Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Hajui political climate ikoje...
Watu washachoshwa na siasa za harakati...na kushambuliana ..

Very soon watamchoka

While I may agree with your line of argument, I also think it is psychologically and emotionally prudent for him to vent.

Lema has not had the kind of attention he has now, and the public was not privy to what he went through behind the scenes, that is why a good number of people criticised his move of seeking political asylum in Canada.

Again, this is his time to set the records straight for the public to understand exactly what happened from his point. In the process he gets a space to vent and get over the horrible trauma from the bad experience he went through.

In my view, we should allow him to heal and this is part of healing.
 
Lema ni jambazi hilo na linatumikia wazungu km lissu dawa yao inajulikana
 
Anaandika, Robert Heriel
  • Kazi na kuwa kipato duni hakuifanyi kazi hiyo kuwa ya Laana.
  • Kazi kufanywa na watu wasio na Elimu hakuifanyi kazi hiyo iwe ya Laana.
  • Kazi kufanywa pasipo kufuata utaratibu hakuifanyi kazi hiyo kuwa na Laana.
Kazi ni ibada kwa wale waamini na waaminio. Kazi yoyote halali aifanyo mtu ni ibada. Lakini pia kufanya kazi kisheria ni kutimiza wajibu ndani ya taifa. Kusema kazi Fulani ni Laana kisa mapato ya Kazi hiyo ni duni, ni dharau na ujinga wa msemaji.

Kazi kuwa hatarishi haimaanishi kuwa ni kazi ya Laana. Bodaboda ni kazi kama kazi zingine, Umachinga ni kazi kama kazi zingine, Udalali ni kazi kama kazi zingine, Ukuli na upiga Debe ni kazi kama kazi zingine.

Ni mtu mpumbavu na mjinga asiyeelewa mambo hayo.

Lena anadharau sijui Vikoba kisa watu wanachanga bukubuku au elfu tatu, hizo pesa zinazochangwa sio pesa za wizi, ni pesa halali, hawajamuibia mtu. Ni jasho Lao, dharau na Kiburi sio Kizuri.

Kwa Watu waungwana, wasomi walioelimika, wenye maadili na hofu ya Mungu huwezi kuwasikia wakiongea mambo ya hovyo kama hayo.

Lema kama mtu ajionaye mwenye akili, exposure na aliyewahi kuwa kiongozi kwa nafasi ya Ubunge, pamoja na sisi wasomi na watu wa serikali pamoja na viongozi wa dini tulipaswa kufanya haya yafuatayo;

1. Kuzitambua kazi mpya zilizozuka hivi karibuni kutokana na mapinduzi ya Teknolojia na ujio wa Utandawazi. Kazi kama za bodaboda, umachinga, kazi za mitandaoni, kazi za udalali n.k, ni muhimu kuzitambua.

2. Kuziwekea Sera, Sheria na Kanuni ili kuwapa Haki na Fursa watakaojiingiza humo.

3. Kutunga na kuingiza mitaala ya kozi fupi na ndefu zitakazofundisha kazi hizo kwa gharama nafuu, ili kuzipa thamani kazi hizo. Kupitia Elimu na Sheria zitakazotungwa kutakuwa na maadili ya hizo kazi.

Utoaji wa Elimu utasaidia kazi hizo kutokufanywa kiholela. Kutawafanya wafanyaji wa kazi hiyo kuwa nadhifu kimavazi, pia utumiaji wa lugha fasaha na zenye nidhamu utazingatiwa kwani ni sehemu ya kazi.

4. Kuandaa mfumo wa Bima ya Afya kwa gharama nafuu inayolingana na kipato cha kazi hizo. Bahati nzuri siku hizi ipo ile Bima ya CHIF ya elfu 40.

5. Kuandaa mifumo ya ulipaji wa Kodi au Ushuru kulingana na eneo la kazi. Hii ni kumfanya kila mtu awajibike kuijenga nchi.
Kwa mfano bodaboda akilipa elfu hamsini kwa mwaka kama Kodi haiwezi kumshinda. Hata hivyo pesa hiyo lazima iingizwe moja kwa moja kwenye Leseni ili kuepusha usumbufu.

