Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Vyote ni vibaya. Na hapa ndipo tunaposhindwa kuelewena. Wewe hutaki kukubali kuwa tumefikia hapa i.e. ujira wa 140,000 kwa mwezi au 10,000 kwa siku kwa sababu tulikosea huko nyuma. Mimi najaribu kuonyesha kuwa siku za nyuma tumekosea sana na ndiyo maana tumejikuta hapa tulipo. Jaribu kuangalia basi in a pig picture. Bodaboda au machinga atafanya hiyo kazi mpaka lini? Unajua kila uchao vijana wengi tu wanazidi kujiingiza kwenye hii biashara? Ni nini mipango ya uzeeni kwa hao waendesha bodaboda na familia zao? Bado narudia: Bodaboda siyo solution ya hapa tulipofikia.
Vizuri, umeongea vizuri Kabisa.
Kwamba kuna sehemu tulikwama, lakini tuwaache Vijana ambao wameamua kujipatia kipato Kwa Njia halali,
Huyo Lema anatakiwa awapongeze hao bodaboda Kwa Akili na ujasiri walionao.
Aseme kama chadema itachukua Dola nini itafanya Kwa wale watakaopenda kufanya kazi ya bodaboda, nini itaboresha ambacho Kwa sasa ni tatizo.
Na sio kuiponda na kuishambulia kazi hiyo na wanaoifanya moja Kwa moja.
Kila kazi ni muhimu,
Hatuwezi fananisha nchi yetu na mataifa mengine, Ila sio kosa kuchukua mazuri kuchukua Kwa wengine.
Hata bodaboda ni Jambo zuri ikiwa litafanywa Kwa utaratibu.
Ninachopinga ni kuibagaza kazi ya bodaboda na kuidharau.
Kudharau Vikoba ambavyo kimsingi vimesaidia baadhi ya wakina Mama.
Matokeo hasi ya Vikoba, ni changamoto ambazo zinaweza kupatiwa ufumbuzi hasa kutoa Elimu ya fedha na namna ya kuzitumia fursa