Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Kwenye hili Lema amekosea, kazi yoyote halali si laana. Tutafikia hatua kila kazi ya chini ya kipato kidogo tutasema ni laana. Watu wa hali ya chini wanaofanya shughuli zao kutokana na uwezo wao kielimu, kiuchumi wapo duniani kote.

Kisingizio cha bodaboda kufa, kuumia, kuwa vilema ni mazingira ya kazi yenyewe. Ukienda nchi kama Rwanda, kuna utaratibu mzuri sana wa bodaboda na usalama wao na hakuna ajali za kizembe kama huku kwetu.

Lema ni mbishi lakini maelezo yake ya awali yamejaa ukakasi sana. Hata alivyozungumzia issue za vikoba ameongea vibaya na ufafanuzi mwepesi sana.

Maisha yanabadilika sana, yumkini haoni mkewe kuja kujiunga na vikoba wala mwanae au mjukuu wake kufanya kazi hiyo ya laana lakini kulikuwa na namna bora ya ku address hili bila swala lenyewe kuliita laana.

Waambieni ukweli viongozi wenu msipende kuwatetea ovyo! Mnawapoteza!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hawataki kuamani ila ndio ukweli huyu Lema kaonyesha zarau kubwa mnoo kwa watanzania na waafrika kwa ujumla .Huwa najiuliza hivi huyu jamaa angekuwa amesoma sijui angekuwa na majigambo ya aina gani aisee
 
Wa Hangaya wanalalamikiwa kukwepa kodi na kusumbuana na TRA Kariakoo
 
Wakuu,

Jana Lema alikiona cha mtema kuni baada ya kuwashambulia wazee wa kubeti.

Wana walimvamia kwenye tweet yake hadi akaifuta. Na aliifuta ndani ya dk 20 tu baada ya kuona vita haiwezi.

Betting iachwe ilivyo. Isiguswe. Na hatuachi
 
Huo ni uthibitisho tosha kuwa betting is insanity, ni mateja.

Vv
 
Umasikini na Ujinga wa WaTz ndio mtaji wa ccm. Wao wamshambulie Lema, ila umasikini na ujinga utawashambulia maisha yao yote.
 
mbona unakatisha hoja yake?

amesema ilimlazimu kuvaa baibui akienda kukagua machimbo yake ya madini kipindi cha magu ili asitambulike kutokana na hofu ya usalama wake.
Kwa hiyo hao waliokuwa wanamtafuta hawaijui migodi yake wakaifunga?
 
Sasa ndio ujikite kwenye hiyo sababu na sio kujikita kwenye uvaaji tu, yaani ni kitu gani kilipelekea hadi huyo ndugu akaamua kuvaa baibui??.
Wengine wanasema sababu ni mambo ya lgbt
 
Kweli ujinga mzigo. Hii nayo ni hoja ya kuleta hapa jukwaani?
1990 Mandela alipokuja hapa Tanzania alizungumzia alizungumzia alivyo toroka SA na kuja mpaka Tanzania akielekea Algeria na jinsi alivyo wahadaa Polisi wa SA miaka ya awali ya 1960s kabla ya kurudi tena na kufungwa.
Wanasiasa mashujaa wamepitia vitimbi vingi kujiokoa na wanastahili pongezi sio upuuzi wenu wa kitoto
 

Alichosema ni kweli hata kama wamemshambulia
 
Betting ni worldwide sio Tanzania tu, halafu wanabet kwa pesa zao unasemaje kuwa hawafanyi kazi?Kama hawafanyi kazi hizo pesa wanazobet wanazitoa wapi?
Ajira hakuna,mikopo halmashauri wanatoa kwa kujuana utalalamika watu wasibet?
Waende shamba wakalime kuna shamba la 500 au 1000?
 
Betting is a worldwide issue, hata huko Canada alipokuwa akilelewa watu wanafanya Betting, kwenye makasino nk. Tatizo ni pale watu wanabweteka hawataki kufanya kazi, wanashinda vijiweni tu.


Kingine, Lema anajisahau kuwa hata huo ubunge wa kila mara anaogombea anafanya kamari tu, anakopa ili kufanya campaigns, akiupata ubunge analipa wadeni wake, akikosa ubunge inabidi auze some of his assets ili alive mkopo.

Asidanganye watu hapa, the little exposure he has kusimfanye alewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…