Arusha: Viongozi wanne wa Madereva wamekamatwa kufuatia mgomo wa usafiri uliobuka Mei 25, 2026

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Your browser is not able to display this video.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude amesema Viongozi wanne wa Madereva wamekamatwa kufuatia mgomo wa usafiri uliobuka Mei 25, 2026 Jijini humo.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Mkude amesema Viongozi hao walikamatwa ili watoe msaada kwanini wamefikia hatua ya kuwaambia wenzao wagome.

“Kuna Watu wamevunjiwa mali zao, gari la Mtu limevunjwa Vioo kwa sababu alipakia abiria, Mtu kama huyu hakufanya kosa la mgomo bali ni ameharibu mali ya Mtu”

Katika hatua nyingine, Mkude amewataka Madereva kufuata Sheria ikiwa ni pamoja na kutoza nauli zilizopangwa pamoja na kuitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA).

Millard Ayo

Pia soma Mgomo wa Daladala Arusha, Dereva Daladala wailalamikia LATRA, wadai haiwatendei haki
 
Ndio inasuluhisha tatizo? Hawa viongozi huwa wanawaza nje ya box kweli?
Una deal na outcome huku mzizi wa tatizo unaacha pale pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…