Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Kwa nini hawakukimbilia hata Malawi jirani? Au Zambia? Au Burundi?
 
Si arudi huko Canada huyu kiazi. Mbona analeta ujinga ujinga mwingi huyu!!

Haitokuja kutokea watu wote wakawa sawa duniani. Hata huko Canada kuna shule binasi.

Lema aache ujinga, kwenda Canada kidogo tu basi kila kitu anataka kifanane na Canada, shenzi kabisa.
 
Kuna Rais alisema Viongozi watibiwe hospital za uma

Hakuna kwenda india.. tuliona muhimbili inaboreshwa .

Angekuwa hai asingeshindwa kusema watoto wa viongozi wasome shule za uma kwa lazima
 
Lema hakupitia hekaheka zozote 🤣🤣🤣, alikwenda kutafuta maisha Canada. Mtu pekee aliyekimbia nchi ni Lissu.

Lissu dhambi yake anaijui vizuri, siungi mkono jaribio la kumuua lakini ukweli lazima usemwe, jamaa alijaribu kufanya usaliti kwa maslahi yake ya kisiasa. Hii ilimuudhi na kumuumiza sana mzalendo JPM.
 
Kuna Rais alisema Viongozi watibiwe hospital za uma

Hakuna kwenda india.. tuliona muhimbili inaboreshwa...
Huyu Lema ashauriwe upepo wa siasa za sasahivi ni tofauti na alivyokua hayupo, watu wanafanya siasa za kistaarabu, sio siasa za chuki, mbona mambo yake mengi bado ni yakuudhi? Kuchochochea chuki tu?

Wanaosoma shule za kata sio watu? Yeye hakusoma shule za kata?
 
Shule za serikali hasa za kata ni janga la kitaifa. Lema yupo sahihi.

Yanayo endelea huko ni vurugu tupu.

Waalimu hawafundishi katikati ya juma (week) vipindi vyote bali ikifika ijumaa wanaagiza watoto waende jumamosi na pesa ya kulipia mtihani. Hii ni pesa ya lazima tena watoto wanapewa vitisho.

Kila jumamosi mitihani tena alfajiri na pesa wanayotoza hakuna risiti na mitihani yenyewe wakati mwingine mzazi haoneshwi matokeo au mitihani ya toka taasisi gani au inaulizwa vitu gani. Shule hizo hulazimisha watoto wafike shule saa 12kasoro asubuhi na wanatoka saa 11 na kitu jioni, nadhani lengo wasiende kusoma tuition sehemu zingine , bahati mbaya muda wote huo wanasoma vipindi vichache sana havizidi vitatu au masomo mawili tu kwa siku nzima.

Some kind of extortion!

Haya yanafanyika hadi Dar es Salaam, je huko mikoani?

Mh. Samia hii job security uliyo wahakikishia watumishi wa umma kwamba tumbua tumbua inasababisha watu washindwe kufanya mipango ya muda mrefu sasa walio chini yako wanaitumia vibaya, watumishi wadogo tu wanaweza kupuuzia maagizo au amri zako.

Mifano:
Huko kanda ya ziwa shule fulani ilikuwa inalazimisha kila mwanafunzi aende na dawati na meza vyote vya chuma, shule ipo kijijini sana kwenye kaya maskini.

Dar es salaam shule flani watoto waliambiwa wasiende shule hadi wanunue viatu vyenye kamba hata kama wanavyo vya kufunga kwa mkanda au kutumbukiza.

Wakati hayo ya madawati na viatu yanafanywa mashuleni viongozi wajuu waliagiza mtoto aende shule hata kama hana sare za shule. Hawa wote walimdharau Mh. Raisi na mawaziri husika.

Sijataja shule makusudi sababu sina lengo la kuwaharibia kazi wakuu wa shule husika ktk mifano. Shule zipo nyingi na matukio mengi siwezi kuweka matukio yote kwenye mifano yangu.

Nashauri wazazi msipeleke watoto wenu shule za kata mambo ya ofu ya kukosa mikopo wakifika elimu ya juu ufumbuzi utapatikana huko huko maana huku katani watakosa sifa za kujiunga elimu ya juu kwa kufanya vibaya ktk mitihani ya taifa.

Waziri wa elimu sijui na/au wa TAMISEMI fanyeni uchunguzi.
 
Sikusoma shule za kata, ila nilisoma shule za serikali.
 
Shule ya kata ndio nini?

Lugha ya wapi hiyo?

Hatutaki uharakati tunahitaji sera.
 
Mbona sisi watu wa chini tunaona umuhimu wa usafiri wa bodaboda?

Mbona zimesaidia ajira kwa vijana wengi waliokuwa wanahangaika vijiweni.

Acha kuropoka
👇


 
Vitu vitatu vinavyowamaliza vijana wa Kitanzania kwasasa: bodaboda, kamari, pombe kali za bei poa. Vyote hivi vitatu vina baraka ya chama cha wala.

Kijana wa bodaboda anaungaunga, akipata anaenda kucheza kamari ili apate nyingi aachane na bodaboda. Akifika huko analiwa zote, anapatwa na usongo mkubwa wa mawazo anapitia kwenye kibanda kinachouza pombe kali, anachukua kichupa cha buku 2 na kukiputa chote.

Anapata stimu na kuondoka na bodaboda yake! Hafiki salama nyumbani, aliinywa ile pombe kwa spidi kubwa na ikapanda kwa haraka akiwa barabarani tayari, akapata ajali na kukimbizwa hospitalini. Kufika huko, aliumia vibaya miguu au mikono. Upasuaji laki 5, lakini hana kato ka ya maskini, daktari ili kuokoa maisha ya kijana, anakatwa kiungo chake na kuingia rasmi kwenye ulimwengu wa walemavu.

Kwa baraka na usaidizi wa chama cha wala, walioleta bodaboda ndio haohao walioleta kamari. Huu ni uhujumu uchumi, lakini chama haki yaoni haya!
 
Namsikiliza Mbunge wa zamani Nndg Lema Jembe FM, anahojiwa alipokeaje suala la yeye kufutiwa kesi zake.

Lema anadai moja ya vitu anavyompongeza Mama ni pamoja na yeye kufutiwa mashtaka pia mikutano ya kisiasa.

Amesema kitu pekee CCM walichoshindwa kufanya ni kutengeneza ajira za maana zaidi kwa Watanzania kujiajiri kwenye kazi duni kama bodaboda na kusajili laini.

"Nikisikia mwanangu ni bodaboda au anasajili laini inabidi atafute sehemu ya kukaa, kwangu simtaki tena," alisema Lema.

Mwamba kaamua sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…