Pre GE2025 Arusha: Zimebakia siku 6 tu kabla Neema ya Maandamano ya Amani

Pre GE2025 Arusha: Zimebakia siku 6 tu kabla Neema ya Maandamano ya Amani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 2911091

Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba yale Maandamano yaliyoletwa na Mungu , ya kupinga Dhiki , Ufukara , Ugumu wa Maisha , Bei kubwa ya bidhaa zote ikiwemo Vyakula , pamoja na kupinga miswada mibovu ya sheria za uchaguzi , Maandamano yanayoandaliwa na Chama chenye Maono CHADEMA , Sasa yameingia Arusha .

Wataalam wa kuhesabu namba baada ya kujua kwamba Maandamano hayo makubwa yamepangwa kufanyika tarehe 27 /02/2024 na baada ya kufahamu kwamba leo ni 21/02/2024 , Wamedai kwamba zimebakia siku 6 tu kabla ya shughuli hiyo kubwa kufanyika .

Usiondoke JF , maana mtumishi wako Erythrocyte atashiriki na atakuletea kila kinachojiri , ikiwemo taarifa za wote wanaoingilia Maandamano hayo kwa shari kama alivyofanya Biteko Mbeya .
Zile sauti za Speaker na vipaza sauti mjioange mnazingua bwana
 
Back
Top Bottom