Kuna hosp nilikuaapo wakat nipo Internship , Kwa siku wagonjwa wapya wa huu ugonjwa walikua wakigundulika 20--30 kila siku.
Kwa CTC sasa ndo usiseme
Muhim watu watumie ndom, nahata ukigundulika Nivema Uanze dawa ,dawa zinaongeza maisha marefu na kupunguza usambazaji.
Mimi nikiwa kavulana nilikuwa na jimama langu linanilea, kuna siku lilisafiri kibiashara, likaniachia nyumba niwe muangalizi,
Sijui kitu gani kilifanya nipekue pekue kule chumbani, bahati mbaya/ nzuri likasahau kufunga dro ya kabati.
Si nikakumbana na mikadi ya mahudhurio yameandikwa CTC
Yalikuwa ya kuchukulia dawa. Nilichanganyikiwa ,asubhuhi na mapema nikayabeba makadi hadi hiyo hospitali yenye hiyo kriniki,ilikuwa hospitali ya wilaya.
Wakanijibu huyu mtu anahudumiwa hapa miaka mingi tu, ni nani yako? Nikawambia ni mpenzi wangu,wakashangaa, wewe kijana limama lote lile la nini? Itabidi tukupime mara tatu kila baada ya miezi mitatu.
Lakini kwakanionya sio vizuri kupekuwa na kubeba vitu binafsi vya watu bila ridhaa yao.
Nilipima majibu yakawa safi ,sikupata maambukizi.
Sasa bhana wakati natoka nimeshika makadi yale nakuta watu kama 100+, wana kama mkutano hivi,waliponiona na zile kadi wamama wakajishika kichwa kwa mshangao.
Nahisi walidhani ni mtumiaji wa yale madawa nakipindi hiko nilikuwa mvulana mdogo.
UKIMWI upo ,tena watu wengi mitaani wanao.
Jinsi alivyorudi na kumpa taarifa ,na jinsi mama alivyolipokea ile taarifa,hiyo ni kesi ingine,pale ndio nilijua uchungu wa mwana aujuae mzazi[emoji38][emoji38][emoji38]