Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani. Kesi yaahirishwa baada ya mashahidi kukosekana Mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ole Sabaya mtu mwenye tuhuma zisizo na idadi , leo tena amefikishwa mahakamani huko Arusha akiwa amevaa Suti iliyopauka ili kusikiza kesi zinazomkabili.

Kesi za aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano, ambao wanakabiliwa na mashtaka sita na mawili ya ujambazi wa kutumia silaha zitaanza kusikilizwa leo.

Mashitaka mawili ambayo leo yanatarajiwa kuanza kusikilizwa ni ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo mawakili wa Serikali, Tumaini Kwema, Abdallah Chagula na Tarsila Garvas walieleza kuwa upelelezi wake umekamilika.

Mashitaka hayo yatafikishwa leo mbele ya mahakimu wawili tofauti; Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha.

-----UPDATE-----

Mahakama ha Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kesi inayomkabiri aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya mara baada ya mashahidi wa kesi ya unyanganyi wa kutumia silaha kutofika Mahakamani.

Mawakili wa Serikali waliiambia Mahakama kuwa Shahidi amepata udhuru na kuahidi kuwa atakuwepo siku nyingine itakayopangwa kesi hiyo.

Kesi imeahilishwa mpaka Tarehe Julai 16, 2021.

--
 
Huyu atashinda kesi tena kwa ujinga wa maccm

Kama aliweza kushinda ile ya kitambulisho fake cha TISS.

Hakika CCM ni ile ile angalia alivyoanza kubadilisha suti

Ukute hata atokei mahabusu huyu mwizi
 
Katiba Mpya inazidi kupata umuhimu ili kuondokana na watu wa aina hii kwenye jamii wanaotumia vibaya madaraka yao kuwaumiza raia wasio na hatia, kisa tu ni wapinzani wao kisiasa.
 
Huyu atashinda kesi tena kwa ujinga wa maccm

Kama aliweza kushinda ile ya kitambulisho fake cha TISS.

Hakika ccm ni ile ile angalia alivyoanza kubadilisha suti

Ukute hata atokei maabusu huyu mwizi
Usichokijua sawa na usiku wa Giza,hivi watu humu jamiiforums mnajifanya kujua kila kitu kwann?

Ukiwa mahabusu unavaa nguo yoyote ile muelewe hilo acheni kujitia kujua kila kitu

Mfungwa ndio anavaa nguo maalum.

Huyo jambazi yupo mahabusu Wala hatokei popote, anatokea gerezani
 
Mbona haraka sana hivyo si juzi juzi tu alikuwa huko.
 
Mtuhumiwa anakuwa presumed innocent until mahakama itakapo-prove otherwise.

Acheni kuchafua watu. Wengi wenu mmejawa chuki kwa kumuona mwenzenu anafanikiwa.

Hiyo chuki na roho mbaya mliyonayo haitawafikisha popote. Badilikeni.
 
Huyu atashinda kesi tena kwa ujinga wa maccm

Kama aliweza kushinda ile ya kitambulisho fake cha TISS.

Hakika ccm ni ile ile angalia alivyoanza kubadilisha suti

Ukute hata atokei maabusu huyu mwizi
Haki ya Mungu akishinda hii kesi raia watamalizana nae uraiani, ameumiza watu wengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…