Arusha: Rais Samia atoa TZS 520BL sawa na 80% ya bajeti nzima ya maji ya Taifa ya mwaka

Hakuna kama Samia nasisitiza,

Haya mambo sio madogo
 
Safi sana Arusha jiji
 

Kama si mahaba niue basi ni kampeni zetu 2025 😁😁
 
Unakosea unapomtaja mbunge kushindwa kusolve tatizo la maji.
Unajua mbunge hakusanyi kodi au ushuru kokote, kazi yake ni kupeleka matatizo ya wananchi wake serikalini ili yatatuliwe. Na hilo tayari wamelifanya na ndio maana serikali imetoa hela. Hadi tutakapoacha kuamini kuwa mbunge anatatua kero zinazohitaji budget ya serikali ndipo tutakapoondokana na utamaduni wa kupigwa ahadi za uongo na hawa wabunge wakati wa kampeni.
 
Hizo pesa ni nyingi sana hujafafanua ni za mradi mmja au? Na zimetoka wapi? Maana 80% ya bajeti sio mchezo..

Anyway congrats kwake,ni vyema tuwe tunafanya vitu kama hivi tukitoka tumetoka.Samia hoyeee.
Ni fedha za mradi mzima hizo alizindua Magufuli mradi bado haujakamilika ni za mkopo toka Benki ya maendeleo ya Africa, Mama alipita kukagua mradi umefikia asilimia ngapi...
 
mziki wa ukweli wa maji upo Kiteto na handeni...huko kwingine watapiga hela tu
 
Onyesha zilipotolewa ile awamu ya masifa, yaani watoa pesa yote hiyo waache kwenda kuuza sura na kujigamba kwenye vyombo vya habari,labda sio awamu ya 5 nayoijua..mtu hadi kuzindua choo ilikuwa sherehe ya kitaifa sembuse mradi wa mabilioni?
Kama kitu hujui ni bora ukae kimya tu
 
Ilikuwa ni mwaka 2018 Magufuli alizindua huu mradi, akaenda kwenye kisima kata ya Kimnyak wilayani Arumeru na hii picha yake, mradi kwa sasa umefikia asilimia 75View attachment 1978279
Unaelewa maana ya kuzindua? Au aliweka Jiwe la msingi?

Magu alikuwaga hana Kazi alizindua hata barabara zilozokamilika toka 2014..

Sasa miaka yote kwa nini mradi haujakamilika?
 
Rudi shule ukajifunze propaganda, huo mradi ni wa enzi za JK, tena dhalimu alitaka kupora hizo hela apeleke huo mradi kanda ya ziwa, watoa mkopo wakamgomea. Katafuteni wajinga wasiojua lolote ndio uwalishe hii propaganda mfu.

Tena huu mradi una mkono wa WB sijui Samia jaingiaje hapa.

Nadhani shule propaganda wanahitaji kubadili sylabus kwasababu hata namna ya kudanganya watu imekuwa ya kijinga sana.
 
Unaelewa maana ya kuzindua? Au aliweka Jiwe la msingi?

Magu alikuwaga hana Kazi alizindua hata barabara zilozokamilika toka 2014..

Sasa miaka yote kwa nini mradi haujakamilika?
Huu mradi ulianza 2018 na yeye ndio alizindua kwa kuweka jiwe la msingi... na fedha ni za mkopo kutoka Afdb...
 
Kuna zingine hizi hapa


Ni Billion 514 ambazo waliwahi kupewa Arusha wakati wa hayati JPM, mwaka 2017 kwa ajli ya mradi wa maji vievile. Aidha zitakuwa hazikumaliza tatizo, au ziliibiwa
 
Huu mradi ulianza 2018 na yeye ndio alizindua kwa kuweka jiwe la msingi... na fedha ni za mkopo kutoka Afdb...

Point hapo ni kweli labda mradi ulikuwepo na pesa zilitoka lkn labda hazijafika kwenye eneo la tukio kwa asilimia zote kutokana hasa na siasa za kipindi cha awamu ya tano mtizamo wao hasi kuhusu kanda ya Kaskazini lkn alipoingia mama haoni sababu ya kuweka figisu za kuumalizia mradi ndo maana pesa imetoka yote na mradi ukamilike

Point sio ulianza lini ila why ulikuwa unasua sua labda isije ikawa ile dhana ya awamu fulani kuhusu kanda fulani
 
Unchoandika si sahihi ni hisia, kama unajua miradi huwezi andika kitu cha namna hii, mbona Barabara ya Tengeru - Sakina ilikamilika

kama unakumbuka kampeni alipokuja Arusha Magufuli alitamani ukamilike Desemba mwaka jana...

tena huu mradi unaendelea huku watu wakipata maji, mfano visima vya Kimnyak vyote vinatoa maji tanki kubwa kwa sasa linatumika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…