Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wananchi wa kata mbili za Sinoni na Lemara wameshikwa na mchangao wa aina yake baada ya halmashauri ya jiji la Arusha kurudisha pesa walizokuwa wametoa kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambalo ni kiunganishi kati ya kata hizo mbili.
Awali baada ya pesa hizo kupatikana kutoka halmashauri Ofisi ya kata ya Sinoni ililazimika kutafuta mkandarasi wa Ujenzi wa daraja hilo kwa kubandika tangazo kwenye ofisi za kata hizo tangu mwezi wa tatu lakini baada ya muda ukimya uliendelea hivyo hadi sasa na hivyo wananchi kuhoji kulikoni ndipo walipojibiwa kuwa pesa zimerudishwa tena halmashauri bila kujulikana sababu maalumu.
Ni miaka zaidi ya mitano sasa tangu kukatika kwa mawasiliano kati ya kata hizo mbili baada ya daraja lilokuwepo kusombwa na Mvua na hivyo wananchi na wanafunzi kulazimika kupita ndani ya maji kuelekea upande wa Pili.
Wananchi wanahoji kuwa mvua za elnino zipo karibu kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa wanafunzi na watu wazima wanaovuka mto huo je ni sawa wanachofanyiwa na serikali yao?