DOKEZO Arusha: Wananchi Meru walalamikia maghala ya Serikali kuwauzia mahindi ya chakula. Serikali yasema utaratibu utabadilika, kupelekwa kila tarafa

DOKEZO Arusha: Wananchi Meru walalamikia maghala ya Serikali kuwauzia mahindi ya chakula. Serikali yasema utaratibu utabadilika, kupelekwa kila tarafa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Wananchi wilayani Arumeru, wametoa malalamiko yao dhidi ya serikali baada kuuziwa mahindi kilo moja kwa sh. 885.

Baadhi ya wananchi wameshindwa kununua mahindi hayo kutokana na hali ngumu ya maisha iliyotokana na ukame kwa madai kuwa serikali ilitakiwa itoe mahindi hayo bure kwa wahanga na sio kufanya biashara na wananchi.

Serikali inatuzuuzia mahindi kilo moja kwa sh. 885 ambapo tunatakiwa kulipa pesa hizo katika ofisi za Kijiji na baada ya hapo ni kufuata mahindi hayo katika ghala la serikali lililopo kikatiti ambapo gharama za nauli ni zaidi ya sh. Elf tano kutoka hapa kata ya Nkoarua,wengi tumeshindwa kufanya hivyo. Anasema Mama Elisha.

Baadhi ya wananchi wanahoji inakuwaje maghala ya serikali yanahifadhi mahindi kwa ajili ya kuwauzia wananchi na sio kutoa msaada kipindi hiki ambapo wamekumbwa na ukame tu mkubwa wa chakula unaopelekea makundi ya Wakina Mama na watoto kupita nyumba kwa nyumba kuomba chakula katika Kata za Mjini.

=========

Tamko la Serikali kuhusu utaratibu wa mahindi hayo.

Arumeru.jpg


SERIKALI YASEMA UTARATIBU UTABADILIKA
Kuhusu suala la kutumia umbali mrefu kupata mahindi hayo, Afisa Kilimo wa Meru, Kombo Daico amesema:

“Ni kweli hata mimi nimejadili na Mkurugenzi hilo suala tumewaachia kwa NFRA ambao ndio wanasafirisha mahindi, mwanzoni wao walikuwa wanapeleka mahindi kwenye senta moja tu ya Wilaya.

"Lakini kwetu ilivyoonekana hiyo changamoto, tukazungumza nao na wamekubali kupeleka kila tarafa, kwahiyo wamelifanyia kazi, hapa tuna tarafa tatu, Mbuguni, King’ori na Poli ndio maelekezo tuliopewa na NFRA ambao walipewa mamlaka ya kusambaza hicho chakula na Wizara.

“Lakini tumewaambia hapo kuna shida, mwanzoni ilikuwa kituo ni kimoja tu, hivyo sasa hivi watagawa ngazi ya Tarafa na baada ya hapo watu wetu ndio watachukua kutokea hapo.

“Hakuna nyongeza yoyote ya bajeti iliyowekwa katika zoezi hilo, litawahusu wenyewe wanaosambaza.”
 
Kumekuchaaaaaaa!!
Njaa again, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Arumeru na 'Arusa' kwa ujumla ni dona kantri inayojitolesheleza kwa kila kitu imekuaje wananchi wake walie lie njaa na hata kukosa 88,500/- kununua gunia la mahindi?
 
Arumeru na 'Arusa' kwa ujumla ni dona kantri inayojitolesheleza kwa kila kitu imekuaje wananchi wake walie lie njaa na hata kukosa 88,500/- kununua gunia la mahindi?
Watu wamesema kuna ukame, sasa hizo hela wanapata vipi na shughuli zao kubwa ni kilimo?. Hawana pesa.
 
Wananchi wilayani Arumeru, wametoa malalamiko yao dhidi ya serikali baada kuuziwa mahindi kilo moja kwa sh. 885

Baadhi ya wananchi wameshindwa kununua mahindi hayo kutokana na hali ngumu ya maisha iliyotokana na ukame kwa madai kuwa serikali ilitakiwa itoe mahindi hayo bure kwa wahanga na sio kufanya biashara na wananchi...
Magufuli angewajibu vizuri "Siyo kazi ya serikali kulisha wananchi" wanamlalamikia nani si wangejiwekea akiba? Kwanza hiyo bei ni ya kawaida sana, serikali haina shamba iliyanunua hayo mahindi, kuyasaririsha na kuyatunza. Halafu ni waongo mno, Kikatiti nauli ya sh,tano imetoka wapi. Wajilishe wenyewe serikali ina majukumu mengine siyo kuwalisha hao watu. Hawana aibu?
 
Back
Top Bottom