kitendo cha kuwachukulia hatua muuguzi na Afisa elimu Arusha nimefurahi kidogo
hongera sana baraza la Wauguzi na wakunga
hongera sana wizara ya Afya
hongera sana OR Tamisemi
lakini kiukweli sijaridhishwa kabisa na hatua zilizochukuliwa
ilitakiwa hawa watu kwanza wawekwe ndani kwa saa 48,
kisha wafukuzwe kazi kabisa sio kusimamishwa,
mambo serious wao wanaleta mizaha ya kijinga,
serikali na wizara wanajitahidi kuelimisha Raia wake ili tupone na janga hili la dunia halafu wapuuzi wachache wanaleta ujinga, ni dharau dhidi ya Rais au?
hawa watu wawekwe ndani mara moja