila halmashauri inatakiwa kutenga 10% ya mapato yake kwa mwaka kwaajili ya maendeleo ya watu wa halmashauri husika kwa mchanganuo ufuatao, 4% kwaajili ya wanawake, 4% kwaajili ya Vijana na 2% kwaajili ya walemavu bila kujali dini, rangi,kabila au itikadi za siasa,

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk John Marco Pima ameukuna mtima wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kutoa tshs 1.37BL kwaajili ya kutekeleza sheria hiyo ya fedha kwa robo ya kwanza ( 1Q ) ya mwaka,Nakwamantiki hiyo kwa mwaka mzima Dk Pima kwa niaba ya Rais Samia atatoa jumla ya Tshs 5.2BL yaani Vijana watapata Tshs 2.08BL,Wanawake Tshs 2.08BL na Walemavu Tshs 1.04BL hii ni zaidi ya Commercial Bank,Arusha changamkieni fursa hii achaneni na mambo ya Ukamanda tumieni hizi fedha ili mjenge familia zenu najua ninyi kamwe hamuwezi kukimbilia Kanada mmecheleweshwa sana Arusha,

Angalia hii,Kama kila kikundi cha watu watano kitapewa Tshs 10M tu Rais Samia kupitia Arusha Jiji atasaidia Jumla ya vikundi 520 kwa mwaka na tutakuwa na Loan Portifolio ya watu|wateja zaidi ya 2,600 ambao kila mmoja atapewa mtaji wa kuanzia wa mil 2,Na hii ndio utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020|25 iliyoahidi ajira 8M kila mwenye macho na aone sasa Juhudi kubwa na nzuri za Rais Samia Suluhu Hassan Mkt wa ccm-tanzania.

Tanzania tuna Jumla ya halmashauri 184 kama kila Halmashauri itakuwa na Loan Portfolio ya wateja 1,000 tu nchi nzima kwa mwaka mmoja tutakuwa na Loan Portfolio ya watu 184,000 hapa Umasikini tutausikia tu redioni, Wakurugenzi wengine mnayohaja ya kuiga mfano huu mzuri wa Dk John Marco Pima mkurugenzi wa Jiji la Arusha na natamani matumizi ya 10% yawe ndio kigezo cha Ubora wa Mkurugenzi kwani wanachi lazima waone umuhimu wa kuendelea kuichagua CCM-Tanzania.

MACHALI WA " R " CHANGAMKENI
 
Tumuelewe nani? Chadema vipi?

Hizi propaganda kawapelekee wajinga huko vijijini wasiojua lolote. Huo mradi ulikuwa ni wa mkopo kipindi cha mwisho wa utawala wa JK, wakati huo mipango yote ilishakamilika na pesa zakaingia wakati dhalimu akiwa madarakani. Mama wa kambo yeye kaokoto dodo chini ya mnazi.
 
Mwenyezi Mungu azidi kumlinda ,kumpa afya njema na kumsimamia kipenzi chetu CHIFU MKUU HANGAYA aaaamin aaaamin🙏

Siempre JMT
 
2.08Bil kwa VIJANA💪

Machalii wa chuga chuganiii KAZI KWENUUU......
 
😍
 
Ebu subiri hayo maji kwanza maana kusema na kutenda ni vitu tofauti kbsa katika nchi hii
 
Bilioni 520 kwa ajili ya maji....

Leo anatuletea UZINDUZI WA KIWANDA CHA NYAMA jirani na Namanga 💪

Siempre JMT
 
asante sana Crde
 
Huko anapozitoa ni wapi na sisi atuambie tuzifuate ?
 
Huyu ndio Rais tulimngojea miaka mingi

Hongera sana Rais Samia
 
Hongera Dk John Marco Pima
Hongera Rais Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…