Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Siasa ni Sayansi,Siasa pia ni hesabu inabidi kuwa makini sana na maneno na pia namna ya kuzungumza hayo maneno.
sayansi haidanganyi. wewe sema awe kama akina magufuli wanamtukuza mungu kumbe ni wauaji, akina Kabudi wanasema tusibagaze nchi kumbe wanatorosha fedha uchina.

Lema naye awe hivyo sema uongo waambie bodaboda mtakuwa matajiri wakubwa kama Bill gates kwa kazi hiyo,basi maisha yaendelee
 
Uyo ni Lema tu ndio anawanyima raha na bado ajaanza kuhoji katiba mpya na tume huru sjui akifika hapo ndio mtasemaje
 
Na kama kazi ya bodaboda ni laana na wanaozitumia pia wana laana. Kuna kundi kubwa sana linafaidika na bodaboda, kuanzia wafanyakazi wa viwandani, maofisini, wachuuzi, mama ntilie, wakulima, wenye maduka n.k.

Amefanya kosa kubwa sana kutumia maneno hayo. Unapozungumzia jambo kama hilo angalia upana wake. Kwa mfano zikipigwa marufuku ndiyo utajua umuhimu wao.
 
Toka ametoka nje sijamuelewa maneno yake anaongea vitu ambavyo kisiasa siyo muhimu wala lazima kuvisema,kiufupi havina tija wala maslahi yoyote kwa chama chake...
Acheni uoga, uoga ni kuwa madhambi yatawekwa hadharani, kilichobaki tubuni madhambi kwa vinywa vyenu wenyewe kabla ya kumwagwa hadharani 😂
 
Waambie bodaboda kuwa kazi yenu ni nzuri inalipa, mtakuwa matajiri wakubwa. Endeleeni kwa bidii, itawatoa. Wanataka kusikia hilo.

Kitokacho mdomoni hakirudi: ufanyeje: waambie nimebadilisha maoni, Mungu amenifunulia na kuniotesha. Kazi yenu imebarikiwa, mtakuwa matajiri wakubwa. Umemaliza mkwaruzano/ mtifuano.
 
Asimame tu na hoja yake na kukazia alichokimaanisha.

Btw, hata akibadilisha haitaondoa ile tafsiri ya kwanza...sana sana kutamfanya adharaulike zaidi.
Tanguliza Mungu kuwa umeoteshwa, watanzania watabadilika! Kama wanawaamini wahuni kuwa ni manabii/watume wa Mungu why not him! Watu wanaamni kukanyaga mafuta kutawaletea neema hao waambie lolote husisha na mungu watakufuata
 
Huyo mchizi mimi ananishangaza kakaa Ulaya mwaka mmoja tu anajifanya anajua na kwamba ana majibu ya mambo complex, kuna watu wameishi USA au Ulaya kwa Wazungu miaka hata 40 na wako kimya yeye mwaka tu tayari anajiona anajua kila kitu, na ana majibu yote.
 
Bora Lema amekaa mwaka 1 amejionea maendeleo ya canada,je wewe umeshawai fika hata Malawi?
 
Sasa si ndio kashangaa inakuaje watu wanaishi kwa kufanya kazi hatarishi namna hii? Wewe ukienda huko Canada ukakaa hata wiki tatu tu nakuhakikishia ukirudi utakua unashinda unaporomosha matusi tu humu kuwaambia watu ukweli kama anao sema Lema
 
Bora Lema amekaa mwaka 1 amejionea maendeleo ya canada,je wewe umeshawai fika hata Malawi?
Ananikumbusha kitabu tulisoma Sekondari cha Mwandishi Mnigeria nafikiri alikuwa Chinua Achebe kilimhusu jamaa aliyesomeshwa na kijiji mpka Chuo kijiji kikamlipia kwenda Ulaya ili akirudi aje kuwasaidia matokeo yake aliporudi akaanza kashfa na kejeli dhidi ya wanakijiji, amenikumbusha mbali sana, …
 
Sasa si ndio kashangaa inakuaje watu wanaishi kwa kufanya kazi hatarishi namna hii? Wewe ukienda huko Canada ukakaa hata wiki tatu tu nakuhakikishia ukirudi utakua unashinda unaporomosha matusi tu humu kuwaambia watu ukweli kama anao sema Lema

Walikuwa wanamuita Magufuli mshamba lkn ukiangalia wao (Lema & Co.) ndiyo washamba kwa maana halisi ya neno ushamba, hamna ushamba zaidi ya huu wa Lema.
 
Back
Top Bottom