Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Lema ameendeleza dharau Kwa watu maskini akisema vikoba ni umaskini.

Ikumbukwe Vicoba ni ubunifu wa wamama katika kujikwamua ila kama kawaida kwa kuwa amefanywa kipofu Ili aumbuke amewatukana tena wamama.

Watu maskini eleweni kwamba huyo sio mtu wenu na kama hamuamini endeleeni kimshabikia.


Kwanza vinasanabisha wake zetu wagongwegongwe ovyo Ili tu kupata Hela ya rejesho
 
Sasa vicoba kwani ni fahari? Mtakuja kusifia hata kamari kisatu imepondwa na msiemtaka
Hivyo vicoba nikwaajili ya maskini. Hakuna waziri,RC,DC,DED, anaecheza vicoba.

Vicoba havijawahi kumkwamua mtu kutoka kwenye lindi la umaskini
 
Ajira ya bodaboda ni laana ya nchi yetu. Laana hutokea pale mtu au nchi in this case inapotawaliwa na viongozi wavivu, wezi na wazembe.

😂😂😂
Ndio maana nikakuambia hujui maana ya Laana.
Ajali inatokana na sababu nyingi, Ila kubwa ni Uzembe, ukosefu WA Elimu, kuvunja sheria za Barabara, kutojali nafasi za wengine uwapo Barabarani n.k.
Na sio kazi ya ubodaboda
 
Sasa vicoba kwani ni fahari? Mtakuja kusifia hata kamari kisatu imepondwa na msiemtaka
Hivyo vicoba nikwaajili ya maskini. Hakuna waziri,RC,DC,DED, anaecheza vicoba.

Vicoba havijawahi kumkwamua mtu kutoka kwenye lindi la umaskini
Eti mwisho wa mwaka wanapokea hela nyingi wanapo vunja kikoba,ndo wanasijikia ufahari 😁
 
Mimi naweza kuiita ni kazi ya laana kwa context moja tu, siyo kazi salama. Inaua vijana wetu wengi wakiwa kwenye umri mdogo sana, na kuwaacha wengi wakiwa na ulemavu.

Kuna wakati, kwenye kampuni yetu, tuliamua kuwapa mikopo isiyo na riba wafanyakazi wetu. Vijana wengi kwa kutumia pesa hiyo wakaamua kununua pikipiki. Ndani ya wiki 3 tukawapoteza vijana 4 na mzee 1 mwenda kwa miguu kwa ajali za pikipiki (aliyegongwa na kijana wetu). Iliumiza sana. Tukasimamisha mikopo. Mwanzoni tukafikiria tutoe conditions za mkopo, kuwa hakuna atakayeruhusiwa kutumia hela ya mkopo kununulia pikipiki. Lakini tukaona kuna shida, maana mkopaji akinunua pikipiki, bado inakuwa ni vigumu kutambua kama ametumia hela ya mkopo au hela yake ya mshahara au mapato mengine. Tukaamua tuzidishe mafunzo, yaliyohusisha wataalam mbalimbali. Tukafanikiwa, mpaka leo hatujashuhudia kifo chochote cha ajali ya pikipiki kwa wafanyakazi wetu.

Kama ni Mtazamo na Maoni yako basi uko sahihi.
Ila katika uhalisia Sio Laana.

Ni Sawa na kina Mpwayungu wanaosema kazi ya ualimu ni laana, ni mitazamo Yao binafsi Ila kiuhalisia sio.
 
Kwako kipi Bora?
Kufanya uzalishaji ulipwe 140,000 Kwa mwezi
Au kufanya bodaboda upate Kwa Siku 10,000/=

Sijasema hao wazalishaji WA viwandani wanafanya vibaya, Nop! Kila mmoja afanye anachoona kipo Mbele yake na anachoweza kufanya.

Kufanya kazi sio tatizo, hakuna serikali duniani inayotaka Vijana wake wateseke, ni kwamba Serikali na taifa lenu na mataifa ya Afrika tayari yameshazidiwa Step na washidani wao wazungu.

Wewe hata ungepewa Urais Kwa miaka 100 huna ambalo utafanya,
Ni vigumu kuelewa mambo haya
Vyote ni vibaya. Na hapa ndipo tunaposhindwa kuelewena. Wewe hutaki kukubali kuwa tumefikia hapa i.e. ujira wa 140,000 kwa mwezi au 10,000 kwa siku kwa sababu tulikosea huko nyuma. Mimi najaribu kuonyesha kuwa siku za nyuma tumekosea sana na ndiyo maana tumejikuta hapa tulipo. Jaribu kuangalia basi in a pig picture. Bodaboda au machinga atafanya hiyo kazi mpaka lini? Unajua kila uchao vijana wengi tu wanazidi kujiingiza kwenye hii biashara? Ni nini mipango ya uzeeni kwa hao waendesha bodaboda na familia zao? Bado narudia: Bodaboda siyo solution ya hapa tulipofikia.
 
