Pre GE2025 Arusha: RC Makonda aiagiza TAKUKURU kumhoji Mrisho Gambo upotevu wa Tsh. Milioni 400 zilizochangwa na wadau kwa ajili ya kusaidia bodaboda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM ndio magwiji wa siasa hizi za majitaka.
Na yule mzee wa 80 naye ni mpenzi kweli wa hii mambo.
Nani ndani ya CCM anaweza kusimama na kutoa hoja ya maana!!?
Chama ambacho kinalea matatizo ya wananchi kweli kinaweza kueleza hoja za kutatua hayo matatizo!!???
Siasa za maji taka
 
Gambo ndio alisema wameshirikiana na TAKuKURU kuzuia Ufisadi wa Watendaji wanaosimamiwa na Bashite Sasa hapo anahojiwa Ili kitokee nini? 🤣🤣

Mbona Bashite anatapatapa?

Mwisho uliwahi ona wapi TAKuKURU akakamata mwanasiasa tofauti na Watendaji wa Serikali?
 
Tangu 2016 miaka 9 nyuma. Siasa ama kweli zina vituko.
 
Ikumbukwe ushahidi wa upande wa RAS utakuwa mgumu sababu alifariki kwa ajali ya gari (Richard Kwitega) - sasa hapa Gambo ataogelea mwenyewe

Akibainika kutumia fedha hizo nje ya malengo jasho litamtoka
 
Shamba la Bwana Heri na Mbuzi ni wa Bwana Heri😀😀 .Mimi Ngoja niendelee tu hapa kutafuta kura za ndio za Rais Samia huku mitaani.
Hapana mimi na imani kuwa wewe lucas ni timu Lissu na utakuwa front kupigania matokeo ya Lissu 2025 election .
 
Hahaha Makonda huwa hakai kimya mpaka apigwe Ban kutoka Ikulu.

Alipambana na Marehemu Dr.Ndugulile Kigamboni, akidai maagizo kutoka ikulu kwamba yeye Makonda ndiye alitakiwa agombee Kigamboni.

Na alimuaminisha kila mtu wakakaa pembeni. Ndicho anakifanya sasa kwa Gambo Arusha.

Magufuli alipopata taarifa alimkaanga hadharani, akasema mimi sijatuma mtu kugombea Kigamboni, wewe kama unataka kugombea kigamboni, ngoja nikupumzishe ukuu wa mkoa sasa ukapambane huko kutafuta jimbo.

Baada ya kauli ya Magufuli hapo hapo zile nguvu zikayeyuka, Makonda akawa kama toilet paper iliyolowa maji.

Hata yule Sheik wa Mkoa Alhaji ASAD akatoka na kumkataa Makonda, na yote yapo mitandaoni, alikuwa akidai waislamu wanamtaka yeye Kigamboni.

Huyo Makonda akiachwa anaweza hata kudhuru kwa madai kwamba katumwa kutoka ikulu.

Inabidi Ikulu impige Ban mapema, kama anataka ubunge wamtoe ukuu wa Mkoa, ili asitumie madaraka vibaya.
 
Gambo alichosema kazuia ni hela za kununulia eneo la kujenga shule. Hizi 400m ni za zamani akiwa RC.
 
Ikumbukwe ushahidi wa upande wa RAS utakuwa mgumu sababu alifariki kwa ajali ya gari (Richard Kwitega) - sasa hapa Gambo ataogelea mwenyewe

Akibainika kutumia fedha hizo nje ya malengo jasho litamtoka
Hizo hela kashawahi kuulizwa sana anatoa majibu ya kisiasa. Halafu kwanini hela za bodaboda azimege na kuwapa mama ntilie?
 
Reactions: Tui
Uko sahihi ila anayempiga spana ndo mfitini aliyekubuhu. Acha wapelekeane moto kwanza.
 
🤣😂🤣😂🤣🙌
Your browser is not able to display this video.
 
Reactions: Okk
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…