Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Lema ameonesha dharau kubwa sana kwa vijana

Yaani kuishi tu CANADA muda mfupi imekuwa nongwa na angepewa uraia kabisa huko?

Amekuwa Mpumbavu na atakosa kura nyingi kwa vijana, vijana wa Arusha wana misimamo sana
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ni mjinga tu ndio ataona Lema amekosea..
kwa nini kuna western countries na third world countries?
Western countries sababu kodi za wananchi zitatumika ipasavyo. Miundo mbinu ni kipaumbele. Usafiri wa public ni wa uhakika.. sasa huku kwetu usafiri wa bodaboda ndio tunajivuninia.. Hakuna ajira kwa sababu ya uzembe wa viongozi…

Yes bodaboda ni laana.. Watawala wajifambue waache matumizi mabovu ya pesa za wenyewe….

Ajira ndio wimbo Mkuu kwa vijana sio bodaboda…

Nchi ina resources za kutosha lakini hakuna ajira kutwa kukopa…
Watawala hawasikii
Kuna nadini kuna vyakula kuna vyanzo vya maji kuna ardhi nzuri kuna vivutio vya wataliii lakini ni maskini wa kutupwa…

Lema yupo sahihi … read between the lines utamwelewa. Kaza ubongo uelewe anamaanisha nini.

Lema kanyaga twende.. Ukweli mchungu

Thank you
 
Inaleta mtafaruku, sintofahamu, mikanganyiko nk, ukimya unapotamalaki kwenye mambo ya msingi yanapohitaji ufafanuzi.

"Zijibiwe hoja zote zinazoibuliwa dhidi ya chama na hasa zinazotokea ndani na zenye kuweza kuleta mkanganyiko"

Tumesafiri sote tukiipita milima na mabonde. Hatimaye tukalitambua tatizo letu kuu kuwa ni katiba ya nchi. Tukajiridhisha kikamilifu kuwa:

1. Kupata katiba mpya ni lazima iwe kipaumbele.
2. Kusifanyike uchaguzi mkuu tena bila ya kuwa na katiba mpya.

Tukiwa kwenye kuusuburi mpango mkakati wa kuyafanikisha mawili haya, lugha zinaanza kubadilika. Wengine wakianza kutangaza nia. Kwa uchaguzi upi?

Maswali ya kujiuliza:

1. Tumeachana na hoja yetu iliyotuimarisha muda wote ya kudai katiba mpya kama kipaumbele?
2. Tumeachana na hoja yetu iliyotuheshimisha ya bila katiba mpya hakuna uchaguzi mkuu?
3. Kama #1 na #2 hapo ni ndiyo, nini tofauti yetu leo na wadada 19 walioko bungeni kwa jina la CHADEMA bila ridhaa ya chama?

Izingatiwe hakipo kisichowezekana chini ya jua panapo mpango mkakati (action plan) thabiti.

Tupeane mwongozo tafadhali. Biashara asubuhi.
 
Unashangaa kuacha hoja ya KATIBA MPYA? Wewe jamaa sijui umeanza kufuatilia siasa lini!!! Vipi kuhusu hoja ya UFISADI iliyotoswa 2015??? Unaweza upo na nia nzuri, bahati mbaya sana umejiside na WAHUNI, and inashangaza sana mtu mwenye akili timamu yupo tayari kuikabidhi nchi kwa Mbowe, Msigwa, Lema, Sugu
 
Lema kazingua. Najua ana ujumbe lakini Je anafahamu kama waTz wengi akili ndogo hawana muda wa ku reason?
Hilo ndilo kosa kubwa alilofanya, mimi kama mimi nimemuelewa, lakini vipi kuhusu mwananchi kule MPITIMBI Songea vijijini? Ataweza kudadavua hiyo kauli kama siye hapa?
 
Unashangaa kuacha hoja ya KATIBA MPYA? Wewe jamaa sijui umeanza kufuatilia siasa lini!!! Vipi kuhusu hoja ya UFISADI iliyotoswa 2015??? Unaweza upo na nia nzuri, bahati mbaya sana umejiside na WAHUNI, and inashangaza sana mtu mwenye akili timamu yupo tayari kuikabidhi nchi kwa Mbowe, Msigwa, Lema, Sugu

Yanakuhusu vipi wewe haya tokea Lumumba? 🤣🤣
 
Haya mambo muhimu yafanyiwe kazi mapema na Chadema, kwangu sioni kama wana muda wa kupoteza tena.

