Arusha: Wananchi walia na kituo cha mabasi makubwa ya abiria ya kwenda mikoani

Arusha hata miaka 50 ijayo haiwezi fikia Nairobi, wala huwezi shindanisha Dar na Nairobi.
 
Arusha ndio mnataka kuifananisha na Mwanza kweli?

Arusha inapambana na miji kama Musoma, Geita, Katoro, nk. Kahama sasa sio level za Arusha tena.

Soon senta kama Kagongwa ama Runzewe zinaipita Arusha.
Kahama stand kubwa imebanana Sana, japo wanasema zipo stand ndogo tatu za mikoa jirani.

Sent from my TECNO CE9 using JamiiForums mobile app
 
Sijui kama wale Wameru na Waarusha kindaki ndaki watakuelewa. Nilijaribu kuwaeleza nikaambulia matusi...

Mkuu una akili kubwa sana!👏👏
 
Hapoa Arusha wanaweza wakafanya mpango wakahamisha hayo makaburi nyuma ya stendi Ndogo kisha eneo lote mpaka huku stendi ndogo likiwa stendi kubwa ya mabasi.Yaani kuanzia hapo stadium kote kunakuwa ni STAND.Inawezekana kabisa
Stendi zipelekwe nje ya mji zikasaidie kukuza maeneo ya pembezoni.
Miji mingine ilipata hii akili 20 years ago...
 
uwanja wa Abeid Karume ndio upi huo?wakazi gani hao wa Arusha wameyasema hayo
 
Kusema kuwa serikali inashindwa kupata maeneo ni kukiri kuwa udhaifu wa serikali. Mbona serikali ikitaka kufanya miradi kama ya barabara, umeme au maji chap chap wanafidia watu na kutekeleza miradi husika??

Iko hivi: Kinachotokea Arusha ni mgongano wa maslahi na fear of the unknown.
Unakuta viongozi wafanya maamuzi wamewekeza kwenye majengo na biashara nyingi zilizosongamana pale mjini.

Wazawa nao wanahofia mizunguko ikihama maisha yatakuwaje.

Tusishau vile vile historia mbaya ya Arusha uliotokana na ile mitandao ya uhalifu! Japo mambo yamebadilika lakini watu bado wana hofu! Kuna maeneo ikifika saa 12 na nusu jioni tayari hata usafiri unaanza kusua sua, maduka yashatiwa kufuli... Watu wana hofu!

Kwa mji unaojinasibu kuwa ni lango na kitovu cha utalii, serikali ya Jiji/mkoa inatakiwa iwaze ndani na nje ya boksi. Kinachoendelea sasa pale Arusha ni kero na aibu!

Kongole kwa A to Z, Braeburn, Bansal, Lenagro, Nida, Auwasa, n.k walioamua kujiwekeza kule nje ya mji.
 
Mjini kupoa pia ni maendeleo. Kwa sasa ule mji wa Arusha unatia kichefu chefu
shida kubwa ya tanzania ni planning. serikali imewaachia watu waendeleze miji kiholela, miji ikikua (kiholela) ndipo inajifnaya kuanza kujali
 
🤣🤣 Hizo Zitakuwa stand au vituo vya daladala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…