Huu uzi watu wanajadili ki-layman sana... Badala ya kujadili kwa mapana na marefu ili ufaidishe jamii iliyomo humu. Na yote imechangiwa na mleta uzi kuugeuza kuwa wa "kimipasho" sana...
Kwa sisi watu wa medical field mngeweza ku-benefit masuala juu ya uhalisia... Mjue watu humu JF, tuna-type, na tuna-enjoy maisha humu, lakini tunadanganyana sana... Wengi tunajifanya tuna maisha mazuri, kama hivi tunajifanya hatuumwi(as if wanaoumwa, huo ugonjwa waliuleta wao, wakati wao wenyewe wameambukizwa), na mengine kama hayo. Tunaishi maisha ya mtandaoni ambayo si uhalisia wetu.
Sasa na wao wapo humu na wamekuwa "carried away" na mkondo mbaya wa mjadala.. Wakati wana uelewa zaidi ya mtunga uzi.
Kifupi napinga na ni uongo mkubwa kuwa ARV zina shida katika matumizi. Labda mtoa uzi arudi aseme, hiyo taarifa aliipata wapi, kwa nani, na lini.