ARV uzisikie kwa wenzako, tutumie condom

ARV uzisikie kwa wenzako, tutumie condom

Wakuu suala la kumeza ARV kwa maisha yako yote toka kugundulika umeathirika usikie tu kwa jirani. Siku za mwanzo maluwe-luwe Kama yote. Tuache ngono zembe. Vaa kondomu ndugu, ule utelezi na joto-joto litakugharimu.

UPDATE
Kama umeoa bora kumtaarifu mapema mwenzio maana siku ukibumbuluka aibu yake unaweza kujaza shazi mtaani.

**Wake zetu wagalatia si unajua vichwa vibovu
!
mzee pole, ushaukwaa?
 
Juzi tumezika chalii bado kinda kasa alizaliwa nao ametumia dawa since kichanga imefika mahali chalii kachoka kula tembe kila siku kapiga chini dawa kujikuta yuko ICU siku saba na mauti ikamkuta.
Jamn huu ungojwa usikie kwa mtu usiombe tuzid kutumia condom au kuacha umalaya itasaidia kupunguza
 
Kuna ndugu yangu alianza kulala makaburini alichizika kbsa kdgo tumalize zizi kwenda kwa waganga wapiga ramli, kumbe jamaa tayari kaukwaa mpka kuja kumpeleka Hospital mbona mda sana dah!ngoma noma sana ickie2 nyumba jirani,
 
Kumrudia Mungu, kujenga uhusiano mzuri na Mungu, kufanya anayotaka na kuacha aliyoyakataza ni MUHIMU SANA.

Wokovu na Neema ya Mungu kwetu ni vitu vya thamani sana. Tuache Uasherati na Uzinzi ni dhambi, na Mshahara wa dhambi ni MAUTI.
 
Kila unapopima ukakutwa safe unasema sifanyi tena,then unajikuta umefanya tena
 
Tunakumbushana sio kwa ubaya. Pasaka hii usiuze mechi, utajuta maisha yote
 
Ni kweli asilimia kubwa ya watu wenye O+ hawapati HIV kirahisi, nina mfano hai wa mtu wangu wa karibu kabisa, miaka hiyo yule bwana na mahawara zake kibao walishaiacha dunia kwa ukimwi ila yeye yupo hadi leo, kila akipima ni negative
Umechanganya madesa..haipo hivyo ni kweli wapo baadhi ya watu hawapati Ngoma kwa kua seli zao nyeupe hazina vipokezi vinavyosapoti HIV kuingia ndani ili afanye yake lakini sio kuzungumzia Magroup ya damu..GROUP LA DAMU HALINA CHOCHOTE KWENYE HIV KWANI YEYE HANA MPANAGO NA RBC(SELI NYEKUNDU ZA DAMU).
 
Back
Top Bottom