Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani. Kesi yaahirishwa baada ya mashahidi kukosekana Mahakamani

Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani. Kesi yaahirishwa baada ya mashahidi kukosekana Mahakamani

Mahakama itende HAKI kwa wale walioumizwa na huyo jamaa ili kuepuka Raia wenye ghadhabu kujichukulia Sheria mikononi.
 
Ole Sabaya mtu mwenye tuhuma zisizo na idadi , leo tena amefikishwa mahakamani huko Arusha akiwa amevaa Suti iliyopauka ili kusikiza kesi zinazomkabili

Kesi za aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano, ambao wanakabiliwa na mashtaka sita na mawili ya ujambazi wa kutumia silaha zitaanza kusikilizwa leo
MAHAKAMA IMESHINDWA KUTHIBITISHA PASI NA SHAKA TUHUMA ZINAZOMKABILI OLE SABAYA ZA UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA
 
Eti atashinda Kesi,ashinde kivipi wakati Ushahidi dhidi ya tuhuma zake umenyooka kama rula!!!atachukua mvua ili aolewe kabisa Jela matako huyu,katutesa sana mjini hapa
Unakumbuka kesi ya zombe wewe ?
 
Kwa mwenendo ulivyo namshauri mama amuachie Sabaya na amrudishie cheo chake cha mkuu wa wilaya pale Hai... na ikimpendeza pia amrudishe Makonda pale Dar es salaam a awape mamlaka zilezile walizopewa na mwendazake...

Kuna vijogoo sasa vinajifanya pumzi imerudi wakati vikuwa vimeufyata na kubaki nyuma ya keyboard huku wengine wakikimbia kimbia huku na kule....

Sio kwamba wengine tulikuwa tunakubaliana na JPM hapana, lakini kutokubaliana na JPM kimtazamo hakutufanyi tukubaliane na ujinga wa wanasiasa wapumbavu wanaotaka nchi iendeshwe na fikra zao na mashinikizo yao..
 
Mahakima ha Hakimu Mkaazi Arusha imeahilisha kesi inayomkabiri aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya mara baada ya mashahidi wa kesi ya unyanganyi wa kutumia siraha kutofika Mahakamani.

Mawakili wa Serikali waliiambia Mahakama kuwa Shahidi amepata udhuru na kuahidi kuwa atakuwepo soku nyingine itakayopangwa kesi hiyo.

Kesi imeahilishwa mpaka Tarehe July 16 2021.
View attachment 1837740
 
Kwenye hii kesi ,Rais Samia shituka kila siku kesi inasogezwa mbele kisa mashahidi hakuna.

Watu walewale waliomzushia Bashiru kwamba amechota hela hazina mara baada ya Magufuli kufariki ndiyo walewale waliomzushia Sabaya tuhuma nyingi zisizo na ushahidi ndiyo maana hawatokei mahakamani.

Jana CAG amesema hakuna hela ypyote iliyochotwa mara baada ya kifo cha rais Magufuli.
==
Kesi ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake watano wanaokabiliwa na mashtaka sita yakiwemo mawili ya ujambazi wa kutumia silaha imeahirishwa hadi Julai 16, 2021.

Juni 18, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Sabaya na wenzake wawili walisomewa mashtaka mawili na leo Ijumaa Juni 2, 2021 ndio ilikuwa siku ya mashahidi kuanza kutoa ushahidi wao lakini ikaelezwa kuwa hawapo.

Siku hiyo ilielezwa kuwa Februari 9, 2021 katika mtaa wa Bondeni, Sabaya akiwa na watuhumiwa wenzake wawili walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kuvamia duka la Said Saad na kuwaweka chini ya ulinzi.

Ilielezwa kuwa Sabaya na walinzi wake, Sylivester Nyingu (26) maarufu Kicheche na Daniel Mbura(38) walitenda kosa hilo baada kumfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetini na kumuibia 390,000.

Katika tukio hilo wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao pia wanatuhumiwa kumpiga mateke kumtishia silaha na kumpora simu na Sh35,000 Ramadhani Ayoub. Watuhumiwa hao ambao walikana mashtaka yanayowakabili wanatetea na wakili, Moses Mahuna.

Leo katika mahakama hiyo ilidaiwa mashtaka mengine manne yanayowakabili upelelezi wake bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Tarsila Garvas aliomba kupangwa siku nyingine ili mashahidi hao waanze kutoa ushahidi wao na hakimu mkazi mkuu, Salome Mshasha alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 16, 2021.
20210702_125336.jpg
Screenshot_20210702-125102_millardayo.jpg
 
Aendelee kukaa sero tu apate utamu wa wale mahabusu aliokua anawasweka bila dhamana halafu uchunguzi haujakamilika
 
hamna kesi hapo ni siasa chafu.
ushabiki mtupu.
ikija tena hakuna shahidi futilia mbali takataka ya kesi hii, mnamtaabisha mtu wa watu buree tu.
huyu DC alifanya kazi kubwa sana ktk wilaya ya Hai, nimefuatilia clips nyingi kafanya kazi ambazo zilimjengea maadui wengi zaidi; wafanya biashara, wanasiasa n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hii kesi ,Rais Samia shituka kila siku kesi inasogezwa mbele kisa mashahidi hakuna.
Watu walewale waliomzushia Bashiru kwamba amechota hela hazina mara baada ya Magufuli kufariki ndiyo walewale waliomzushia Sabaya tuhuma nyingi zisizo na ushahidi ndiyo maana hawatokei mahakamani.
Jana CAG amesema hakuna hela ypyote iliyochotwa mara baada ya kifo cha rais Magufuli.View attachment 1837735View attachment 1837736
Tulia wewe mama, inatakiwa iwe hivyo hata miaka miwili. Hajamaliza hata miezi mi5 mshaanza kulalamika? Kuna waliokaa miaka 8
 
Njama hizo kupunguza temper ya wananchi baadae utasiki DPP hana nia ya kuendelea na kesi
 
Kwenye hii kesi ,Rais Samia shituka kila siku kesi inasogezwa mbele kisa mashahidi hakuna.
Watu walewale waliomzushia Bashiru kwamba amechota hela hazina mara baada ya Magufuli kufariki ndiyo walewale waliomzushia Sabaya tuhuma nyingi zisizo na ushahidi ndiyo maana hawatokei mahakamani.
Jana CAG amesema hakuna hela ypyote iliyochotwa mara baada ya kifo cha rais Magufuli.View attachment 1837735View attachment 1837736
Uyu jamaa soon ataachiwa na kupangiwa kazi nyingine
 
Wanafanya hivi hili siku za kukaa gerezani kwa huyo dogo Sabaya ziongezeke kidogo
 
Back
Top Bottom