Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Lkn ndio karud nchini kwa mara ya kwanza je haitakiw kusema madhira waliyopitia? Kusema ukwel uovu uliotaka kufanyiwa ni dhambi? Kwann mchukie watu kusema maumiv waliyopitia? Na kwann yasisemwe? Sheria ya Nchi inakataza? Kuna maumiv gan mnapata wahanga wakisema waliyopitia?
Lema muongo kama alikuwa anakwenda kukagua migodi yake kwa kuvaa baibui, ukafikiri Serikali aina watu wake huko kwenye migodi? Serikali ikikutaka hata uchimbe shimo inakukuta huko kwenye shimo, Serikali kama ilikuwa inamwitaji hatawakati wa kuvuka mpaka angelikamatwa tu, mbona Nyarandu alirudishwa na akuna kilichompata!na mpaka Sasahivi yuko ccm anakula bata; Chadema uongo wanaotunga kuaribu sifa za Magufuli utawarudia tu, hauwezi kupanda kwa kukanyaga mtu au kimchafua ukadhani wewe utakuwa salama.Akuna jipya ambalo Magufuli alitenda ambalo watangulizi wake hawakuwai kulitenda.
 
Anaandika, Robert Heriel

  • Kazi na kuwa kipato duni hakuifanyi kazi hiyo kuwa ya Laana.
  • Kazi kufanywa na watu wasio na Elimu hakuifanyi kazi hiyo iwe ya Laana.
  • Kazi kufanywa pasipo kufuata utaratibu hakuifanyi kazi hiyo kuwa na Laana.

Kazi ni ibada kwa wale waamini na waaminio. Kazi yoyote halali aifanyo mtu ni ibada. Lakini pia kufanya kazi kisheria ni kutimiza wajibu ndani ya taifa. Kusema kazi Fulani ni Laana kisa mapato ya Kazi hiyo ni duni, ni dharau na ujinga wa msemaji.

Kazi kuwa hatarishi haimaanishi kuwa ni kazi ya Laana. Bodaboda ni kazi kama kazi zingine, Umachinga ni kazi kama kazi zingine, Udalali ni kazi kama kazi zingine, Ukuli na upiga Debe ni kazi kama kazi zingine.

Ni mtu mpumbavu na mjinga asiyeelewa mambo hayo.

Lena anadharau sijui Vikoba kisa watu wanachanga bukubuku au elfu tatu, hizo pesa zinazochangwa sio pesa za wizi, ni pesa halali, hawajamuibia mtu. Ni jasho Lao, dharau na Kiburi sio Kizuri.

Kwa Watu waungwana, wasomi walioelimika, wenye maadili na hofu ya Mungu huwezi kuwasikia wakiongea mambo ya hovyo kama hayo.

Lema kama mtu ajionaye mwenye akili, exposure na aliyewahi kuwa kiongozi kwa nafasi ya Ubunge, pamoja na sisi wasomi na watu wa serikali pamoja na viongozi wa dini tulipaswa kufanya haya yafuatayo;

1. Kuzitambua kazi mpya zilizozuka hivi karibuni kutokana na mapinduzi ya Teknolojia na ujio wa Utandawazi. Kazi kama za bodaboda, umachinga, kazi za mitandaoni, kazi za udalali n.k, ni muhimu kuzitambua.

2. Kuziwekea Sera, Sheria na Kanuni ili kuwapa Haki na Fursa watakaojiingiza humo.

3. Kutunga na kuingiza mitaala ya kozi fupi na ndefu zitakazofundisha kazi hizo kwa gharama nafuu, ili kuzipa thamani kazi hizo. Kupitia Elimu na Sheria zitakazotungwa kutakuwa na maadili ya hizo kazi.

Utoaji wa Elimu utasaidia kazi hizo kutokufanywa kiholela. Kutawafanya wafanyaji wa kazi hiyo kuwa nadhifu kimavazi, pia utumiaji wa lugha fasaha na zenye nidhamu utazingatiwa kwani ni sehemu ya kazi.

4. Kuandaa mfumo wa Bima ya Afya kwa gharama nafuu inayolingana na kipato cha kazi hizo. Bahati nzuri siku hizi ipo ile Bima ya CHIF ya elfu 40.

