Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Watu wenye ubongo matope kama wewe ni hasara kwa nchi. Hivi mtu mwenye akili zake anaweza kuona suala la bodaboda lilipofikia kuwa kila kitu kiko sawa? Au wamachinga waliozagaa kila sehemu mtu na akili zako unasifu na kusema ni jambo zuri? Bodaboda na umachinga ni zao la ukosefu wa ajira unaotokana na mipango mibovu ya serikali kwa sababu ya viongozi wenye akili ndogo kama wewe. Na hapa sizungumzii tu ajira za ofisini. Tanzania tuna ardhi kubwa sana na tungekuwa na viongozi wenye vision basi kilimo na usindikaji wa mazao i.e. viwanda ingekuwa ndiyo ajira kwa vijana wengi. Anyways, kuna siku mtaelewa ni kwa nini Lema yuko sahihi. Siku ambayo bodaboda na wamachinga watakapoamua kudai haki yao kwa nguvu.
Big up sana hii ndo akili sawa....nakubali
 
Hapana mkuu unajua viongoz wa afrika hasa Tz wanatumia mfumo wa umaskini kama mtaji wao kwa sasa.....
Bodaboda
Vikoba
Ect.....

Embu fafanua ni Kwa namna gani bodaboda ni umaskini?
Ikiwa kijana anayeendesha bodaboda anapata kipato Kwa Siku 10,000/=
Alafu uje kwenye dhana ya umaskini Kwa Muktadha wowote ule uwe Muktadha wa kisomi, kidini, kimila.
Weka mbali kasumba na dhana potofu.
 
Lema ametumia platform alipewa na ccm kuropoka uongo mwingi mwingi sana,sijali huo uongo wake kwasababu haubadilishi ukweli wowote

Ila ninachotaka kusema lema anaongea uongo wa kumiliki mashimo kumbe ni uongo hana shimo ila alipokea pesa ya waarabu flan ili yeye awe front

Na kwenye mashimo ameweka majina ya ndugu yake ili kukwepa kodi kwasababu anadaiwa madeni mengi

Lema aliyekaribia kufilisika kukaribia Hadi kuuza nyumba ya kuishi kutokana na mamikopo yake aliyokopa kichwa kichwa yakala mieleka

Lema usiongee bla bla game ndio kwanza linaanza,kesho ni njema sana kwa watu unaowadhani wabaya kwako

Lamba asali kimya kimya
Mwenye Jimbo lake amerejea tafuteni shughuri nyingine zakufanya.
 
Unajua maana ya Laana?
Au huyo lema anajua maana ya Laana?

Elimu ni muhimu. Ninyi ndio mnafanya Vijana wasijiajiri Kwa dhana potofu na zakijinga
Ubongo wako ni finyu na sitegemei uone maana ya alichokisema Lema. Watu kama nyie mpaka mambo yatakapoharibika ndiyo mnaelewa. Mtu mwenye akili zako unasifia nchi yenye kundi la vijana amabao walitakiwa kuwa kwenye uzalishaji kukaa barabarani na pikipiki kutwa wakisubiri kukusanya sh 10, 000! Ni kweli kuwa hamuoni hili ni tatizo?
 
Lema kweli ni nabii kiongoz ana maono makubwaa japo alikua mbali na inch lakini kaliona hili...
Saiv kati ya vijana 100 basi hapa70 ni bodaboda, 10 job less kabisa, 10,wabiga debe ect, 10 ndo wanaajira rasmi hapo boda boda atafanya biashara gani au watabebana wao kwa wao huko badaye..........
 
