Wakuu natanguliza salamu , poleni kwa Ugumu wa Maisha unaowakabili nchini Tanzania kwa sasa , , basi baada ya pole hizo naingia moja kwa moja kwenye mada
Ile siku iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Wananchi wa Arusha , imekwisha wadia , Unaambiwa usiku wa deni hauchelewi , yaani ukieagama tu kumekucha !
Taarifa kutoka kwenye kamati ya Mapokezi inaonyesha kwamba ndege ya ETH 815 aliyopanda Lema ambaye pia anatambulika kama Nabii wa Mungu , kutokana na unabii wake wote kutimia , imeondoka Addis Ababa , Ethiopia saa 4:40 asubuhi hii na inatarajiwa kutua KIA saa 6:39 mchana .
Tayari njia zilizotangazwa kutumika kwa ajili ya msafara huo Mkubwa na unaotarajiwa kuvunja rekodi , zimekwisha furika Wananchi , huku wengi wakiwa wanapeperusha bendera za Chadema na matawi ya miti , kiukweli shamra shamra ni kubwa kiasi ambacho kimewafanya baadhi ya WATALII KUAHIRISHA KUTEMBELEA MBUGA ZA WANYAMA , huku wakijawa na Shauku ya kutaka kumuona mtu anayesubiriwa kwa kiasi hicho .
Kama kawaida
Erythrocyte atawaleta kila kinachojiri .
Usiondoke JF
==========
UPDATES :
Inasemekana Rais Samia naye ametua Arusha , ila bado haijajulikana kama naye atashiriki Mapokezi hayo au ana shughuli nyingine .