5. Kuandaa mifumo ya ulipaji wa Kodi au Ushuru kulingana na eneo la kazi. Hii ni kumfanya kila mtu awajibike kuijenga nchi.
Kwa mfano bodaboda akilipa elfu hamsini kwa mwaka kama Kodi haiwezi kumshinda. Hata hivyo pesa hiyo lazima iingizwe moja kwa moja kwenye Leseni ili kuepusha usumbufu.

Leseni na Kodi isizidi 100,000/= kwa upande wa madereva bodaboda. Kama dereva bodaboda ni wa kuajiriwa basi watashare yeye na bosi wake gharama ya Kodi, huku Leseni ikibaki kuwa wajibu wa dereva mwenyewe. Mfano kama Kodi ni 50,000 kwa mwaka basi mmiliki wa bodaboda atalipia 25,000/= na dereva bodaboda atalipia 25,000/= Kwa Mwaka. Huku gharama za Leseni ikibaki kuwa ya dereva.

6. Angalau kila mwaka itolewe semina ya madereva bodaboda, na mafunzo kwa Madereva bodaboda kwa ngazi ya Kata.
Kazi Hii waifanye Polisi Kata wakipewa Posho kwa kazi hiyo watakayoifanya.

7. Iundwe Programu ya kuhamasisha watu kupenda kazi zao bila kujali wanapata kiwango gani cha fedha na iundwe sheria ni marufuku kwa mtu kutoa maneno ya kashfa kwa kazi zingine; yaani maneno ya kutusi, kudharau na kujeli kazi zingine, ili kukifanya kizazi kinachokuja kisije lukua na kasumba mbaya kuhusu baadhi ya Kazi. Kudharau kazi za wengine ni chanzo kikuu cha janga la ajira.

8. Kutokana na nchi yetu bado ni Maskini, kazi za umachinga haziepukiki, utaratibu maalumu hasa katika ngazi ya Serikali za Mitaa uundwe ili kuhakikisha unasimamia machinga katika maeneo waliyomo nje ya katikati ya jiji.

Wawekewe muda maalumu wa kuendesha shughuli hizo kwa kupanga pembeni ya barabara sehemu ambazo ni salama (nasisitiza sehemu ambazo ni salama). Kwa mfano kuwaruhusu wafanya shughuli hizo kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 4:00 usiku chini ya masharti yafuatayo;

  • Kuhakikisha eneo hilo ni Safi kabla na baada ya biashara.
  • Kutokupanga biashara kwa wapita njia.
  • Kutoa Ushuru kila siku labda ni buku, au kiwango chochote kulingana na eneo bila kutoa excuse yoyote ya sijui sijauza au nimeuza.
  • Kutokujenga kibanda chochote eneo hilo.
  • Kufanya biashara kwa muda uliopangwa na Serikali.
  • Kuuza bidhaa halali.
  • Kuuza bidhaa zenye thamani itakayowekwa na Serikali kama itakavyoona inafaa, labda tuseme bidhaa zitakazopangwa barabarani ziwe bidhaa ndogondogo mfano nguo, matunda, maji n.k na sio mtu aweke biashara yenye mtaji wa mamilioni ya pesa.
  • Kulipa Faini ya kiwango kitakachowekwa na Serikali au kufukuzwa eneo hilo na kutopewa eneo jingine ikiwa atavunja kwa makusudi taratibu zilizowekwa n.k.

Kitu kikubwa ambacho Lema angekisema ni kuiambia, au kuilaumu serikali kwa kushindwa kuwasaidia hao wenye hizo kazi anazoziita ni za laana. Na sio kuwaponda watu walioamua kujishughulisha kwa shughuli halali.

Au anafikiri kuwa mwanasiasa kwa kupiga mdomo na kubwabwaja kwenye majukwaa ndio kazi ya baraka au kazi bora kuliko kazi nyingine? Kila kazi ni bora itategemea na mtazamo wa anayeifanya.

Wapo Watu ambao hata uwaambie wawe wabunge hawatotaka kuwa wanasiasa. Kudharau kazi ya mtu mwingine au kipato cha mtu mwingine ni dalili ya kutokuwa muadilifu, dalili ya kiburi na ushamba fulani hivi.

Unadharau kazi ambayo kuna watu wanaendeshea familia zao, wanatoa Sadaka kwa Miungu yao, Wanahudumia watu katika maeneo yao. Wewe kwa akili yako ndogo unawakejeli.

