Pre GE2025 Arusha: RC Makonda aiagiza TAKUKURU kumhoji Mrisho Gambo upotevu wa Tsh. Milioni 400 zilizochangwa na wadau kwa ajili ya kusaidia bodaboda

Pre GE2025 Arusha: RC Makonda aiagiza TAKUKURU kumhoji Mrisho Gambo upotevu wa Tsh. Milioni 400 zilizochangwa na wadau kwa ajili ya kusaidia bodaboda

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Magufuli alimtoa wakati tayari kashajaza fomu za kuutaka ubunge. Uwe na kumbukumbu.
Haijalishi,Wamtoe sasa hivi ili kuweka mnyukano sawa, siyo atumie madaraka kumkandamiza mwenzake. Kama anataka ubunge aende jimboni kwake?

Kwani makonda ni mkazi wa Arusha?

kule alipelekwa kikazi.
 
Haijalishi,Wamtoe sasa hivi ili kuweka mnyukano sawa, siyo atumie madaraka kumkandamiza mwenzake. Kama anataka ubunge aende jimboni kwake?

Kwani makonda ni mkazi wa Arusha?

kule alipelekwa kikazi.
Wewe unaipangia mamlaka ya uteuzi kama nani? Kuna mtu anamiliki jimbo hadi useme aende jimboni kwake? Swali lako la kama Makonda ni mkazi wa Arusha ni la kipumbavu sana lililojaa ubaguzi. Mtanzania anaruhusiwa kuishi popote ndani ya Tanzania bila kuvunja sheria. Hata wewe unaweza kwenda kuishi mkoa mwingine na ukagombea nafasi ya uongozi ukiwa huko.
 
Kwani na yeye ametoa wapi hela za kununua ngombe 400 na kugawa bure
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha kufanya uchunguzi wa upotevu wa kiasi cha fedha shilingi milioni 400 zilizochangwa na wadau kwa ajili ya kusaidia waendesha pikipiki maarufu bodaboda.

Fedha hizo zimepotea na hazijapata majibu kuanzia mwaka 2016, baada ya harambee iliyoongozwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo, wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Makonda ameelekeza TAKUKURU kumuhoji Mbunge Gambo kwa kuwa alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa ukusanyaji wa fedha hizo.

Maelekezo haya ameyatoa leo kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichowakutanisha wadau mbalimbali na taasisi za serikali.

"Fedha ni ngumu, tulishachangiwa hapa na matajiri shilingi milioni 400, iliwekwa kwenye akaunti, lakini ilipowekwa tukaambiwa kuwa hizi fedha ni za bodaboda na wametuchangia matajiri zetu hapa mjini. Tulipochaguliwa kuwa viongozi wa bodaboda na kwenda kuangalia kwenye akaunti hatukukuta hata shilingi mia moja, sasa tunauliza zimeliwa na nani? Mimi nilipambana hadi TAKUKURU," alisema mmoja wa viongozi wa waendesha bodaboda na kuongeza,

"Mbunge (Gambo) alielekeza shilingi milioni 120 iende kwa akina mama kwenye kikundi kinachoitwa UWAWAJA."

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, amesema kwamba, alikumbana na madai ya upotevu wa fedha hizo hata alivyokuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi pindi alipofanya ziara katika mkoa huo.

"Hata nilipokuja hapa niliambiwa kuna hela za boda, sasa hivi mkiniambia kuwa mna milioni 20 ambazo Mheshimiwa Rais amechanga na mnatakiwa milioni 100 ili mpewe pikipiki, najiuliza hizi fedha zinazochangwa sasa zitakuwa salama vipi wakati zile milioni 400 hazijulikani ziko wapi?" aliongeza Makonda.

Kwa sasa, wananchi wanajiuliza ni nani alihusika na upotevu wa fedha hizo, huku matumaini yakielekezwa kwa TAKUKURU kufanya uchunguzi wa haki na kutoa majibu kwa umma.
Pia soma:
Pia TAKuKURU wasisahau kuhoji hela za kununua Ng'ombe 400 zimetoka wapi?
 
Back
Top Bottom