Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya


Vizuri, umeongea vizuri Kabisa.
Kwamba kuna sehemu tulikwama, lakini tuwaache Vijana ambao wameamua kujipatia kipato Kwa Njia halali,
Huyo Lema anatakiwa awapongeze hao bodaboda Kwa Akili na ujasiri walionao.
Aseme kama chadema itachukua Dola nini itafanya Kwa wale watakaopenda kufanya kazi ya bodaboda, nini itaboresha ambacho Kwa sasa ni tatizo.

Na sio kuiponda na kuishambulia kazi hiyo na wanaoifanya moja Kwa moja.

Kila kazi ni muhimu,
Hatuwezi fananisha nchi yetu na mataifa mengine, Ila sio kosa kuchukua mazuri kuchukua Kwa wengine.
Hata bodaboda ni Jambo zuri ikiwa litafanywa Kwa utaratibu.

Ninachopinga ni kuibagaza kazi ya bodaboda na kuidharau.
Kudharau Vikoba ambavyo kimsingi vimesaidia baadhi ya wakina Mama.

Matokeo hasi ya Vikoba, ni changamoto ambazo zinaweza kupatiwa ufumbuzi hasa kutoa Elimu ya fedha na namna ya kuzitumia fursa
 
Hizi boda boda biashara yake haijafikisha miaka 20, wakifikisha miaka 30 ndipo tutajua athari za hiyo kazi.
Kwa sababu za kisiasa tuendelee ziweka kwenye kundi la ajira

Kila kazi inamatokeo chanya na hasi. Hasa utaratibu usipofuatwa, na pasipokuwa na kiasi.
 
Ni mjinga mmoja tu. Maisha hayana formula moja. Mke wake hawezi kuwa na qualifications za vicoba. Vicoba ni utekelezaji wa sera ya financial inclusivity. Lakini pia yeye ana uwezo wa kushika hela nyingi kwa wakati mmoja tofauti na wanawake wenye maisha ya chini. Mtu amekaa ubunge miaka 15, amepewa pesa na mabeberu akiwa Canada, halafu anaanza kutuona hatuna akili? Kazi zetu ndogo ndogo ni laana?
 
Kwa hiyo wasubiri mpaka serikali itakapowapatia maisha bora ndio waanze kutafuta, kwa sasa wakae tu nyumbani?
Ndio maana nikasema akili ndogo haielewi!
Sikusema wakae wala wasubiri. Soma tena; Waidai serikali ijenge mazingira mazuri.
 
Kwa waislamu huyu Lema yupo sahihi wala msimpinge
 
Unasubir jeshi au serikali ikupe evidence? Btw bado mdogo ukikua utaelewa tu!!
Wewe ujui siasa ilivyo ndio maana siasa waliita ni mchezo mchafu kwasababu wanasiasa hawaaminiki Lema si ndio huyo huyo akisema Lowassa ni fisadi na Ndio miongoni mwa mtu aliyempokea chamani na kumpigia kampeni ya Uraisi kama aliongea haya mimi ni nani niamini maneno yake
 
Kwani ajali za barabarani hasa mabasi ya mikoani huwa haziui? mbona kuna wakati zinafululiza mpaka watu wanashtuka?

Kwa hiyo tuseme na kuendesha mabasi ya mikoani pia ni kazi ya laana?

Bodaboda wana umuhimu wao kwenye jamii yetu, hawa kinachohitajika kwao ni kupewa elimu ya kujikinga na ajali, na wazingatie sheria za usalama barabarani.

Jitahidi kupunguza hisia kwenye maandishi yako, tafakari kwa kina.
 

Aliyesema pikipiki haikuundwa kama chombo cha umma ni Nani?
 
Kama ni Mtazamo na Maoni yako basi uko sahihi.
Ila katika uhalisia Sio Laana.

Ni Sawa na kina Mpwayungu wanaosema kazi ya ualimu ni laana, ni mitazamo Yao binafsi Ila kiuhalisia sio.
Uwalimu, hata siku moja, haiwezi kuwa ni kazi ya laana. Kwa hapa Tanzania, uwalimu inaweza kuwa ni kazi ya kipato kidogo, lakini kamwe siyo kazi ya laana. Tena, naweza kudiriki kusema kuwa kazi ya uwalimu, ni kazi ya baraka. Kumwelimisha mtu, kumtoa ujinga mtu, hakuwezi kuwa kazi ya laana, bali ni baraka, ni kazi takatifu, japo ndani ya uwalimu wapo waliolaanika, ndio wale tunasikia mpaka wanabaka wanafunzi wao.