Watu wanatafuta Maisha mazuri lakini kupata pesa nyingi haimaanishi ndio maisha mazuri. Maisha mazuri ni kupata kipato halali kwa kazi halali, kwa jasho lako. Tuache kudharau Watu na kazi zao.

Ujumbe huu umemtumia Lema kama mwakilishi wa watu wote wenye dharau na kejeli na Kiburi, sio kwa Lema peke yake.

Nawatakia Sabato njema.

Ni yule Mtibeli,

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Risala ndefu lakini hakuna content. Na inaonekana umekosa kabisa hata kuelewa context nzima ya neno hilo lilivyotumika.

Hivi alisema kuwa kazi hiyo ni ya laana kwa sababu ina kipato kidogo? Kama umeshindwa kuelewa msingi wa hoja, hata mchamgo wako wote unakuwa hauna maana.
 
Badaboda sio ajira ni kuhangaika nafsi tuu japo siwezi kuita ni laana
 
Labda kama unafikiri ulisikia na kuona mwenyewe lakini tulimsikia na kumuona akisema hivyo, kuwa bodaboda ni kazi ya Laana.
 
Hana migodi ?au ana migodi kaweka majina ya ndugu zake? Which is which?
Huyo mleta uzi ni taahira asiyejielewa, anaji-contradict mwenyewe kwa ku-force hate post yake hiyo matokea ameonekana zuzu. Hao ndiyo waliodai hawezi kurudi kwani amekimbia madeni sasa wamejigeuza spin masters waigeuze story yao kivingine, haelewi hata jinsi ilivyo rahisi kumiliki migodi kiasi kwamba anadhani Lema hawezi kumiliki migodi.
 
Badaboda sio ajira ni kuhangaika nafsi tuu japo siwezi kuita ni laana

Ndio Kula Kwa jasho Huko Mkuu.
Kila kazi inamahangaiko yake.
Huyo Lema anavyohangaika jukwaani au alivyokimbia nchi hayo sio mahangaiko?,
Ndio maana ya kazi Mkuu.
 
Anadhani kila mtu anaweza kwenda kuolewa canada kama yeye
 
Lema ametumia platform alipewa na ccm kuropoka uongo mwingi mwingi sana,sijali huo uongo wake kwasababu haubadilishi ukweli wowote

Ila ninachotaka kusema lema anaongea uongo wa kumiliki mashimo kumbe ni uongo hana shimo ila alipokea pesa ya waarabu flan ili yeye awe front

Na kwenye mashimo ameweka majina ya ndugu yake ili kukwepa kodi kwasababu anadaiwa madeni mengi

Lema aliyekaribia kufilisika kukaribia Hadi kuuza nyumba ya kuishi kutokana na mamikopo yake aliyokopa kichwa kichwa yakala mieleka

Lema usiongee bla bla game ndio kwanza linaanza,kesho ni njema sana kwa watu unaowadhani wabaya kwako

Lamba asali kimya kimya

Hoja yako ni ipi hapa?!
 
Lema aache roporopo, nimesikia pia eti anaenda kumuona Sabaya gerezani sijui leo au kesho.
Hicho ni kiherehere.
 
Ushamba tu, kuishi canada hyo miaka sijui 5 ndo anajifanya kasahau maisha ya m'tz
 
Lema ametumia platform alipewa na ccm kuropoka uongo mwingi mwingi sana,sijali huo uongo wake kwasababu haubadilishi ukweli wowote

Ila ninachotaka kusema lema anaongea uongo wa kumiliki mashimo kumbe ni uongo hana shimo ila alipokea pesa ya waarabu flan ili yeye awe front

Na kwenye mashimo ameweka majina ya ndugu yake ili kukwepa kodi kwasababu anadaiwa madeni mengi

Lema aliyekaribia kufilisika kukaribia Hadi kuuza nyumba ya kuishi kutokana na mamikopo yake aliyokopa kichwa kichwa yakala mieleka

Lema usiongee bla bla game ndio kwanza linaanza,kesho ni njema sana kwa watu unaowadhani wabaya kwako

Lamba asali kimya kimya
Kama hana mashimo anawekaje majina ya ndugu zake.
Akidanganya inaathiri vipi maisha yako na ya wengine
 
