Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wakazi wa kata ya Sinoni, na Ungalimited wanaotumia barabara kuu ya Engosengiu inayotokea mjini kuelekea katika Kata hizo mbili wamedai kuchoshwa na ubovu wa barabara hiyo kiasi cha kuwaletea usumbufu mkubwa hata katika vyombo vyao vya moto.
Baadhi ya madereva wa Bajaji na Hiace wanaotumia njia hiyo wamesema ubovu wa barabara hiyo pamoja na mashimo unawaharibia magari yao mara kwa mara.
Baadhi ya wananchi wanaotumia barabara hiyo wamedai wakati wa jioni madereva kubadilisha ruti na pia kupandishiwa nauli hivyo kuwaletea usumbufu hasa nyakati za jioni.
Wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa kila mwaka hudanganywa na viongozi kuwa barabara hiyo itawekwa Lami lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea.
Miaka mitatu iliyopita madereva wa Hiace waligoma wakishinikiza kuwekewa lami lakini badala yake wakawekewa kifusi cha udongo na kuahidiwa kuwekewa lami lakini hadi sasa hali ni Ile ile.
Bara bara hiyo ipo katika halmashauri ya jiji la Arusha.