Embu fafanua ni Kwa namna gani bodaboda ni umaskini?
Ikiwa kijana anayeendesha bodaboda anapata kipato Kwa Siku 10,000/=
Alafu uje kwenye dhana ya umaskini Kwa Muktadha wowote ule uwe Muktadha wa kisomi, kidini, kimila.
Weka mbali kasumba na dhana potofu.
Iyo 10k per day ilikua zaman saiv wengi wanashindwa mikataba hawamudu
 
una akili timamu ?
Wanataka tu kuambiwa Lema amewadharau bodaboda issues za oppression hawaoni ka zinahitaji kujadili.
Utafikiri hawajaenda shule. Wajue kuwa kipindi cha waafrika kuelekea uhuru major ussue ilikuwa oppression na waandishi wengi kipindi kile waliandika kuhusu hilo, mashairi mengi yaliandikwa.
Baada ya uhuru watawala weusi waliwa betray waafrika wenzao wakageuka wakoloni weusi.
Kipindi hiki watawala wamegundua kuwa ili waendelee kutawala mbinu zote za kibabe kwa kutumia vyombo vya maguvu lazima vitende kazi kikamilifu. Mbinu hii ilitumiwa na wakoloni sana. Sasa Lema anabainisha kwamba, jamani haya mambo ni mabaya lakini wajinga na walafi hawamwelewi, wanakuja na kejeli na matusi. Lema ni mpaaza sauti kwa wanaoonewa yeye anaweza kupenya lakini vipi wale ambo hawajui wapenye wapi. Nawaonea huruma hawa wajinga.
 
Ubongo wako ni finyu na sitegemei uone maana ya alichokisema Lema. Watu kama nyie mpaka mambo yatakapoharibika ndiyo mnaelewa. Mtu mwenye akili zako unasifia nchi yenye kundi la vijana amabao walitakiwa kuwa kwenye uzalishaji kukaa barabarani na pikipiki kutwa wakisubiri kukusanya sh 10, 000! Ni kweli kuwa hamuoni hili ni tatizo?

Kwako kipi Bora?
Kufanya uzalishaji ulipwe 140,000 Kwa mwezi
Au kufanya bodaboda upate Kwa Siku 10,000/=

Sijasema hao wazalishaji WA viwandani wanafanya vibaya, Nop! Kila mmoja afanye anachoona kipo Mbele yake na anachoweza kufanya.

Kufanya kazi sio tatizo, hakuna serikali duniani inayotaka Vijana wake wateseke, ni kwamba Serikali na taifa lenu na mataifa ya Afrika tayari yameshazidiwa Step na washidani wao wazungu.

Wewe hata ungepewa Urais Kwa miaka 100 huna ambalo utafanya,
Ni vigumu kuelewa mambo haya
 
Embu fafanua ni Kwa namna gani bodaboda ni umaskini?
Ikiwa kijana anayeendesha bodaboda anapata kipato Kwa Siku 10,000/=
Alafu uje kwenye dhana ya umaskini Kwa Muktadha wowote ule uwe Muktadha wa kisomi, kidini, kimila.
Weka mbali kasumba na dhana potofu.
Bodaboda siyo kuwa tu laana, bali ni bomu ambalo litalipuka muda wowote kama radical measures hazitachukuliwa haraka sana sana. Trust me.. bodaboda ni zaidi ya laana na kuna siku itaingiza nchi yetu kwenye machafuko na kuja kurudia hali ya kawaida itachukuwa muda mrefu. Bodaboda na machinga ni kielelezo cha failure za uongozi wa nchi kutokuwa na mikakati ya kuongoza. Ni mtu mjinga tu ndiye hawezi kuona hili.
 
Iyo 10k per day ilikua zaman saiv wengi wanashindwa mikataba hawamudu

Wanashindwa Kwa sababu sio waaminifu, hawapendi hiyo kazi, wanajiweka Rafu, Hawana nidhamu ya fedha n.k.

Hiyo biashara nimeshaifanya miaka 4 iliyopita, naelewa nikisemacho.
 
Wanashindwa Kwa sababu sio waaminifu, hawapendi hiyo kazi, wanajiweka Rafu, Hawana nidhamu ya fedha n.k.

Hiyo biashara nimeshaifanya miaka 4 iliyopita, naelewa nikisemacho.
Kwa maelezo yako haya umekubali kua ni kazi iliyojaa laana ndani yake..
 