Lema muongo kama alikuwa anakwenda kukagua migodi yake kwa kuvaa baibui, ukafikiri Serikali aina watu wake huko kwenye migodi? Serikali ikikutaka hata uchimbe shimo inakukuta huko kwenye shimo, Serikali kama ilikuwa inamwitaji hatawakati wa kuvuka mpaka angelikamatwa tu, mbona Nyarandu alirudishwa na akuna kilichompata!na mpaka Sasahivi yuko ccm anakula bata; Chadema uongo wanaotunga kuaribu sifa za Magufuli utawarudia tu, hauwezi kupanda kwa kukanyaga mtu au kimchafua ukadhani wewe utakuwa salama.Akuna jipya ambalo Magufuli alitenda ambalo watangulizi wake hawakuwai kulitenda.
Umeandika utoto sana.
 
Lema ametumia platform alipewa na ccm kuropoka uongo mwingi mwingi sana,sijali huo uongo wake kwasababu haubadilishi ukweli wowote

Ila ninachotaka kusema lema anaongea uongo wa kumiliki mashimo kumbe ni uongo hana shimo ila alipokea pesa ya waarabu flan ili yeye awe front

Na kwenye mashimo ameweka majina ya ndugu yake ili kukwepa kodi kwasababu anadaiwa madeni mengi

Lema aliyekaribia kufilisika kukaribia Hadi kuuza nyumba ya kuishi kutokana na mamikopo yake aliyokopa kichwa kichwa yakala mieleka

Lema usiongee bla bla game ndio kwanza linaanza,kesho ni njema sana kwa watu unaowadhani wabaya kwako

Lamba asali kimya kimya
Idadi ya wapumbavu inasonga mbele, hongera nawe umo

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Unatukana Vikoba ambavyo Watu wanakusanya Pesa Kwa hiyari Yao, Kwa Pesa Yao ya jasho halali, kisa tuu wanakusanya miambili miambili.
Lema amekwama, na wapo Watu wengi WA mfano wake.
Watu wote wanafiki wanaoshabikia kazi inayoua vijana wetu kwa idadi kubwa wamelaanika maana hawathamani maisha ya vijana wengi wanaoangamia na kupata ulemavu wa kudumu kila siku.

Serikali ithamini maisha ya vijana wetu. Itengeneze mazingira mazuri yatakayoeawezesha watu wafanye kazi halali, zinazowapatia kipato, hata kama ni vipato vidogo, lakini wawe salama.

Tuachane na wanafiki wanaishabikia vijana waendelee kuwa bodaboda, huku kazi yenyewe inawaua na kuwapa ulemavu kwa idafi kubwa, ilihali watoto wao hawawafanyi wawe bodaboda.

Amelaanika mtu yule anayemtumia binadamu mwenzake kufanya matendo ya hatari huku yeye akijinufaisha ama kwa mapato ama kwa umaarufu, wakati mtendakazi akipoteza maisha au kuwa kilema.

Tunafahamu, wapo wengi humu wanaitetea kazi ya bodaboda kwa sababu wamenunua pikipiki na kuwapa vijana wazitumie, huku wao wakiletewa pesa kila siku. Kama kweli ni kazi yenye baraka na salama, kwa nini hawanunui na kuwapa watoto wao wakatafutie pesa ili wawaletee?

Pikipiki ni usafiri wa mtu mmoja mmoja, tena kwa mazingira fulani tu, haustahili kuwa usafiri wa umma. Uendeshaji wa pikipiki una risk kubwa ya kiusalama kwa sababu tatizo dogo la barabarani, mwendesha pikipiki anakuwa victim wa kifo au ulemavu.

Uhalali wa kazi hautokani na ukweli tu kuwa kwa sababu unapata kipato. Leo boda boda mpaka wanatengewa wodi zao mahospitalini, halafu mtu mjinga na mnafiki anatetea kuwa ni ajira inayostahili kuendelezwa! Tusiwe wanafiki, tujali maisha ya vijana hawa kama tunavyoyajali maisha yetu na ya watoto wetu. Vijana hawa wapo tayari kuhatarisha hata maisha yao kwa sababu jamii imeshindwa kuwapa hifadhi. Hili siyo tatizo la waendesha bodaboda bali ni tatizo la jamii yetu nzima.
 
Back
Top Bottom