Anaandika, Robert Heriel

  • Kazi na kuwa kipato duni hakuifanyi kazi hiyo kuwa ya Laana.
  • Kazi kufanywa na watu wasio na Elimu hakuifanyi kazi hiyo iwe ya Laana.
  • Kazi kufanywa pasipo kufuata utaratibu hakuifanyi kazi hiyo kuwa na Laana.

Kazi ni ibada kwa wale waamini na waaminio. Kazi yoyote halali aifanyo mtu ni ibada. Lakini pia kufanya kazi kisheria ni kutimiza wajibu ndani ya taifa. Kusema kazi Fulani ni Laana kisa mapato ya Kazi hiyo ni duni, ni dharau na ujinga wa msemaji.

Kazi kuwa hatarishi haimaanishi kuwa ni kazi ya Laana. Bodaboda ni kazi kama kazi zingine, Umachinga ni kazi kama kazi zingine, Udalali ni kazi kama kazi zingine, Ukuli na upiga Debe ni kazi kama kazi zingine.

Ni mtu mpumbavu na mjinga asiyeelewa mambo hayo.

Lena anadharau sijui Vikoba kisa watu wanachanga bukubuku au elfu tatu, hizo pesa zinazochangwa sio pesa za wizi, ni pesa halali, hawajamuibia mtu. Ni jasho Lao, dharau na Kiburi sio Kizuri.

Kwa Watu waungwana, wasomi walioelimika, wenye maadili na hofu ya Mungu huwezi kuwasikia wakiongea mambo ya hovyo kama hayo.

Lema kama mtu ajionaye mwenye akili, exposure na aliyewahi kuwa kiongozi kwa nafasi ya Ubunge, pamoja na sisi wasomi na watu wa serikali pamoja na viongozi wa dini tulipaswa kufanya haya yafuatayo;

1. Kuzitambua kazi mpya zilizozuka hivi karibuni kutokana na mapinduzi ya Teknolojia na ujio wa Utandawazi. Kazi kama za bodaboda, umachinga, kazi za mitandaoni, kazi za udalali n.k, ni muhimu kuzitambua.

2. Kuziwekea Sera, Sheria na Kanuni ili kuwapa Haki na Fursa watakaojiingiza humo.

3. Kutunga na kuingiza mitaala ya kozi fupi na ndefu zitakazofundisha kazi hizo kwa gharama nafuu, ili kuzipa thamani kazi hizo. Kupitia Elimu na Sheria zitakazotungwa kutakuwa na maadili ya hizo kazi.

Utoaji wa Elimu utasaidia kazi hizo kutokufanywa kiholela. Kutawafanya wafanyaji wa kazi hiyo kuwa nadhifu kimavazi, pia utumiaji wa lugha fasaha na zenye nidhamu utazingatiwa kwani ni sehemu ya kazi.

4. Kuandaa mfumo wa Bima ya Afya kwa gharama nafuu inayolingana na kipato cha kazi hizo. Bahati nzuri siku hizi ipo ile Bima ya CHIF ya elfu 40.

5. Kuandaa mifumo ya ulipaji wa Kodi au Ushuru kulingana na eneo la kazi. Hii ni kumfanya kila mtu awajibike kuijenga nchi.
Kwa mfano bodaboda akilipa elfu hamsini kwa mwaka kama Kodi haiwezi kumshinda. Hata hivyo pesa hiyo lazima iingizwe moja kwa moja kwenye Leseni ili kuepusha usumbufu.

Leseni na Kodi isizidi 100,000/= kwa upande wa madereva bodaboda. Kama dereva bodaboda ni wa kuajiriwa basi watashare yeye na bosi wake gharama ya Kodi, huku Leseni ikibaki kuwa wajibu wa dereva mwenyewe. Mfano kama Kodi ni 50,000 kwa mwaka basi mmiliki wa bodaboda atalipia 25,000/= na dereva bodaboda atalipia 25,000/= Kwa Mwaka. Huku gharama za Leseni ikibaki kuwa ya dereva.

6. Angalau kila mwaka itolewe semina ya madereva bodaboda, na mafunzo kwa Madereva bodaboda kwa ngazi ya Kata.
Kazi Hii waifanye Polisi Kata wakipewa Posho kwa kazi hiyo watakayoifanya.