Leseni na Kodi isizidi 100,000/= kwa upande wa madereva bodaboda. Kama dereva bodaboda ni wa kuajiriwa basi watashare yeye na bosi wake gharama ya Kodi, huku Leseni ikibaki kuwa wajibu wa dereva mwenyewe. Mfano kama Kodi ni 50,000 kwa mwaka basi mmiliki wa bodaboda atalipia 25,000/= na dereva bodaboda atalipia 25,000/= Kwa Mwaka. Huku gharama za Leseni ikibaki kuwa ya dereva.

6. Angalau kila mwaka itolewe semina ya madereva bodaboda, na mafunzo kwa Madereva bodaboda kwa ngazi ya Kata.
Kazi Hii waifanye Polisi Kata wakipewa Posho kwa kazi hiyo watakayoifanya.

7. Iundwe Programu ya kuhamasisha watu kupenda kazi zao bila kujali wanapata kiwango gani cha fedha na iundwe sheria ni marufuku kwa mtu kutoa maneno ya kashfa kwa kazi zingine; yaani maneno ya kutusi, kudharau na kujeli kazi zingine, ili kukifanya kizazi kinachokuja kisije lukua na kasumba mbaya kuhusu baadhi ya Kazi. Kudharau kazi za wengine ni chanzo kikuu cha janga la ajira.

8. Kutokana na nchi yetu bado ni Maskini, kazi za umachinga haziepukiki, utaratibu maalumu hasa katika ngazi ya Serikali za Mitaa uundwe ili kuhakikisha unasimamia machinga katika maeneo waliyomo nje ya katikati ya jiji.

Wawekewe muda maalumu wa kuendesha shughuli hizo kwa kupanga pembeni ya barabara sehemu ambazo ni salama (nasisitiza sehemu ambazo ni salama). Kwa mfano kuwaruhusu wafanya shughuli hizo kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 4:00 usiku chini ya masharti yafuatayo;
  • Kuhakikisha eneo hilo ni Safi kabla na baada ya biashara.
  • Kutokupanga biashara kwa wapita njia.
  • Kutoa Ushuru kila siku labda ni buku, au kiwango chochote kulingana na eneo bila kutoa excuse yoyote ya sijui sijauza au nimeuza.
  • Kutokujenga kibanda chochote eneo hilo.
  • Kufanya biashara kwa muda uliopangwa na Serikali.
  • Kuuza bidhaa halali.
  • Kuuza bidhaa zenye thamani itakayowekwa na Serikali kama itakavyoona inafaa, labda tuseme bidhaa zitakazopangwa barabarani ziwe bidhaa ndogondogo mfano nguo, matunda, maji n.k na sio mtu aweke biashara yenye mtaji wa mamilioni ya pesa.
  • Kulipa Faini ya kiwango kitakachowekwa na Serikali au kufukuzwa eneo hilo na kutopewa eneo jingine ikiwa atavunja kwa makusudi taratibu zilizowekwa n.k.
Kitu kikubwa ambacho Lema angekisema ni kuiambia, au kuilaumu serikali kwa kushindwa kuwasaidia hao wenye hizo kazi anazoziita ni za laana. Na sio kuwaponda watu walioamua kujishughulisha kwa shughuli halali.

Au anafikiri kuwa mwanasiasa kwa kupiga mdomo na kubwabwaja kwenye majukwaa ndio kazi ya baraka au kazi bora kuliko kazi nyingine? Kila kazi ni bora itategemea na mtazamo wa anayeifanya.

Wapo Watu ambao hata uwaambie wawe wabunge hawatotaka kuwa wanasiasa. Kudharau kazi ya mtu mwingine au kipato cha mtu mwingine ni dalili ya kutokuwa muadilifu, dalili ya kiburi na ushamba fulani hivi.

Unadharau kazi ambayo kuna watu wanaendeshea familia zao, wanatoa Sadaka kwa Miungu yao, Wanahudumia watu katika maeneo yao. Wewe kwa akili yako ndogo unawakejeli.

Watu wanatafuta Maisha mazuri lakini kupata pesa nyingi haimaanishi ndio maisha mazuri. Maisha mazuri ni kupata kipato halali kwa kazi halali, kwa jasho lako. Tuache kudharau Watu na kazi zao.

Ujumbe huu umemtumia Lema kama mwakilishi wa watu wote wenye dharau na kejeli na Kiburi, sio kwa Lema peke yake.

Nawatakia Sabato njema.

Ni yule Mtibeli,

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Hata nami naona kauli ya Lema haikuwa sahihi, alikosea, na inawezekana wenge alilotoka nalo Canada ndilo likamfanya atamke vile.

