Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Ila kazi kama Ualimu ni laana
Kufanya kazi yoyote hata kuuza karanga hata kama unapata Mia moja Kwa siku sio Laana.
Acha kiburi na dharau.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila kazi kama Ualimu ni laana
Bodaboda Sio kazi ni kuangaika,LEMA AACHE UJINGA NA DHARAU; KUFANYA KAZI ZENYE KIPATO DUNI SIO LAANA.
Anaandika, Robert Heriel
Kazi na kuwa kipato duni hakuifanyi kazi hiyo kuwa ya Laana.
Kazi kufanywa na watu wasio na Elimu hakuifanyi kazi hiyo iwe ya Laana.
Kazi kufanywa pasipo kufuata utaratibu hakuifanyi kazi hiyo kuwa na Laana.
Kazi ni ibada Kwa wale waamini na waaminio. Kazi yoyote halali aifanyo mtu ni ibada. Lakini pia kufanya kazi kisheria ni kutimiza wajibu ndani ya taifa.
Kusema kazi Fulani ni Laana kisa mapato ya Kazi hiyo ni duni, ni dharau na ujinga wa msemaji.
Kazi kuwa hatarishi haimaanishi kuwa ni kazi ya Laana.
Bodaboda ni kazi kama kazi zingine,
Umachinga ni kazi kama kazi zingine,
Udalali ni kazi kama kazi zingine,
Ukuli na upiga Debe ni kazi kama kazi zingine
Ni MTU mpumbavu na mjinga asiyeelewa mambo hayo.
Lena anadharau sijui Vikoba kisa Watu wanachanga Bukubuku au elfu tatu, hizo Pesa zinazochangwa sio Pesa za wizi, ni pesa halali, hawajamuibia MTU. Ni jasho Lao, dharau na Kiburi sio Kizuri.
Kwa Watu waungwana, wasomi walioelimika, Wenye maadili na hofu ya Mungu huwezi kuwasikia wakiongea mambo ya hovyo kama hayo.
Lema kama MTU ajionaye mwenye Akili, Exposure na aliyewahi kuwa Kiongozi Kwa nafasi ya ubunge, pamoja na Sisi wasomi na watu WA serikali pamoja na viongozi wa dini tulipaswa kufanya haya yafuatayo;
1. Kuzitambua kazi Mpya zilizozuka hivi karibuni kutokana na mapinduzi ya teknolojia na Ujio WA utandawazi..
Kazi kama za bodaboda, umachinga, kazi za mitandaoni, kazi za udalali n.k Ni muhimu kuzitambua.
2. Kuziwekea Sera, sheria na Kanuni ili kuwapa Haki na fursa watakaojiingiza humo.
3. Kutunga na kuingiza mitaala ya kozi fupi na ndefu zitakazofundisha kazi hizo Kwa gharama nafuu,
Ili kuzipa thamani kazi hizo, kupitia Elimu na sheria zitakazotungwa kutakuwa na Maadili ya hizo kazi.
Utoaji wa Elimu utasaidia kazi hizo kutokufanywa kiholela,
Kutawafanya wafanyaji WA KAZI hiyo kuwa nadhifu kimavazi, pia utumiaji wa Lugha fasaha na zenye nidhamu utazingatiwa kwani ni sehemu ya Kazi.
4. Kuandaa mfumo wa bima ya afya Kwa gharama nafuu inayolingana na kipato cha kazi hizo. Bahati nzuri siku hizi Ipo Ile bima ya CHIF ya elfu 40.
5. Kuandaa mifumo ya ulipaji wa Kodi au ushuru kulingana na eneo la kazi. Hii ni kumfanya kila MTU awajibike kuijenga nchi.
Kwa mfano bodaboda akilipa elfu hamsini Kwa Mwaka kama Kodi haiwezi kumshinda.
Hata hivyo Pesa hiyo lazima iingizwe moja Kwa moja kwenye Leseni ili kuepusha usumbufu.
Leseni na Kodi isizidi 100,000/= Kwa upande wa Madereva bodaboda.
Kama dereva bodaboda ni wakuajiriwa basi watashare yeye na bosi wake gharama ya Kodi, huku Leseni ikibaki kuwa wajibu wa dereva mwenyewe. Mfano kama Kodi ni 50,000 Kwa Mwaka basi Mmiliki wa bodaboda atalipia 25,000/= na dereva bodaboda atalipia 25,000/= Kwa Mwaka. Huku gharama za Leseni ikibaki kuwa ya dereva.
6. Angalau kila Mwaka itolewe semina ya Madereva bodaboda, na mafunzo Kwa Madereva bodaboda Kwa ngazi ya Kata.
Kazi Hii waifanye Polisi Kata wakipewa Posho Kwa kazi hiyo watakayoifanya.