7. Iundwe Programu ya kuhamasisha watu kupenda kazi zao bila kujali wanapata kiwango gani cha fedha na iundwe sheria ni marufuku kwa mtu kutoa maneno ya kashfa kwa kazi zingine; yaani maneno ya kutusi, kudharau na kujeli kazi zingine, ili kukifanya kizazi kinachokuja kisije lukua na kasumba mbaya kuhusu baadhi ya Kazi. Kudharau kazi za wengine ni chanzo kikuu cha janga la ajira.

8. Kutokana na nchi yetu bado ni Maskini, kazi za umachinga haziepukiki, utaratibu maalumu hasa katika ngazi ya Serikali za Mitaa uundwe ili kuhakikisha unasimamia machinga katika maeneo waliyomo nje ya katikati ya jiji.

Wawekewe muda maalumu wa kuendesha shughuli hizo kwa kupanga pembeni ya barabara sehemu ambazo ni salama (nasisitiza sehemu ambazo ni salama). Kwa mfano kuwaruhusu wafanya shughuli hizo kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 4:00 usiku chini ya masharti yafuatayo;

  • Kuhakikisha eneo hilo ni Safi kabla na baada ya biashara.
  • Kutokupanga biashara kwa wapita njia.
  • Kutoa Ushuru kila siku labda ni buku, au kiwango chochote kulingana na eneo bila kutoa excuse yoyote ya sijui sijauza au nimeuza.
  • Kutokujenga kibanda chochote eneo hilo.
  • Kufanya biashara kwa muda uliopangwa na Serikali.
  • Kuuza bidhaa halali.
  • Kuuza bidhaa zenye thamani itakayowekwa na Serikali kama itakavyoona inafaa, labda tuseme bidhaa zitakazopangwa barabarani ziwe bidhaa ndogondogo mfano nguo, matunda, maji n.k na sio mtu aweke biashara yenye mtaji wa mamilioni ya pesa.
  • Kulipa Faini ya kiwango kitakachowekwa na Serikali au kufukuzwa eneo hilo na kutopewa eneo jingine ikiwa atavunja kwa makusudi taratibu zilizowekwa n.k.

Kitu kikubwa ambacho Lema angekisema ni kuiambia, au kuilaumu serikali kwa kushindwa kuwasaidia hao wenye hizo kazi anazoziita ni za laana. Na sio kuwaponda watu walioamua kujishughulisha kwa shughuli halali.

Au anafikiri kuwa mwanasiasa kwa kupiga mdomo na kubwabwaja kwenye majukwaa ndio kazi ya baraka au kazi bora kuliko kazi nyingine? Kila kazi ni bora itategemea na mtazamo wa anayeifanya.

Wapo Watu ambao hata uwaambie wawe wabunge hawatotaka kuwa wanasiasa. Kudharau kazi ya mtu mwingine au kipato cha mtu mwingine ni dalili ya kutokuwa muadilifu, dalili ya kiburi na ushamba fulani hivi.

Unadharau kazi ambayo kuna watu wanaendeshea familia zao, wanatoa Sadaka kwa Miungu yao, Wanahudumia watu katika maeneo yao. Wewe kwa akili yako ndogo unawakejeli.

Watu wanatafuta Maisha mazuri lakini kupata pesa nyingi haimaanishi ndio maisha mazuri. Maisha mazuri ni kupata kipato halali kwa kazi halali, kwa jasho lako. Tuache kudharau Watu na kazi zao.

Ujumbe huu umemtumia Lema kama mwakilishi wa watu wote wenye dharau na kejeli na Kiburi, sio kwa Lema peke yake.

Nawatakia Sabato njema.

Ni yule Mtibeli,

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
UNGETUNGA KITABU UNAICHOSHA SERVER
 
😂😂😂
Ndio maana nikakuambia hujui maana ya Laana.
Ajali inatokana na sababu nyingi, Ila kubwa ni Uzembe, ukosefu WA Elimu, kuvunja sheria za Barabara, kutojali nafasi za wengine uwapo Barabarani n.k.
Na sio kazi ya ubodaboda
Jaribu kusoma tena kwa ufahamu. Mimi sikuzungumzia suala la ajali hata kidogo. Nimeandika ''AJIRA'' na siyo ''AJALI''
 
Haya ni maandalizi ya Zama mpya na upinzani mpya HATA ikiwezekana na chama kipya tawala kabisa kutokana na aina za siasa wanazofanya wapinzani!

Ukichunguza KWA MAKINI utagundua wanapewa script ya kile wakisemacho kabla ya kukisema,Bado haijaeleweka wanafanya KWA maslahi ya Nani hasa!je ni system,je ni mtu,je ni chama Tawala au ni faida yao wenyewe!