Bodaboda ni ajira kama ni halali, na inayompatia mfanyaji kipato halali, tusikariri kila ajira lazima mfanyaji akae ofisini.

Huwezi kusema bodaboda ni kazi ya laana ikiwa tuna watu wenye maisha duni, wasioweza kujikimu mahitaji yao kila siku, kunywa chai bila sukari, au uji unawekwa chumvi wengine hata pesa ya kununua kidonge cha Aspirin hawana.

Kwa familia hizi akitokea kijana wao akaendesha bodaboda, kwao ni sawa na ukombozi, hizo elfu moja.. moja wanazokusanya kwa siku zinatosha kuwainua hali zao kiuchumi nyumbani, halafu hawa uwaambie bodaboda ni laana, watakulaani wewe, na Mungu atasikia sala zao kwasababu wanajitafutia kipato halali, hawaibi au kukamba mtu yeyote.
 
Lema ametumia platform alipewa na ccm kuropoka uongo mwingi mwingi sana,sijali huo uongo wake kwasababu haubadilishi ukweli wowote

Ila ninachotaka kusema lema anaongea uongo wa kumiliki mashimo kumbe ni uongo hana shimo ila alipokea pesa ya waarabu flan ili yeye awe front

Na kwenye mashimo ameweka majina ya ndugu yake ili kukwepa kodi kwasababu anadaiwa madeni mengi

Lema aliyekaribia kufilisika kukaribia Hadi kuuza nyumba ya kuishi kutokana na mamikopo yake aliyokopa kichwa kichwa yakala mieleka

Lema usiongee bla bla game ndio kwanza linaanza,kesho ni njema sana kwa watu unaowadhani wabaya kwako

Lamba asali kimya kimya
 
Hata nami naona kauli ya Lema haikuwa sahihi, alikosea, na inawezekana wenge alilotoka nalo Canada ndilo likamfanya atamke vile.

Bodaboda ni ajira kama ni halali, na inayompatia mfanyaji kipato halali, tusikariri kila ajira lazima mfanyaji akae ofisini.

Wengi tunakuwa na conservative mind, Yaani hatutaki Kubadilika kulingana na nyakati, tunataka kazi zilezile zilizofanywa na Wazee wetu nasi tuzifanye au ndio tunaziona ndio kazi
 
Kitendo cha mtu kudharau kazi ya mtu mwingine na ni kazi halali, mtu huyu ni mpumbavu asie jitambua.

Kwa mtu kama huyu bwana lema hakupaswa kutoa matamsh kama hayo kwa watu,

Unatukana Vikoba ambavyo Watu wanakusanya Pesa Kwa hiyari Yao, Kwa Pesa Yao ya jasho halali, kisa tuu wanakusanya miambili miambili.

Lema amekwama, na wapo Watu wengi wa mfano wake.
 
Kwenye psychology kuna kitu kinaitwa "allow the victim to vomit" Hivi haya mambo kina Lema wangeyasemea wapi Kama sio kwenye majukwaani ya mikutano ya kisiasa na kwenye media? Je awamu ya tano ingewezekana? Clouds iliyovamiwa na Bashite na Nape kufukuzwa uwaziri ingeweza kufanya mahojiano live coverage na Lema? Hivi tunakosa kabsa akili ya kuelewa kuwa Lema anatema nyongo ikizingatiwa alishakaa gereza la Kisongo Arusha zaidi ya miezi minne kwa kosa la kuota ndoto kuwa Magufuli akiendeleza unyanyasaji Mungu atamchukua. Hatujui Sugu alisha kaa gerezani? Badae alifatwa na Dr Kitila Mkumbo akishawishiwa kuunga Juhudi akagoma badae kina Pole pole wakampelekea plain cheque imesainiwa tu yeye aandike amount tu akagoma hotel yake ikapigwa x kwamba ibomolewe hapo bado Mbowe akikusimulia kuanzia bill canas mpaka kule Machame kwenye mashamba yake utashangaa. Mambo waliyofanyiwa upinzani awamu ya tano hawatakuja kuyasahau kamwe ni kama vile mwanaume aliyegundua na kushuhudia mke wake kamsaliti sasa anajaribu kumsamehe na kusahau HAIWEZEKANI KAMWE.
Lema ana impact gani au nisababu zipi auliwe
 
Back
Top Bottom