Yesu Kristo, ni MWALIMU, kuhani, masihi, mfalme na nafsi ya Mungu kamili.
 
Bwanamdogo huyu kwa sasa hachagui la kusema yaani kuishi canada kidogo anajifanya anaweza kufikiri tofauti na waliobaki Arusha!

Kazi ya Bodaboda kasema ni laana kubwa, karudia tena kuwa vicoba vya akina mama ni laana kubwa pia, aangaliwe vizuri anaweza kutaja hadi kazi ya walimu maana hajui kuchagua maneno huyu jamaa.
 

Hao wanadharau kazi za wenzao.

Elimu itolewe, pia kiwango na idadi ya pikipiki idhibitiwe ili kudhibiti jams kubwa Barabarani. Na hili wanaweza kulifanya Kwa kuandaa utaratibu wa Akili ili kuyafanya mambo yaende pasipo kuleta madhara kwao.
 
Kama Lema aliita bodaboda ni kazi ya laana kwa sababu ina kipato kidogo, hapo alikosea. Kipato kidogo siyo kigezo cha kazi kuwa ya laana.

Lakini jambo moja lililodhahiri bodaboda ni tatizo kubwa linalohitaji ufumbuzi wa haraka ili kuwapa matumaini vijana hawa wanaoangamia kila siku.
 
Inabidi usaidiwe na serikali sio lema.

Acha aongee aaliyopitia.

Unataka usaidiwe na lema kwani ndio serikali.


Una kichaa wewe

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Bodaboda hawazalishi chochote kwenye uchumi

tunahitaji nguvu ya moja kwa moja kwenye kujenga nchi hasa kutoka kwa vijana.. Kijana wa boda boda anachotafuta ni hela ya kula yeye na kwa risk kubwa sana...

tungeweza kumpa ajira jeshini na kumpa mafunzo akawa hata operator wa tractor kwenye miradi mikubwa ya mashamba makubwa ya serikali chini ya JWTZ..
Kijana huyu akiwa jeshini tunampa mafunzo yatakayomfanya awe skilled labor force, lakini wakati huo huo anakuwa modern trained soldier ambaye ikitokea vita anakuja kama askari wa akiba.. Akiwa jeshini anazalisha, tunamlipa mshahara mzuri, tunampa bima ya afya na familia yake nk, anapewa mikopo nafuu kudevelop familia yake.

Hawa vijana wote tukiwatumia kwenye mlengo huo, in 5yrs taifa litakuwa na mashamba makubwa ya chakula na biashara, kwa mwaka tunaweza kuwa na kipato kikubwa sana kama Taifa...
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ndio maana nikakuambia hata anayesema bodaboda ni Laana huo NI mtazamo na Maoni yake lakini kiuhalisia sio Laana.

Kazi ya Bodaboda ni kazi muhimu kwani inawatumikia wananchi hasa wananchi WA kawaida na Maskini kuwasafirisha Kutoka pointi moja kwenye nyingine. Inaharakisha Watu kwenda kwenye shughuli zao ikiwemo hao waalimu.
Ni gharama nafuu na unaweza kupelekwa sehemu ambayo Kwa gari usingepelekwa Kwa gharama hiyo.

Kila kazi ni muhimu, na baraka katika jamii Fulani.
Huweziita ualimu ni laana kisa wapo waalimu wanaochapa Watoto mpaka wanakufa au Kupata ulemavu.
Vivyohivyo huwezi ita ubodaboda ni laana kisa wanapata ajali au kusababisha ulemavu Kwa Watu.
Ni ishu ya Elimu kutolewa, udhibiti wa kisheria n.k
 
Vikoba havina msaada,

Ni hela yako inakatwa sijui, akiba sijui nini, wa kufaidi ni wachache.

Vikoba lazima mgombane mpaka mtishiane kurogana.

Kosa la Lema anasema ila hatoi option B, bila vikoba au bodaboda watu wapateje hela?
Wewe ndie umemaliza vizuri, no option B.
 
Vicoba ni dalili ya umasikini kwenye jamii, baadala yake watu wafundishwe namna yakuwa productive popote walipo, familia zifundishwe uwekezaji wa viwanda vidogovidogo hata majumbani ziwe zinafanya production ya quality products kwa ajili ya viwanda vinavyofanya mass production...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…