7. Iundwe Programu ya kuhamasisha Watu kupenda kazi zao bila kujali wanapata kiwango gani cha fedha
Na iundwe sheria NI marufuku Kwa mtu kutoa maneno ya kashfa Kwa kazi zingine, yaani maneno ya kutusi, kudharau na kujeli kazi zingine, ili kukifanya kizazi kinachokuja kisije Kukua na KASUMBA Mbaya kuhusu baadhi ya Kazi.
Kudharau kazi za wengine ni chanzo kikuu cha janga la ajira.
8. Kutokana na nchi yetu bado ni Maskini kazi za umachinga haziepukiki, utaratibu maalumu hasa katika ngazi ya serikali za mitaa uundwe ili kuhakikisha unasimamia machinga katika maeneo waliyomo nje ya katikati ya jiji.
Wawekewe Muda maalumu wa kuendesha shughuli hizo Kwa Kupanga pembeni ya Barabara sehemu ambazo ni salama (nasisitiza sehemu ambazo ni salama)
Kwa mfano kuwaruhusu wafanya shughuli hizo kuanzia saa 11;00jioni mpaka saa 4:00usiku Chini ya masharti yafuatayo;
1. Kuhakikisha eneo hilo ni Safi Kabla na Baada ya biashara
2. Kutokupanga biashara kwa wapita Njia.
3. Kutoa ushuru kila Siku labda ni Buku, au kiwango chochote kulingana na eneo bila kutoa excuse yoyote ya sijui sijauza au nimeuza.
4. Kutokujenga kibanda chochote eneo hilo.
5. Kufanya biashara Kwa muda uliopangwa na serikali.
6. Kuuza bidhaa halali
7. Kuuza bidhaa zenye thamani itakayowekwa na serikali kama itakavyoona inafaa, labda tuseme bidhaa zitakazopangwa Barabarani ziwe bidhaa ndogondogo mfano nguo, matunda, maji n.k na sio MTU aweke biashara yenye mtaji wa mamilioni ya Pesa
8.. kulipa faini ya kiwango kitakachowekwa na serikali au kufukuzwa eneo hilo na kutopewa eneo jingine ikiwa atavunja Kwa Makusudi taratibu zilizowekwa n.k.
Kitu kikubwa ambacho Lema angekisema ni kuiambia, au kuilaumu serikali Kwa kushindwa kuwasaidia hao wenye hizo kazi anazoziita ni zalaana. Na sio kuwaponda Watu walioamua kujishughulisha Kwa shughuli halali.
Au anafikiri kuwa mwanasiasa Kwa kupiga mdomo na kubwabwaja kwenye majukwaa ndio kazi ya baraka? Au kazi Bora kuliko kazi nyingine.
Kila kazi ni Bora itategemea na mtazamo wa anayeifanya.
Wapo Watu ambao hata uwaambie wawe wabunge hawatotaka kuwa wanasiasa.
Kudharau kazi ya MTU mwingine au kipato cha MTU mwingine ni dalili ya kutokuwa muadilifu, dalili ya kiburi na ushamba Fulani hivi.
Unadharau kazi ambayo kuna Watu wanaendeshea familia zao, wanatoa Sadaka Kwa miungu Yao, wanahudumia Watu katika maeneo Yao. Wewe Kwa Akili yako ndogo unawakejeli.
Watu wanatafuta Maisha mazuri lakini Kupata Pesa nyingi haimaanishi ndio Maisha mazuri. Maisha mazuri ni Kupata kipato halali Kwa kazi halali, Kwa jasho lako,
Tuache kudharau Watu na kazi zao.
Ujumbe huu umemtumia Lema kama mwakilishi wa Watu wote wenye dharau na kejeli na Kiburi, sio Kwa Lema pekeake.
Nawatakia Sabato NJEMA.
Ni yule Mtibeli,
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kazi kama Changudoa ni laana
Huwa nakuona kama mtu unayeandika baada ya kufikiri kumbe sivyo.Hajui political climate ikoje...
Watu washachoshwa na siasa za harakati...na kushambuliana ..
Very soon watamchoka
Bodaboda Sio kazi ni kuangaika,
Hakuna mtu anaenda kutoa sadaka ya shukrani kwa kupata kazi ya bodaboda.
Angalia kinachowapata boda wa Kenya.
Lema Mcanada ... bado hajasema kuishi Tanzania ni laana ...
Huku alimlilia Kikwete arudi Tz...
Limbukeni la Canada
Nyie mnaona ni mambo ya mzaha ndio maana mnakejeli waliyopitia wapambanaji hawa.Wakichafua hali ya hewa, wanakuja na yale ya kuonewa huruma.
[emoji56][emoji56][emoji56][emoji28]
Aikambe! Baibui tena, kwahiyo hata miziki yake kwenye ndinga ilikuwa ya mimbo ya kimduara duara!