Kwa hiyo Viongozi wa Chadema ni wavaa baibui wastaafu
 
Ukitaka kujua siasa ni uwenda wazimu jitenge nayo alafu angalia wanao mtetea lema Kisha chukua maneno hayohayo yageuze mfano angekua ameyasema mtu wa ccm ungeona watu haohao wanao muunga mkono lema jinsi wangeyalaani hayo maneno pengine hata Lema mwenyewe angeyalaani
 
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mh Godbless Lema amesema alilkimbia nchi Baada ya kukoswakoswa kuuawa mara kadhaa na kutekwa pia

Lema amesema kama ilivyokuwa kwa Tundu Lisu na Ben Saanane hata yeye alikuwa akipokea vitisho vingi na Nyumba yake ya Machame ilichomwa moto

Hata alipoenda kukagua Migodi yake ya madini imlazimu avae baibui ili kuwakwepa maadui zake

Lema anasema ilifika Wakati mkewe aliwekewa madawa ya kulevya na kuna Wakati alibambikiwa kesi ya Wizi wa Gari ambalo mali yao

Lema alikuwa akihojiwa na Watangazaji nguli wa Clouds Media

Source: Clouds
Huyu anaropoka sana anaatack watu hovyo hovyo
 
Bodaboda siyo kuwa tu laana, bali ni bomu ambalo litalipuka muda wowote kama radical measures hazitachukuliwa haraka sana sana. Trust me.. bodaboda ni zaidi ya laana na kuna siku itaingiza nchi yetu kwenye machafuko na kuja kurudia hali ya kawaida itachukuwa muda mrefu. Bodaboda na machinga ni kielelezo cha failure za uongozi wa nchi kutokuwa na mikakati ya kuongoza. Ni mtu mjinga tu ndiye hawezi kuona hili.

Hapo kwenye Laana ndio unashindwa kupaweka Sawa.
Laana maana yake ni nini?

Bodaboda sio tatizo, Hilo liko wazi.
Ni Ajira nzuri mno inayohitaji utaratibu tuu.
Kusema bodaboda ni Laana Wakati sio shughuli haramu ni dalili ya kutojua maana ya istilahi "Laana"

Ninarafiki zangu wanamiliki makampuni yanayohusiana na hizo bodaboda.
Wanafanya Free delivery na kusafirisha packaging Kutoka eneo moja kupeleka eneo jingine. Wanapata Pesa nzuri tuu(ingawaje Hii sio kipimo)
Kazi yoyote inahitaji Akili ya MTU na mtazamo chanya Kati kazi hiyo
 
Propaganda hizi za Western media. Hao vipi wajuba?

Ila awamu ya tano...........................??
 
Wewe angekuwa Mama yako au Baba yako au watoto wako wamepotea hujaona hata makaburi yao ungekubali huo ujinga

Unaongea kwa kuwa hayajagusa familia yako, Watu wanasema msiba ni kwa jirani

Watu lazima watoe uchungu wao wote wa moyoni ndio maana wanasema iundwe Tume ya maridhiano kama yalivyofanyika Rwanda baada ya mauaji ya kimbari

Lazima ukweli usemwe ili yasijirudie tena kwa wajukuu zetu

Tena hii kampeni ilipasa ccm waiendeshe nchi nzima kusema utekaji na kupoteza kwa watu

CCM kama walivyo fanya kwa Ole Sabaya ilipasa wafanye kwa DPP, Paul Makonda, Humprey Pole Pole na Bashiru Ally

Wote Walio husika na kupora Mali za watu, Kuteka, kubaka Yapasa wasemwe hadharani na wachukuliwe hatua kama Sabaya
Wazalendo Wana kazi sana
 
Ukitaka kujua siasa ni uwenda wazimu jitenge nayo alafu angalia wanao mtetea lema Kisha chukua maneno hayohayo yageuze mfano angekua ameyasema mtu wa ccm ungeona watu haohao wanao muunga mkono lema jinsi wangeyalaani hayo maneno pengine hata Lema mwenyewe angeyalaani

Lema mwenyewe juzi kajikosoa kuwa alikosea
 
Back
Top Bottom