Niwapongeze CHADEMA kwa namna wanavyojua kupangilia Matukio yao ya kisiasa kwa ubunifu na pia kuweza kumantain kuaminika na Watanzania wengi hadi sasa.
Ila lazima tukubali ukweli kuwa kuna Platform wanaziandaa vizuri wanapata watu wengi sana ila wanashindwa kuzitumia vizuri sana ikiwemo ya Mapokezi ya Godbless Lema na uzinduzi wa Mikutano ya hadhara Mwanza.
Niwapongeze walivyotumia Platform ya Mapokezi ya Lissu vizuri na kufikisha vyema ujumbe wa Katiba Mpya bila kuchanganya Mambo na ukafika vizuri sana.
Nimefuatilia mapokezi ya Godbless Lema yalienda vizuri na alifanikiwa kueleza vizuri sababu ya kuondoka ila hoja Kuu kama umuhimu wa Katiba Mpya hazikupewa uzito wa kutosha katika jukwaa muhimu kama lile, pia kuna Maneno ambayo Godbless aliyasema hayakuhitajika kusemwa kwa waliofuatilia vyema mtanielewa.
Ni wakati sasa Team ya CHADEMA inayoandaa Matukio haya kuhakikisha wanawaandaa Viongozi wake vyema kutumia vizuri Platforms hizo kusukuma kwa uzito Agenda Kuu za Chama.