Wacha nijichekeshe
Chawa wake watakuja kukumwagia mapovu
Mbona hata Mimi Lofa namiliki mgodi? Au unaposikia mgodi unaelewa nini?Lema ametumia platform alipewa na ccm kuropoka uongo mwingi mwingi sana,sijali huo uongo wake kwasababu haubadilishi ukweli wowote
Ila ninachotaka kusema lema anaongea uongo wa kumiliki mashimo kumbe ni uongo hana shimo ila alipokea pesa ya waarabu flan ili yeye awe front
Na kwenye mashimo ameweka majina ya ndugu yake ili kukwepa kodi kwasababu anadaiwa madeni mengi
Lema aliyekaribia kufilisika kukaribia Hadi kuuza nyumba ya kuishi kutokana na mamikopo yake aliyokopa kichwa kichwa yakala mieleka
Lema usiongee bla bla game ndio kwanza linaanza,kesho ni njema sana kwa watu unaowadhani wabaya kwako
Lamba asali kimya kimya
Unaongea kitaarabu nani wa kukuelewa. After all si kila mtu ni mlamba asali. Wengine hutegemea juhudi zao. Acha kujidhalilisha.Lema ametumia platform alipewa na ccm kuropoka uongo mwingi mwingi sana,sijali huo uongo wake kwasababu haubadilishi ukweli wowote
Ila ninachotaka kusema lema anaongea uongo wa kumiliki mashimo kumbe ni uongo hana shimo ila alipokea pesa ya waarabu flan ili yeye awe front
Na kwenye mashimo ameweka majina ya ndugu yake ili kukwepa kodi kwasababu anadaiwa madeni mengi
Lema aliyekaribia kufilisika kukaribia Hadi kuuza nyumba ya kuishi kutokana na mamikopo yake aliyokopa kichwa kichwa yakala mieleka
Lema usiongee bla bla game ndio kwanza linaanza,kesho ni njema sana kwa watu unaowadhani wabaya kwako
Lamba asali kimya kimya
Lakini mboga mboga hawataki kusikia hayo!!Kwenye psychology kuna kitu kinaitwa "allow the victim to vomit" Hivi haya mambo kina Lema wangeyasemea wapi Kama sio kwenye majukwaani ya mikutano ya kisiasa na kwenye media? Je awamu ya tano ingewezekana? Clouds iliyovamiwa na Bashite na Nape kufukuzwa uwaziri ingeweza kufanya mahojiano live coverage na Lema? Hivi tunakosa kabsa akili ya kuelewa kuwa Lema anatema nyongo ikizingatiwa alishakaa gereza la Kisongo Arusha zaidi ya miezi minne kwa kosa la kuota ndoto kuwa Magufuli akiendeleza unyanyasaji Mungu atamchukua. Hatujui Sugu alisha kaa gerezani? Badae alifatwa na Dr Kitila Mkumbo akishawishiwa kuunga Juhudi akagoma badae kina Pole pole wakampelekea plain cheque imesainiwa tu yeye aandike amount tu akagoma hotel yake ikapigwa x kwamba ibomolewe hapo bado Mbowe akikusimulia kuanzia bill canas mpaka kule Machame kwenye mashamba yake utashangaa. Mambo waliyofanyiwa upinzani awamu ya tano hawatakuja kuyasahau kamwe ni kama vile mwanaume aliyegundua na kushuhudia mke wake kamsaliti sasa anajaribu kumsamehe na kusahau HAIWEZEKANI KAMWE.
Hajui hata alisemalo, hii migodi ya Primary license jamaa anaona labda ni big deal.Hana migodi ?au ana migodi kaweka majina ya ndugu zake? Which is which?
Shughuli yoyote ikishaharamishwa haitwi Kazi.
Vijana mlienda kusomea ujinga
Akili za aina hii zitakuzuiaje kuwa kama yule askari wa Zenji?Tajiri aliyekuwa akiongoza kwa kukopa bungeni. Sasa hizo hela za migodi na biashara zote alikuwa anapeleka wapi.
Viongozi wa chadema wana story au hiyo migodi yake ilikuwa aitemi.
Lema mtu wa fantasy sana mara hii baada ya kutoka ulaya anashangaa struggle ambazo juzi alikuwa anaona kawaida.
Mtu ambae alikuwa akitaka kumuua kila mara alikuwa anaenda halipo, mara kadhaa Lema alikuwa sehemu ambazo Magufuli yupo atawenzake wakisusia na Magufuli akimwita anaenda mbio kakenua meno yote.
Hila watu wanavipaji vya uongo.
Lissu naona baada ya kuona hawana mpango na kushindana uchaguzi ujao kaone bora asepe awaachie utapeli wao hakina Mbowe, nyonyo anayopata Belgium inatosha kuendesha maisha.
Punguza akili kuganda!! Kila jambo lina conclusion zake kweny vyombo husika!! Acheni waseme waliyopitia ili nafsi zao ziridhike, mnaumia juu ya wao kusema wengi wenu ni wahusika wa mauaji na utekaji!!Wewe yanakusaidia nini au yanabadilisha nini kwenye hii bei ya mchele iliyopanda
Alikuwa kafungwa mdomo muda mrefu ni muda wake wa kuongea sasaLema imekuwaje? Mbona kama vile kawa kichaa?