Kwasababu kutoka leo mpaka 2024 kwenye uchaguzi wa SM ni mwaka mmoja umebaki, na kutoka kwenye uchaguzi wa SM kuelekekea uchaguzi mkuu 2025 nao ni mwaka mmoja uliobaki.

Sasa kwa tofauti hiyo ya mwaka mmoja uliobaki, kwangu naona kuanzisha mchakato wa kuipata Katiba Mpya ni muda mfupi, huo mchakato kimsingi ulitakiwa uanze juzi, wala sio jana.

Kwasababu hii michakato tumeshaona kule tulipotoka, mara nyingi huibua makundi kinzani ambayo hutetea maslahi hao, sasa mpaka kuyaweka sawa haya makundi, lazima muda unahitajika.

Kuhusu hao walioanza kuonesha nia ya kugombea ubunge 2025, hawa inawezekana wameshajua nia ya chama chao ni kutuzuga wananchi, au wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.

Kama wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi, basi tutarajie kuibuka kwa Covid wengine wapya ifikapo 2025, na hawa wataibuka kwa sababu wanaiona nafasi ya kushinda uchaguzi awamu hii ni nyepesi ...

Hivyo wametanguliza matumbo yao, kama walivyokuwa wale wanawake 19, hawaiwazi tena kesho yao kama atatokea kiongozi mwingine wa sampuli ya Maguful, hapa ndipo zitathibitika tabia za wanasiasa wetu, ni maslahi yao kwanza, mengine ni majaliwa.
 
Katiba mpya, nzuri itapatika ikiwa Chadema itakuwa na wawakilishi Bungeni, huwezi pigana ukiwa nje ya ulingo.

Wingi wa chadema bungeni utaipa uzito hoja yao kama 2010-2015

Bila uwepo wao hata mawazo yao hayatasikika. Wakisusa ACT inapata nafasi
 
Lema ameelekeza kampeni yake nyumba Kwa nyumba Karatu, hii NI ngome kubwa Kwa chadema. Je, atamtembelea Dr. Slaa kimya kimya nyumbani kwake au watapanda wote jukwaani?

Kama anaweza kwenda gerezani kumwona Sabaya kwanini asiende kumwona Dr. Slaa? Je, utakuwa msimamo wa Dr. Slaa kuhusu bodaboda na Vicoba? Ataungana na Lema au watatofautiana kifikra?
 
Lema mara zote wanasema ukiwa na hasira sana usiongee lolote .lakini pia ukiwa na furaha jizuie usiongee chochote! Hiyo ndio ilimtokea lema akiwa jukwaani ,kelele za washangiliaji zikamwondolea hekima zikamletea kichaa akajikuta anaanza kulaumu hata watu ambao sio sehemu ya ajenda ya mkutano!! Mfano anamwambia mchungaji na nabii geordavie kwamba alikosea kuwasaidia wananchi badala yake angekarabati kanisa lake ! Hiyo haikuwa na mantiki yoyote kwenye hotuba yake !! Pili anadai biashara ya boda boda ni laana ! Anasahau Ile biashara ni kama biashara zingine !! Anataka kutuambia wanaoagiza pikipiki nje waache kuziagiza kwa kuwa ni laana! Anataka kusema maduka ya pikipiki kariakoo na nchi nzima yafungwe kwa sababu ni laana . Labda alitaka kusema makampuni yapikipiki yaache kuiuzia Tanzania pikipiki kwa kuwa ni laana ?? Watanzania wangapi wanaendesha maisha Yao kwa kutegemea pikipki na bajaji ! Ni Kodi kiasi Gani serikali inapata kwa biashara ya pikipiiki. Lema hotuba Yako imekuondolea heshima mtu mzima huchutama waombe radhi bodaboda nchi nzima maana umewatukana!!!
Mkuu umelenga Ukweli mtupu hapo!
Msikilize hapo chini katika sehemu tofauti tofauti za hotuba yake......


 
Msikilizeni kwenye hixi video clips na mtaelewa ninachomaanisha!



Wale wa mapovu na mioshi mingi tukutane pia
Maana watu makini huishi kwa tafakuri!
hqdefault%20(1)_remastered.jpg
 
Back
Top Bottom