Ni rasmi Sasa upinzani wa miaka mingi ulikuwa na baba yao anaoulea Ndio huyo anaetajwa kuwa aliwashauri nini cha kufanya waje au wasije nchini!matamshi ya lema yanapigia mstari dhana hii!!

Katika Zama hizi za katiba mpya kutajwa tajwa ni RASMI sasa kuwa katiba hii iliyopo inakufa na siasa zake na kuzaliwa mpya!

Wote KWA pamoja tukiri kwamba nchi yetu ni ya thamani kuliko chama CHOCHOTE wala upinzani wowote!

Wote tuseme Mungu ibariki Tanzania nchi yetu tuipendayo sana!
 
Vikoba havina msaada,

Ni hela yako inakatwa sijui, akiba sijui nini, wa kufaidi ni wachache.

Vikoba lazima mgombane mpaka mtishiane kurogana.

Kosa la Lema anasema ila hatoi option B, bila vikoba au bodaboda watu wapateje hela?
 
Mimi pia sioni faida,yaan pesa zako unaweka halafu unakuja kurudishiwa mwisho wa mwaka..then what? Kwamba umeshindwa kuhifadhi wewe mwenyewe? Kama hyo ndo logic
Wajanja wanafanyia hela za maskini kazi maskini anashangaatu
 
Watu Kufa au Kupata ulemavu Kwa sababu ya bodaboda ni Kutokana na ukosefu WA Elimu katika kazi hiyo na kutofuata sheria za udereva na usalama Barabarani, Na sio kuwa kazi hiyo ni Laana.

Ni jukumu la serikali kuandaa Mpango na utaratibu na kuupa nguvu kuhakikisha ili uwe bodaboda na uendeshe MTU lazima upate mafunzo na upewe Leseni,
Kisha iundwe sheria kuwa endapo utakuwa hauna Leseni na hauna cheti cha mafunzo utapewa adhabu ya kifungo cha muda Fulani.
Pia endapo utasababisha ajali na hauna Leseni wala mafunzo itahesabika kama umefanya mauaji ya kukusudia

Ni Sawa na MTU ajenge nyumba alafu Hana gani ya uhandisi majengo, nyumba ikianguka anapaswa kupewa adhabu Kali. Lakini huwezi sema ujenzi wa nyumba au ufundi Washi ni Laana.

Ndio maana Elimu ni muhimu.
Lakini sio Elimu ya kupotosha Watu kuwa kuna kazi ni Laana ilhali sio Laana.
Ndivyo wasomi wengi WA siku hizi mlivyo,
Huwezi kubeba tractor ukaliweka barabarani liwe linasafirisha abiria, kila kukitokea ajali maafa ni makubwa, halafu useme eti dereva wa tractor apewe mafunzo ya namna salama ya kusafirisha abiria. Tractor kwake ni huko mashambani, halijatengenezwa kwaajili ya kusafirisha abiria.

Pikipiki hazijatengenezwa kwaajili ya public transport. Kuna baadhi ya nchi, pikipiki hutumika zaidi mashambani tu ambako hakuna msongamano wa magari. Kule Australia, pikipiki zinatumika zaidi na wachunga kondoo. Pikipiki haijatengenezwa kwaajili ya kutembea kwenye highway, ndiyo maana kama ilivyo baiskeli, ina gurudumu moja mbele moja nyuma ili iweze kupita kwenye tracks (vinjia vyembamba). Kuziweka kama chombo cha usafiri wa umma ni makosa makubwa. Pikipiki kutokyluwa salama, hakusababishwi tu na uendeshaji mbaya wa pikipiki, mwenye gari anaweza kumgonga mwenye pikipiki. Kila wakati barabarani magari yanakwanguana lakini athari inakuwa ni ndogo sana kwa sababu yanakwanguana magari, abiria ndani wakiwa salama. Gari likiikwangua pikipiki, inamkwangua mwendesha pikipiki.
 
Vikoba havina msaada,

Ni hela yako inakatwa sijui, akiba sijui nini, wa kufaidi ni wachache.

Vikoba lazima mgombane mpaka mtishiane kurogana.

Kosa la Lema anasema ila hatoi option B, bila vikoba au bodaboda watu wapateje hela?
Tupatie uzoefu wako Mama mdenyi kuhusu vikoba.
 
Hizi boda boda biashara yake haijafikisha miaka 20, wakifikisha miaka 30 ndipo tutajua athari za hiyo kazi.
Kwa sababu za kisiasa tuendelee ziweka kwenye kundi la ajira
 
Back
Top Bottom